image

Siku za kupata ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata ujauzito

SIKU YA KUPATA UJAUZITO

 

Swala la kupata ujauzito limekuwa likikabiliwa na imani nyingia ambazo sio sahihi. Watu wengi wamekuwa wakipoteza muda na fedha kujaribu kutatua maswali yao. Leo nitakusaidia kutatua swali hili Je..! ni zipi dalili za mimba changa. Swali hili ni la msingi kwani kuna watu wengi wamekuwa wakichanganya dalili za ujauzito na shida nyingine za kiafya. Hapa nitajaribu kukufahamisha utofauti wa dalili hizi na nyingine ili upate kufahamu vyema.

 

Imani potofu kuhusu dalili za ujauzito:-1.Mimba inaingia siku yeyote ile. Hii sio sahihi kabisa mimba inasiku maalumu ambazo huweza kutungwa. Kitaalamu siku hizi zinafahamika kama fertile window2.Siku yya 14 ndio siku ambayo mimba hingia. Hii pia sio sahihi, kwani wanawake sio wote wanaingia siku 28, kuna wengine ni kati ya 21 mpaka 353.Unaweza kupima mimba kwa ktumia sukari, chumvi, mafuta, sabuni, delto. Hizi zote sio sahihi kabisa.

 

Ni siku gani mimba huingia.Mimba huweza kuingia siku ambayo yai litakutana na mbegu ya kiume kwenye mirija ya falopia kwenye tumbo la uzazi la mama. Yai la mwanamke kuzalishwa kwenye ovari. Mwanamke ana ovari mbili, moja upande wa kulia na nyingine kushoto. Hizi mbili hupeana zamu ya kutoa mayai. Yaani kama mwezi huu limetoa hili na nyingine itatoa mwezi ujao.

 

Tafiti zinaonyesha kuwa yai huweza kuanza kukomaa kuanzia siku ya 10 toka kupata hedhi mpaka siku ya 14. hii ni kwa wanawake wengi. Ila si wote. Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla ya kupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12 nyuma, kisha toa siku 4 mnyuma ndani ya siku nne zizi ndizo yai hutolewa. siku hizi ndizo moja wapo yai hutolewa. Kwa mfano:--

 

1.Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla ya kuingia hedhi (21 - 12 = 9) kisha toa nne nyuma (9-4=5) basi mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 5 na 9 katika siku zake.

 

2.Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kabla ya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku nne tena nyuma (20-4=16) kwa hiyo mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 16 mpaka 20.

 

4.Mwanamke mwenye siku 28: 28-12 = 16 kisha toa siku 4 nyuma 16 - 4 = 12. hivyo siiku ambazo yai hukomaa kwa mwenye siku 28 ni kati ya 12 mpaka 16.

 

Sasa baada ya kuzijua siku hizi ambazo yai hukomaa, inabidi ufahamu kuwa yai la mwanamke huweza kuishi kati ya masaa 12 mpaka 24 toka kukomaa (ovulation). kwa upande mwingine mbegu za kiume huisho kati ya siku 3 mpaka 5. hivyo ujauzito unaweza kutungwa kwa mbegu ambayo ilikuwepo toka siku tatu zilizopita.

 

NI IPI HASA SIKU AMBAYO NITAFUTE UJAUZITO?Kama ulipojifunza hapo juu kuwa zipo siku maalaumu ambazo yai hukomaa. Katika siku hizo mojawapo yai huletwa kwenye mirija ya falopia. Baada ya kukokotoa siku zako hapo juu sasa itakubidi kuongeza siku moja ama mbili nyuma. Hii ni kwa sababu makadirio ya siku hutofautiana. Na si lazima kkutafuta toto katika siku zote hizi. Unaweza kuruka kwa siku moja moja.

 

Jitahidi kufanya tendo la ndoa hasa katika siku hizo nne ulizozipata baada ya kukokotoa. Katika siku hizo jitahidi kufanya tendo siku ambayo itakuwa na sifa zifuatazo:-

 

1.Majimaji ya mwanamke ukeni yatakuwa ni mengi kuliko siku zilizopita. Mwanamke mwenyewe anaweza kujichunguza hali hii na kuigundua ila taabu. Anaweza kutumia kidole ama kitambaa safi kuchunguza uwepo wa majimaji haya katika ukeni kwake. Kumbuka hali hii isiambatane na shida nyingine za afya kama PID. Wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kuchunguza hasa kwa wale wanaotumia uzazi wa mpango hasa hasa kwa kutumia vidonge vya homoni.

