Saratani zinazowasumbua watoto.

Posti hii inahusu zaidi saratani zinazowashambulia watoto. Hizi ni aina mbalimbali za saratani ambazo upenda kuwasumbua watoto ambao ni chini ya umri wa miaka mitano na uleta madhara katika kipindi cha makuzi yao.

Saratani zinazowashambulia watoto.

1.Kwanza kabisa tunajua kuwa saratani ni Ugonjwa ambao utokea kwa sababu ya kuwepo kwa seli zisizohitajika zinaweza kutokea katika sehemu yoyote ile ya mwili . Kwa watoto Sababu za kuwepo kwa tatizo la saratani hazijathibitishwa bado ila kuna vitu ambavyo vinaweza kuchangia kama vile uvutaji wa sigara wakati wa ujauzito, pombe kali na mtindo wa maisha wa Mama kwa a ujumla wakati wa ujauzito unaweza kusababisha kuwepo kwa saratani kwa watoto. Kwa hiyo watoto wanashambuliwa na saratani zifuatazo.

 

2.Kuna saratani ya damu.

Aina hizi ya saratani utokea pale ambapo mtoto anakuwa anaishiwa na damu mara kwa mara inawezekana kupitia sehemu yoyote kama vile puani au inawezekana isipite sehemu yoyote ila mnaongeza damu ila baada ya siku chache mtoto anaishiawa damu, aina hii ya saratani kama haijafahamika mapema inaweza kumchukua mtoto mara moja kwa hiyo baada ya tatizo hili kutokea wazazi au walezi wanapaswa kuwasiliana na wataalamu zaidi wanaohusika na Magonjwa ya saratani.

 

3. Saratani ya macho.

Pia ni mojawapo ya saratani inayowapata watoto unakuta jicho la mtoto linakuwa na uvimbe mdogo na kuwasha na kadiri mda unavyokwenda unakuta uvimbe unaongezeka na mtoto anashindwa kuona na kwa wakati mwingine unakuta jicho limetokezea kwa nje na kumfanya mtoto kuangaika kwa sababu ya kuwepo kwa maumivu makali kwenye jicho. Kwa hiyo wazazi na walezi baada ya kuona tatizo kama hili mnapaswa kumpeleka mtoto hospitalini mapema ili kupunguza ukali wa tatizo.

 

4. Kuna saratani ya mifupa.

Pia na hii ni aina ya saratani ambayo ushambulia mifupa kwa na kabisa mtoto uanza kusikia maumivu anapotembea na pia kadri siku zinavyoenda anashindwa kutembea kabisa kwa sababu mifupa uanza kusagika na kwa hiyo ukimgusa sehemu yoyote ile anaanza kulia kwa hiyo mtoto anaweza kuishi kwa kulala maisha yake yote na kushindwa kuendelea kukua katika hatua za makuzi ya mtoto.

 

5. Kuna saratani ya ubongo na ngozi.

Aina hii tena ya saratani uwapata watoto chini ya miaka mitano kwa sababu unakuta watoto wanakuwa kama zezeta na wanashindwa kukua katika hatua za mtoto na pengine mtoto hawezi kukaa na kusimamia viungo na pia macho yao huwa yanaangalia makengeza na pengine mtoto anashindwa kuwa na balance. Hali utokea kwa sababu ya kukosa mawasiliano kati ya ubungo na misuli.

 

6. Pia kwenye ngozi ya mtoto panakuwepo na ma upele ambayo hayaeleweki na hata yakitibiwa mara hali inajirudia kuna wakati mwingine ngozi ya mtoto inaweza kubadilika kwa namna moja ama nyingine, pengine ngozi inaweza kuwa nyeupe au pengine nyeusi zaidi na kwa wakati mwingine kuwa na rangi ya mabaka mabaka kwa hiyo ngozi ubadilika Mara nyingi kwa hiyo baada ya kuona hali kama hizi ni wazi kubwa hiyo ni kansa ya ngozi.

 

7. Kwa hiyo kwa akina Mama wanapaswa kujua kuwa saratani kwa kawaida yake ikionyesha Dalili za mwanzoni na mtoto akapelekwa hospitali  na tatizo likagunduliwa mapema anaweza kupona na kurudia kwenye hali ya kawaida kwa hiyo pindi mama akiona dalili hambazo hazieleweki kwa watoto anapaswa kufuata matibabu mara moja ili kuepuka madhara zaidi. Ila kwa walio wengi wanasubiri tatizo likiwa kubwa ndio wanakuja na kusema kweli tiba inakuwa ni shida na kupona kwa mtoto itakuwa bahati.

 

8.Kwa hiyo wazazi, walezi na jamii kwa ujumla inapaswa kupewa elimu kuhusu kuwepo kwa saratani kwa watoto na kuwaambia Dalili zake na pia wajue madhara yatokanayo na tatizo hili na pia akina Mama wakati wa ujauzito wanapaswa kufuata mashariti yote na kuachat na ulevi pamoja na uvutaji wa sigara, na kutumia vitu visivyofaa wakati wa ujauzito ili kuepuka matatizo ya saratani kwa watoto.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/03/10/Thursday - 09:19:18 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 823

Post zifazofanana:-