Saratul-humaza
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
- Suratul-Humaza (104): Imeteremshwa Makkah, Ina Aya Tisa.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
- Adhabu kali itamthubutikia kila mwenye kuramba kisogo, asengenyaye, msengenyaji.
- Ambaye amekusanya mali na kuihesabu (tu bila ya kuitumia katika njia za kheri).
- Anadhania kuwa mali yake itambakisha milele.
- Hasha! Bila shaka atavurumishwa katika (moto unaoitwa) Huttama.
- Na ni jambo gani litakalokujulisha (hata ukajua) ni nini (huo moto unaoitwa) Huttama?
- (Huo ni) moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa (kwa ukali bara bara).
- Ambao unapanda (mpaka) nyoyoni.
- Hakika watafungiwa ndani ya moto huo.
- Kwa manguzo marefu (ili wasiweze kutoka).
Mafunzo kwa Ufupi.
- Kusengenya ni katika makosa makubwa kabisa.
- Ni makosa makubwa kukusanya mali bila kuitumia katika njia za kheri.
- Matumizi mabaya ya ulimi na neema zingine hupelekea kwenye maangamizi na adhabu.
- Matumizi mabaya ya ulimi kama fitna, uongo, usengenyi, n.k. huleta chuki, husda na mtafaruku katika jamii.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 web hosting 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Sababu za kushuka surat an-Nas na surat al Falaq
Sura mbili hizi pia hujulikana kwa jina la al muawidhatain ambazo ni surat an Nas na surat al falaq.
Soma Zaidi...surat al mauun
SURATUL-MAM’UUN Imeteremshwa Maka, anasimulia Ibn Jurayj kuwa Abuu Sufyan ibn Harb alikuwa na kawaida ya kuchinja ngamia wawili kila wiki, hivyo siku moja yatima mmoja alikuja kwake na kumlilia shida, na hakumsaidia kwa chochote na hatimaye akampiga yat..
Soma Zaidi...Je, mtu anaweza kusoma quran akiwa amelala?
Kusoma Qur'an kuna faida kubwa kwa Muislamu, kwanza kunampatia thawabu, kunatoa nuru maisha yake, mwili wake na kumlinda na mashetani na watu wabaya. Quran ni dawa na pozo kwa magonjwa. Thawabu za Qur-an hulipwa kwa kila herufi. Quran pia huja kutet
Soma Zaidi...Aina za Madda twabiy kwenye usomaji wa Quran
Madda zimegawanyika katika maeneo makuu mawili ambayo ni madda twabiy na madda fariy
Soma Zaidi...