Dalili za gonorrhea - gonoria
Jifunze dalili za gonorrhea na namna inavyoambukiza, zipi athari za gonori kwa wanawae na wanaume
Dalilii za gonorrhea
Gonorrhea au gonoria ni moja kati ya magonjwa yanayoenezwa kupitia ngono. Huweza kusababishwa na bakteria na kuathiri wanaume na wanawake. Kuweza kuathiri mdomo, koo, mkundu na sehemu za siri kwa wanaume na wanawake. Huweza kuambukizwa kwa kupitia ngono ya mdomo, ngono ya ukeni ama kwenye mkundu. Kwa watoto huweza kuathiri macho. Gonorrhea (gonoria) huambukizwa kutoka kwa mama kuja kwa mtoto wakati wa kujifunguwa.
Dalili za gonoria (gonorrhea) zinaweza kuchelewa kuonekana kwa wanawake kuliko kwa wanaume. Wapo wengine hawaonyeshi dalili yeyote ile hadi hali itakapokuwa ni mbaya zaidi. Kwa mara nyingi dalili za gonoria (gonorrhea) huonekana kuanzia siku 2 mpaka 7 baada ya kuambukizwa. Na kwa wanawake inaweza kuchelewa zaidi hadi mwezi.
Ni zipi dalili za gonoria (gonorrhea)?
Dalili za gonoria (gonorrhea) unaweza kuwa na dalili tofautitofauti kulingana na jinsia. Dalili kwa wanawae na kwa wanaume zinaweza kutofautiana kulingana na maumbile ya jinsia hizi. Muda wa kutokea dalili hizi pia hutofautiana. Pia huweza kuahiri maeneo mengi mwilini.
Dalili za gonorrhea kwa wanaume:-
1.Maumivu wakati wa kukojoa
2.Kutokwa na majimaji kama usaha kwenye uume.
3.Kuvimba pamoja na maumivu ya korodani.
Dalili za gonorrhea kwa wanawake
1.Kutokwa na uchafu sehemu za siri
2.Maumivu makali ya maeneo ya nyonga
3.Maumivu makali wakati wa kukojoa
4.Kutokwa na damu kabla ya hedhi na baada ya hedhi
Dalili za gonoria (gonorrhea) katika maeneo mengine ya mwili:
1.Maumivu ya mkundu, na kutokwa na kama kinyesi pamoja na maumivu ya tumbo na mvurugiko.
2.Maumivu ya macho, kushindwa kuvumilia mwanga mkali, na macho kutoa kama usaha
3.Vidonga vya koo na kuvimba kwa tezi na lumph kwenye shingo
4.Maumivu ya viungio pamoja na kuwa na joto.
Ni nini chanzo na sababu ya gonoria (gonorrhea)
Kama nilivyotangulia kukuambia hapo juu kuwa gonoria huambukizwa na bakteria. Bakteria hawa hufahamika kwa jina la bacterium Neisseria gonorrhoeae. Na huenezwa kwa njia ya kufanya ngono ya mdomo, mkundu ama ukeni.
Waliohatarini kupata gonorrhea (gonoria)
Watu wa umri wowote wanaweza kupata ugonjwa huu. Hata hivyo kuna ambao wapo hatarini zaidi. Kwa wanawake walio zaidi ya miaka 25 wapo hatarini zaidi. Na wanaume ambao wanashiriki ngono ya mkundu wapo hatarini zaidi. Pia wafuatao wanaweza kuwa hatarini kupata gonorrhea:-
1.Kuanza mahusiano na mpenzi mpya
2.Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja (michepuko)
3.Kuwa na penzi ambayo ana wapenzi wengine (michepuko zaidi)
4.Kuwa na maambukizi ya goniria hapo nyuma ama kuwa na maambukizi mengine ya magonjwa ya ngono.
