Kiungulia, dawa yake na namna ya kuzuia kiungulia

Kiungulia, dawa yake na namna ya kuzuia kiungulia

Tambuwa kiungulia, sababu zake, dawa za kiungulia na namna ya kupambana na kiungulia

Kiungulia, dawa yake na namna ya kuzuia kiungulia

NJIA ZA KUZUIA KIUNGULIA
Kiungulia hutokea pale tindikali zilizopo tumboni zinapanda juu na kufikia koo sehemu ambayo inaunganisha tumbo na koo la chakula. Kiungulia sio shida sana kiafya kwani huwa kiaondoka chenyewe. Hata hivyo kuna watu wapo hatari kupata kiungulia cha mara kwa mara.



Je na wewe ni mmoja katika wanaopata kiungulia mara kwa mara. Je kiungulia ni kikali kiasi cha kuharibu ratiba na uhuru wako? Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa nitakuletea njia ambazo zitakusaidia kuzuia kiungulia cha mara kwa mara.



Njia za kuzuia kiungulia
1.Usile chakula kingi kupitiliza
2.Punguza uzito ulio nao
3.Punguza unywaji wa pombe
4.Usinywe sana chai ya majani ya chai yenye caffein kwa wingi
5.Tafuna bigjii zisizo na sukari nyingi
6.Wacha kutumia kitunguu kisichopikwa kama kwenye kachumbari
7.Epuka vinywaji vyenye carbonate. Soma lebo ya kinywaji chako kama ni soda ama maji kama kuna carbonate
8.Usinywe kwa wingi juisi zilizotokana na vitu vya uchachu kama limao
9.Punguza kula chokoleti kwa wingi
10.Unapolala inuka kichwa chako kwa mfano tumia mto
11.Usilale ndani ya masaa matatu baada ya kula
12.Ukilala lalia upande wa kushoto usilalie upande wa kulia.



Dawa za kutibu kiungulia
Unaweza kutibu kiungulia kwa kutumia antacid kama vile Tums, Rolaids na Maalox. Dawa ambazo zimetengenezwa kwa madini ya calcium carbonate au magnesium ni nzuri pia. Magnesium si nzuri kama ujauzito upo mwishoni.



Madaktari wengi wanakataza kwa wajawazito matumizi ya antacid ambazo zimechanganywa na sodium, ama zila lebo ya aluminium carbonate kwani zinawza kupelekea kukosa choo. Pia dawa hizi za kiungulia zinakatazwa kwa wajawazito Alka-Seltzer.





                   



Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF
Views: 4008

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 ai web app     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zinazofanana:

Nini sababu ya kuchubuka midomo na kuwa myeupe

Kama una tatizo la midomo kuchubuka na kuwa myeupe ama kuwa na vidonda. Post hii inakwenda kuangalia swala hili.

Soma Zaidi...
Homa ya dengue: Dalili na jinsi inavyoenezwa na mbu.

Homa ya Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoambukizwa kwa binadamu kupitia kuumwa na mbu aina ya Aedes aegypti. Ugonjwa huu ni tishio kubwa katika maeneo ya kitropiki na mikoa yenye joto. Ingawa visa vingi ni vya wastani, baadhi ya watu wanaweza kupata Dengue kali (Dengue Hemorrhagic Fever) ambayo inahitaji uangalizi wa haraka wa kimatibabu. Makala hii inaelezea mzunguko wa uenezaji wa virusi hivi na umuhimu wa usafi wa mazingira katika kudhibiti mbu.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kupunguza maumivu ya hedhi kwa njia asilia.

Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi, kitaalamu kama dysmenorrhea, huwasumbua wanawake wengi kila mwezi. Ingawa mara nyingi hutibika kwa dawa za dukani, njia za asili zinaweza kusaidia sana kupunguza makali ya maumivu hayo bila kuathiri mfumo wa mmeng'enyo wa chakula au figo. Makala hii inaangazia mbinu bora za asili unazoweza kuzitumia nyumbani ili kupata nafuu.

Soma Zaidi...
Dalili za uvumilivu wa pombe

Uvumilivu wa pombe unaweza kusababisha athari za haraka, zisizofurahi baada ya kunywa pombe. Ishara na dalili za kawaida za kutovumilia kwa pombe ni pua iliyojaa na Kuvuta ngozi. Uvumilivu wa pombe husababishwa na hali ya maumbile ambayo mwili hauwezi k

Soma Zaidi...
Dalili za UKIMWI na VVU kutoka mwanzoni mwa siku za mwanzo

Je na wewe ni katika wanaosumbuka sana kujuwa dalili za kwanza za ukimwi toka siku ya kwanza, ama dalili za ukimwi kwenye ulimi, ama unatakakujuwa ni muda gani ukimwi huonekana, na je ukishiriki ngono zembe ndio utapata ukimwi? Basi makala hii ni kwa ajil

Soma Zaidi...
Njia za kujilinda na kujikinga na UTI

Somo hili linakwenda kukuletea njia za kujilinda na kujikinga na UTI

Soma Zaidi...