 

2.Joto la mwanamke litakuwa ni kubwa kuliko siku nyingine. Joto hili sio homa, na lisiambatane na sababu nyingine kama maumivu ya kichwa, ama kutokana na kulala sana, ama misongo ya mawazo. Kikawaida siku ambayo yai hutolewa joto la mwanamke linakuwa kubwa hivyo akishiriki siku hii ujauzito ni rahisi kuingia.

 

3.Siku ambayo mwanamke atakuwa na hamu sana ya kushiriki tendo. Wakato ambapo yai hutolewa kuna homoni huzalishwa kwa wingi. Homoni hizi zinaweza kusababisha mwanamke kutamani sana kushiriki tendo zaidi ya siku nyingine.

 

Pindi mwanamke atakapojigundua kuwa siku hii ameipata basi ni vyema kushiriki tendo ndani ya siku hii ama siku itakayofata haraka iwezekanavyo, maana yai la mwanamke linaweza kufa ndani ya muda mchach masaa 12 mpaka 24





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2291


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Sababu za kutoona hedhi kwa wakati
Posti hii inahusu zaidi sababu za kukosa hedhi wakati mda wa kuona hedhi umefika ni tatizo linalowasumbua baadhi ya wasichana wachache katika jamii na hii ni kwa sababu zifuatazo. Soma Zaidi...

Malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama.
Posti huu inahusu zaidi malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama, ni huduma muhimu ambazo zimetolewa kwa akina Mama ili kuweza kuepuka hatari mbalimbali zinazowakumba akina Mama wakati wa ujauzito, kujifu na malezi ya watoto chini ya miaka mitano. Soma Zaidi...

MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA
Maumivu wakati wa tendo la ndoa kitaalamu huitwa dyspareunia. Soma Zaidi...

Madhara ya kutumia vidonge kwa akina dada vya uzazi wa mpango
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango kwa akina dada. Soma Zaidi...

Sababu za maumivu ya tumbo wakatu wa tendo la ndoa
Jifunze sababu kuu zinazosababisha kuhisi maumivu makali ya tumbo wakati wa kushiriki tendo la ndoa Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia kwa mtoto mara tu anapozaliwa
Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuzingatia kwa mtoto pindi anapozaliwa,tunajua wazi kuwa mtoto anapoanza kutokeza kichwa tu ndio mwanzo wa kuanza kumtunza mtoto na kuhakikisha anafanyiwa huduma zote za muhimu na zinazohitajika. Soma Zaidi...

Zijuwe Dalili za minyoo na dalili kuu 9 za minyoo
Utajifunza dalili za minyoo, sababu za minyoo na namna ya kujiepusha na minyoo. Dalili kuu 5 za minyoo mwilini Soma Zaidi...

Tiba ya awali kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID
Posti hii inahusu zaidi tiba ya awali kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID, tunaita tiba ya awali kwa sababu baada ya kupima na kugunduliwa kwamba una tatizo au changamoto ya PID ni vizuri kutumia tiba hiii baadae ndipo utumie dawa. Soma Zaidi...

Njia za kugundua kama mtoto amevunjika baada ya kuzaliwa
Post hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo mtoa huduma anaweza kuzitumia kuangalia kama mtoto amevunjika baada ya kuzaliwa. Soma Zaidi...

UTARATIBU WA KULEA MIMBA
Soma Zaidi...

Zijue sababu zinazosababisha kupungua kwa idadi ya mbegu za kiume
Kupungua kwa idadi ya mbegu za kiume kunamaanisha kuwa Majimaji (shahawa) unayotoa wakati wa kufika kileleni huwa na mbegu chache kuliko kawaida. Hesabu yako ya manii inachukuliwa kuwa chini kuliko kawaida ikiwa una chini ya mbegu milioni 15. Kuwa na idad Soma Zaidi...

Je bado unasumbuliwa na nguvu za kiume?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuondoa tatizo la nguvu za kiume Soma Zaidi...