MADHARA YA GONORIA (GONORRHEA) ENDAPO HAITATIBIWA
Endapo gonoria itachelewa kutibiwa inaweza kuleta madhaya mengi ndani ya mwili kuanzia ugumba, kudhoofu mwili, maumivu na mengineye. Yafuatayo ni madhara ya kuchelewa kutibu gonoria:-
1.Ugumba kwa wanawake. Ugonjwa huu kwa mwanamke unakula via vya uzazi kwa fujo sana. Unaathiri mirija ya falopia ambayo nduo inayohusika kubeba yai na utungaji mzima wa mimba na kusababisha PID yaani Pelvic Inflamatory Deseases. Hivyo mwanamke anahitajika atibiwe mapema kabla madhara hayajakuwa makubwa.
2.Ugumba kwa wanaume. Kwa wanaume gonoria huathiri vimirija vijidogo vilivyopo kwenye korodani. Mirija hii hujulikana kama epididymis. Hali hii hupelekea kuharibika kwa mirija hii hivyo kushindwa kubeba mbegu za kiume kuzitoa nje. Ugonjwa unaosababishwa na uharibifu huu hujullukana kama epididymitis.
3.Mashambukizi ya viungo vingine vya mwili na kuleta homa, upele, vidonda, maimivu ya viungo, kukaza na kuvimba kwa viungio.
4.Huongeza hatari zaidi kwa mwenye VVU na UKIMWI. Watu wenye VVU na UKIMWI ni rahisi kueneza gonoria kwenda kwa mwingine.
5.Kwa watoto waliop[ata gonoria wakati wa lujifunguwa wanaweza kupata upofu na madhara mengine kati afya zao.
NJIA ZA KUPAMBANA NA KUKABILIANA NA GONORIA (GONORRHEA)
1.Kuwa mwaminifu katika mahusiano wacha kuchepuka
2.Hakikisha mwenza wako yupo salama
3.Usishiriki ngono na mtu aliyeathiriwa na magonjwa ya ngono bila kinga
4.Tumia kondomu
5.Pima mara kwa mara gonoria.
.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 ai web app 👉5 web hosting 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Athari za kutokunywa maji ya kutosha kwa afya ya figo.
Figo ni kiungo muhimu kinachohusika na kusafisha damu na kudhibiti uwiano wa maji mwilini. Makala hii inachunguza kwa kina uhusiano wa moja kwa moja kati ya ulaji wa maji na afya ya figo. Tutajadili jinsi upungufu wa maji (dehydration) unavyoweza kusababisha magonjwa sugu ya figo, mawe kwenye figo, na shinikizo la damu, pamoja na kutoa mwongozo wa kisayansi wa kiasi sahihi cha maji unachohitaji ili kulinda afya yako.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa Uti wa Mgongo (Meningitis): Dalili za dharura.
Ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis) ni dharura ya kitabibu inayohitaji utambuzi na matibabu ya haraka. Makala haya yanachunguza kwa kina maana ya ugonjwa huu, visababishi vyake (bakteria, virusi, na fangasi), dalili hatarishi zinazohitaji huduma ya dharura, na njia za kujikinga. Lengo ni kutoa mwongozo wa kitaalamu kwa jamii ili kupunguza vifo na madhara ya kudumu yatokanayo na ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Sababu za maumivu ya uti wa mgongo
Posti hii inahusu zaidi sababu za uti wa mgongo, ni ugonjwa unaotokana na kuwa na maumivu kwenye uti wa mgongo, hasa hasa ugonjwa huu ushambulia watu kuanzia miaka ishilini mpaka kwenye arobaini hivi, zifuatazo ni sababu za maumivu katika uti wa mgongo.
Soma Zaidi...ATHARI ZA KUTOTIBIWA VIDONDA VYA TUMBO
ATHARI ZA KUTOTIBIWA VIDONDA VYA TUMBO Kuachwa kwa vidonda vya tumbo bila kutibiwa, vinaweza kusababisha: Kutokwa na damu kwa ndani.
Soma Zaidi...Fahamu Ugonjwa wa uchovu sugu.
Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa uchovu sugu ni ugonjwa tata unaoonyeshwa na uchovu mwingi ambao hauwezi kuelezewa na hali yoyote ya matibabu. Uchovu unaweza kuwa mbaya zaidi kwa shughuli za kimwili au kiakili, lakini haiboresha kwa kupumzika
Soma Zaidi...Namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo, hizi ni njia ambazo zinapaswa kufuatwa ili kutokomeza kabisa maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.
Soma Zaidi...