Maradhi ya macho, dalili zake na matibabu yake

Maradhi ya macho, dalili zake na matibabu yake

Makala hii itakufundisha maradho makuu ya macho, matibabu yake na tiba zake

Maradhi ya macho, dalili zake na matibabu yake

MARADHI YA MACHO



Matatizo ya macho yapo mengi katika jamii, lakini mara nyingi matatizo ya macho yanatibika iwapo mgonjwa ataonana na daktari mara atakapoona dalili. Miongoni mwa matatizo ya macho ni kupoteza uwezo wa kuona.



1.Kutoona karibu (long sightedness)
Tatizo hili mara nyingi huwatokea watu wenye umri wa miaka 40 na kuendelea.



Dalili
A.Katika mazingira ya kawaida anaona sawa sawa
B.Kushindwa kusoma herufi ndogo ndogo
C.Kushindwa kufanya kazi za sehemu ndogo ndogo mfano kutunga sindano.



Matibabu: Kutumia miwani ya kusomea.



2.Kutoona Mbali (short sightedness)
A.Hayana umri maalum
B.Myopia – haoni mbali vizuri
C.Hyperopia – haoni mbali na kichwa kinauma akikosa kuvaa miwani yenye namba ndogo kusaidia lense.



NB: Mgonjwa anasoma karibu bila miwani
Matibabu: Kutumia miwani ya kuonea mbali



3.Mtoto wa Jicho (cataract)
Dalili
A.Kidoto cheupe katikati ya kioo cheusi cha jicho (kinafunika mboni ya jicho)
B.Kidoto cheupe kisichobadilika kwa mwangaza
C.Kupunguza nuru ya macho



NB - Mtu anaweza kuzaliwa nacho au kupata ukubwani, inaweza kuwa kwenye jicho moja au yote. Mgonjwa huona mchanganyiko wa rangi anapoangalia mwangaza kama taa za umeme au gari.



Matibabu
Mtoto wa Jicho huwa anatibika kwa upasuaji mdogo na kumuwezesha mgonjwa kuona tena.



4.Presha ya macho (glaucoma)
Tatizo hili husababishwa na kuongezeka presha ya jicho (intraocular pressure) kutokana na kukosekana uwiano wa mzunguko wa majimaji ndani ya jicho (aqueous fluid) kinachotoka kidogo kuliko kinachoingia.



Matokeo
Glaucoma hukandamiza na kuuharibu mshipa wa fahamu ya jicho na kusababisha kupungua kwa nuru na baadae kupoteza nuru ya macho.



Matibabu: Kuonana na daktari kwa ushauri na dawa




5.Macho tongo
Hutokea ama kwa mtu mmoja mmoja, makundi au kwa msimu.



Sababu:
Vimelea ambavyo huzaliwa kwenye sehemu za uchafu Wakati wa msimu huambukiza kwa kukosa elimu ya afya, kwa mfano kutokuosha mikono baada ya kuamkiana na mgonjwa mwenye maradhi haya au kutumia vifaa vya macho kwa zaidi ya mtu mmoja kama vile miwani.



Dalili
A.Kuhisi kama kuna mchanga ndani ya jicho
B.Kuvimba mifuniko ya macho bila kupoteza nuru.
C.Macho kuwa mekundu sana (conjuctivitis)
D.Kutoka tongo kila mara



Matibabu
Mgonjwa atumie dawa alizoandikiwa na daktari tu, kwani dawa za matone za macho ni nyingi na zina kazi tofauti.



6.Matatizo ya sehemu nyeusi ya jicho (cornea)
Kuna matatizo manne makubwa
1. Kovu - kidoto/kibaka cheupe
2. Kidonda - kidoto kijivujivu
3. Kuingiwa na kitu - kemikali,mdudu, vumbi n.k
4. Kutoboka na kutoa maji.
Indhari: hali ya pili mpaka ya nne zikitokea mgonjwa akimbizwe
hospital wakati jicho limefunikwa baada ya huduma ya kwanza



Dalili
KOVU
1.Haina maumivu
2.Jicho haliwi jekundu
3.Jicho halivimbi
4.kupungua nuru jicho



KIDONDA
A.Kinayo maumivu
B.Jicho lililoathirika huwa
C.jekundu
D.Jicho kupunguka nuru
E.Kuuma jicho kwenye
F.mwangaza
G.Kutoka machozi
H.Jicho kuvimba



Kidonda kinaweza kusababishwa na bakteria, fangas, ukosefu wa vitamin A au kwa kuumia mfano; kujichoma na kitu chenye ncha au kitu kigumu, kuingiwa na kitu jichoni, kuungua au kuingia kemikali jichon.



