Zijuwe dalili kuu 7 za vidonda vya tumbo, kama kiungulia, tumbo kujaa, maumivu ya umbo..
Vidonda vya tumbo huweza kutokea ndani ya tumbo kutokana na mashambulizi ya bakteria aina ya H.pylori, ama kutokana na athari za madawa flani ama mashambulizi ya wadudu wengineo ama kwa sababu ya ugonjwa wa saratani. Makala hii inakwenda kukuletea dalili duu za vidonda vya tumbo.
1.Maumivu ya tumbo; hii pengine ndio katika dalili kuu zaidi ambazo wengi wenye vidonda vya tumo wanaipata. Maumivu haya yanawza kuwa makali sana wakati mgonjwa akiwa na njaa.Tumbo hili ni tofauti na tumbo la ngiri ama chango. Maumivu haya yanaweza kuanzia chini ya kitomvu na kupanda juu hadi kifuani. Maumivu haya yanaweza kufuatana na dalili zifuatazo hapo chini.
2.Tumbo kujaa; tumbo linaweza kujaa gesi hata akashindwa kula vyema. Huenda mgonjwa akajihisi ameshiba badala ya kuka kidogo. Uhalisia si kwamba ameshiba ila tumbo ndio limejawa na gesi.
3.Kukosa hamu ya kula; hii ni katika dalili ya hatari sana, maana umuhimu wa chakula unafahamika vyema. Mgonjwa anaumwa na tumbo na anakosa kabisa hamu ya kula pia anahisi tumbo kujaa.
4.Kupata kiungulia cha mara kwa mara. Kiungulia unaweza kukitibu kwa kutumia dawa, kwani hazina tabu kwa vidonda vya tumbo. Pia unaweza kulamba majivu, hii ni tiba mbadala ambayo inatumka kutibu kiungulia. Lakini epuka kula vyakula vyenye gesi.
5.Kupungua uzito; vidonda vya tumbo vinaweza kusababisha mtu kupungua uzito, bila ya kujuwa sababu maalumu. Inaweza kuwa ni kutokana na kutokula kwake kwa sababu ya kukosa hamu ya kula.
6.Kichefuchefu na kutapika. mgonjwa wa vidonda vya tumbo wakati mwingine anapata kichefuchefu kisicho na sababu maalumu. Hali hii inaweza kumpelekea akatapika ama asitapike. Na wakati mwingine anaweza kuona dmau kwenye matapishi yake.
7.Mapadiliko kwenye kinyesi. Mgonjwa anaweza kuona mabadiliko kwenye rangi ya kinyesi chake. Kinaweza kuwa cheusi sana na chenye harufu mbaya sana. Na wakati mwingine kinaweza kuwa na damu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Malaria ni moja ya magonjwa hatari yanayoongoza katika vifo vya watoto wengi duniani walio chni ya umri wa miaka 5. Katika post hii utakwend akujifunza kuhusuugonjwa huu jinsi unavyotokea, hatuwa zake na dalili zake.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya maradhi yanayosababishwa na hali za maisha
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Aina za kansa, Kansa ni Aina ya ugonjwa unaosababishwa na kuzaliana kwa seli ambazo sio za kawaida.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi vyanzo vya kuwepo kwa kiungulia, kiungulia ni kitendo cha kupanda kwa gesi kutoka kwenye tumbo mpaka kwenye mdomo,hali uwasumbua wengi na kusababisha hali isiyo rafiki.
Soma Zaidi...post inaonyesha dalili mbalimbali za Kushindwa kwa moyo, wakati mwingine hujulikana kama kutofaulu kwa moyo, hutokea wakati misuli ya moyo wako haisukuma damu kama inavyopaswa. Hali fulani, kama vile ateri nyembamba katika moyo wako (Ugonjwa wa ateri y
Soma Zaidi...Upungufu wa maji mwilini hutokea unapotumia au kupoteza Majimaji mengi zaidi ya unayonywa, na mwili wako hauna maji ya kutosha na Majimaji mengine ya kufanya kazi zake za kawaida. Usipochukua nafasi ya Vimiminika vilivyopotea, utapungukiwa na maji.
Soma Zaidi...Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za ukimwi za kwenye ulimi na mdomo
Soma Zaidi...Post ya leo inaenda kufundisha dalili na hatari za presha ya kupanda. Presha ni ugonjwa unaosababishwa na baadhi ya vitu mbalimbali.pressure hujulikana kwa jina lingine ambolo ni hypertension (pressure ya kupanda). presha hugundulika pale ambapo presha ya
Soma Zaidi...Wajawazito wanaposumbuliwa na ugonjwa wa UTI, dalili za UTI na namna ya Kujikinga na UTI
Soma Zaidi...