SIRI YA KIFO YAFICHUKA


image


Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela


SIRI YA KIFO YAFICHUKA

Kijana akaanza kueleza kuwa huyu binti ni mkewangukabisa na ni mtoto wa mjpomba wangu, na huyo mjomba ni huyu mzee. Mimi na mkewangu tuliiishi vyema sana. Mkewangu alinipenda sana na miaka yote tulioishi sikuweza kumuona na tabia mbaya hata siku moja. Niliweza kuzaa nay watoto watatu. Siku moja alikuwa anaumwa, maradhi haya yali dumu kwa muda uliokaribia mwezi mmoja kisha akapata nafuu kidogo. Haikuchukuwa muda mrfu akaumwa tena baada ya siku kadhaa akapata nafuu tena.

 

Siku moja alinipa matumaini kuwa kuwa amepata nafuu sana. Sasa akaniambia kuwa ana hamu na tunda epo na hatokwnda kuoga mpaka ale tunda hilo. Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana mke wangu. Nilikwenda kumtafutia tunda epo popote pale. Nilihangaika sana kwenye mabostani mengi ya mjini. Lakini bila mafanikio. Siku hiyo nilirudi mtupu kwa mke wangu. Loo siku hiyo mke wangu hakwenda kuoga. Basi siku ilofata nikatoka tena kwenda kutafuta tunda epo. Wakati nilipokuwa nimekata tamaa kabisa ya tunda ndipo nikakutana na mze mmoja akanileza kuwa kuna mji matunda hayo yanapatikana. Basi nikafunga safari kulekea huko.

 

Safari ilinichukuwa siku tatu hata kufika na kurudi na nilinunua matunda matatu kwa gharama ya vipande 15 vya dhahabi. Cha ajabu niliporudi mke wangu hakuwa tena na hamu ya tunda epo. Lakini alichukuwa matunda yale na kuyaweka kwenye kabati. Siku tatu zikapita bil mke wangu kugusa yale matunda. Basi siku ya nne nilipokuwa mtaani nilikutana na kijana mmoja mtanashati sana akiwa na tunda la epo. Kijana yule nikamuuliza wapi amepata ili nikanunue mengine. Kijana akanieleza kuwa “nimepewa na mpenzi wangu kama zawadi, mumewe alikwenda mbali safari ya siku tatu kununua maepo matatu kwa thamani ya vipande 15 vya dhahabu. Na mkewe ambaye nimpenzi wangu wa siri akanipatia kama zawadi.

 

Niliposikia maneno haya nilistaajabu sana na kuvurugwa moyo wangu. Nilitoka mbio hadi kwa mke wangu. Nilipoangalia kabatini nilikuta tunda moja halipo na yamebakia mawili. Nilistaajabu na kuyasadikisha maneno ya yule kijana. Nilimkamata mkewangu na kmchoma kisu cha tumbo kisha nikamchinja na kumkatakata vipande na kuvifunga kama ulivyoona kwenye boksi. Baadaye nilianza kujuta sana na kulia sana.

 

Kitu cha ajabu siku ya tatu niimkuta mwanagu analia sana. Nilikuwa na uhakika kuwa hatambui kuwa kama mama yake nimemchinja. Basi nikamuuliza mwanangu kipi kinakuliza?. akanieleza kuwa “naogopa mama akirudi atanipiga, matunda yake matatu nimechukuwa mmoja, nikaenda nalo kucheza. Mkaka mmoja akaninyang’anya na kunipiga, nikamwambia kuwa ni la mama ameletewa na baba kutoka mbali safari ya siku tatu na amenunua kwa thamani ya vipande vitatu vya dhahabu. Yule mkaka akakimbia nalo” basi hapo hapo nikamwambia mwanangu anyamaze.

 

Dah nikagundua kuwa yule kijana alikuwa ni muongona ndiye chanzo cha kifo cha mke wangu. Niliia sana sanaaaa. Baba mkwe wangu ambaye ni mjomba wangu huyu hapa akaja. Nikamueleza kila kitu naye alilia sana. Hivyo khalifa mimi ndiye niliyemuuwa huyu binti, tafadhal niadhibu mimi niweze kulipa deni la nafsi ya mke wangu. Baada ya kusikia habari hii khalifa akamueleza waziri Mansur. “Nenda ukanitafutie huyu kijana, ninakupa siku tatu tu, na endapo hutamleta nitakuchinja kama alivyochinjwa huyu binti”.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    2 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    4 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    6 Hadiythi za alif lela u lela    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Deni la mapenzi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Hadithi ya kinyozi yeye mwenyew
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Kila kitu ambacho wanaume wanatakiwa kufahamu kuhusu wanawake.
Hii ni siri kubwa kuhusu wanawake. Hapa utajifunza jinsi ya kumfanya mwanamke asikuache. Soma Zaidi...

image Hadithi ya tabibu wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Jaribio la pili la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Mafundisho kutokana na hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mafundisho ambayo tunayapata kutoka kwa binti mfalme, tunapotoa hadithi sio kusoma na kufurahia tu ila kuna mafundisho muhimu katika maisha yetu. Soma Zaidi...

image Familia mpya baada ya harusi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image WAKATI WA KUFUMBUKA SEHEMU YA 2
Post hii ni mwendelezo wa hadithi ambayo Kwa jina inaitwa wakati wa Kufumbuka, ni mwendelezo wa pale maria anawekwa mbele ya wazee Ili akili kwamba John sio mtoto wa Mzee maganga ila maria akikumbuka wazi kwamba John ni mtoto wa Mzee maganga anakataa kukiri na anaangua kilio na watoto pia wanaangua kilio na pia wanaamua kumpeleka Mari kwenye mizimu Ili iweze kuamua. Soma Zaidi...

image Kifo cha mtoa burudani wa sultani
Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu hadithi ya kifo cha mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

image Hasara za wivu na kutokuwa wazi (sehemu ya 4)
Posti hii inaendelea kuelezea hasara za kuwepo kwa wivu na kutokuwa wazi katika, jamii inafikia wakati baba anapifahamu ukweli anawaita wazazi wawili na kuwaombeza kwa kuwa kimya baada ya kuona matatizo yaliyokuwa yanampata mtoto Lisa. Soma Zaidi...