Indhari: Iwapo jicho litaumia lifunike jicho lisipate mwangaza kisha mpeleke mgonjwa hospitali.



7. Kemikali na kuungua
Kama mgonjwa ameingia kemikali kama vile acid, alkali, saruji, chokaa mtie maji ya mchuruziko kwa takriban dakika 15 mfululizo na baadae mpeleke hospitali




8.Macho kuwasha na kutokwa na machozi (conjuctivitis)
Huwakumba zaidi watoto wa umri kati ya miaka 5 -15 ambao hupendelea kucheza sehemu za vumbi au kwenye muangaza mkali (pwani yenye mchanga mweupe sana)



Watu wazima wenye kufanya kazi kwenye viwanda vinavozalisha vumbi, na wenye pumu ya muda mrefu.



Dalili
A.Macho kuwasha (Nuru ya macho haipungui)
B.Macho kubadilika rangi (kahawia)
C.Kutokwa na machozi mengi (sana)
D.Kushindwa kuangalia kwenye muangaza mkali



Matibabu
Kusafisha macho mara kwa mara kwa maji safi.
Kutumia dawa kwa maelekezo ya daktari



9.Kinundu katika mfuniko wa juu au chini wa jicho



DALILI
A.Kinundu kisichouma
B.Mara nyingi hupona wenyewe au unaweza kukikanda kwa maji ya uvuguvugu.
C.Kisipopona au kitakapokuwa kikubwa huhitaji upasuaji mdogo.



10.Uvimbe katika mfuniko wa jicho (cellulitis)



A.uvimbe kwenye mifuniko ya jicho
B.inaweza kuzuwia jicho kucheza (kutembea tembea)
C.mara nyingi hutokea baada ya kusambaa kwa maambukizo
D.ya socket ya jicho kutoka pembezoni kwa saines (sinusitis) za pua
E.husababisha kupoteza nuru za macho



Matibabu: Mpeleke mgonjwa kwa daktari wa masikio, pua na koo (ENT).





                   



Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views: 9167

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 web hosting    

Post zinazofanana:

Madhara ya gonorrhea endapo haitotibiwa

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya gonorrhea endapo haitotibiwa

Soma Zaidi...
Fahamu ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito.

Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito, kaswende inaweza kukaa kwa mtu zaidi ya miaka mingi bila kuleta madhara ya moja kwa moja lakini kadiri ya siku zinavyokwenda madhara utokea hasa wakati wa ujauzito, madhara hayo umwadhiri mtot

Soma Zaidi...
Njia salama za kuongeza uwezo wa kushika mimba.

Kupata ujauzito ni safari inayohitaji maandalizi ya mwili na akili. Kwa wanandoa wengi, mabadiliko madogo lakini yenye tija katika mtindo wa maisha yanaweza kuongeza nafasi za kupata mtoto kwa kiasi kikubwa. Makala hii inaangazia mbinu zilizothibitishwa kisayansi za kuboresha afya ya uzazi na kuongeza nafasi za kushika mimba kwa njia salama na ya asili.

Soma Zaidi...
SABABU ZA KUTOKEA KWA VIDONDA VYA TUMBO

SABABU ZA KUTOKEA KWA VIDONDA VYA TUMBO Sababu za kawaida za vidonda vya tumbo ni maambukizo na bakteria Helicobacter pylori (H.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kutofautisha maumivu ya kichwa cha kawaida na ya malaria.

Maumivu ya kichwa ni tatizo la kawaida linaloweza kusababishwa na mambo mengi, kuanzia uchovu, njaa, hadi magonjwa kama malaria. Kwa kuwa malaria ni ugonjwa unaoweza kuwa hatari ndani ya muda mfupi, ni muhimu kujua jinsi ya kutofautisha maumivu ya kichwa ya kawaida na yale yanayoashiria maambukizi ya vimelea vya malaria. Makala haya yanakupa mwongozo wa dalili za msingi ili uweze kuchukua hatua sahihi za kiafya.

Soma Zaidi...
Kukosa choo

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za kukosa choo

Soma Zaidi...