Hizi ni siku hatari kwa mwanamke ambazo ni ahisi kwake kubeba mimba, siku nitakueleza ni zipi na ni zipi sifa zake
SIKU ZA KATARI NA SIKU ZA KUSHIKA MIMBA.
Kila mwanamke ana siku yake ambayo ni hatari zaidi kushika mimba. Siku hii inaweza kufanana na mwanamke mwingine ambaye anafanana naye mahesabu. Hata hivyo wanaweza kutofautiana kutokana na vyakula, maumbile na hali za maisha. Hapa nitakuletea orodha ya siku hatari za mwanamke.
Nini maana ya siku hatari?
Hizi ni siku ambazo mwanamke anakadiriwa kupata ujauzito. Ni mfululizo wa siku ambazo makadirio ya mwanamke kupata ujauzito ni mkubwa kuliko siku nyingine. Kabla ya kuzijuwa siku hizi kwanza hakikisha unajuwa vyema idadi ya siku mwanamke anazokwenda hedhi. Wanawake wanakwenda hedhi ndani ya mzunguruko unaoanzania siku 21 mpaka 35. hii inamaana kuna am,bao siku zao ni nyingi na wengine ni kidogo.
Sasa ni ipi siku hatari kwa mwanamke, siku ambayo mawanamke atapata ujauzito?. siku hii nitakuorodheshea, ila kwanza nataka tu nikujuze kwa ufupi sifa ya siku hiyo. Kwa nini, ni kwa sababu siku hizi zipo nyingi na zote ni hatari kwani zinaweza kuleta mimba. Ila katika hizo ipo ambayo ni hatari zaidi. Siku hiyo ina sifa hizi:-
1.Mwili wa mwanamke katika siku hii utakuwa na joto kulinganisha na siku zilizopita. Kwa urahisi unaweza kugunduwa kama unatumia kipima joto. Ila ukiwa makini unaweza kujigunduwa kama joto lako limepanda. Hakikisha ongezeko hiki ka joto hakiambatani na shida nyingine za kiafya kama maradhi.
2.Uteute unaopatikana kwenye shingo ya kizazi utakuwa umeongezeka na ni wenye kuteleza kama vile majimajiya yai lililopasuliwa. Kama utaingizakidole ndani zaidi ya uke unaweza kuupata kwenye kidole chako.
3.Siku hii hamu ya kushiriki tendo la ndoa nikubwa kuliko siku yingine. Hii haina haja ya kuielezea. Kama mwanamke homoni zake hazina shida basi lakima kutakuwa na siku ambayo atahitaji sana kushiriki ngono kuliko siku nyingine.
Nitaijuwaje siku hatari, ya kupata mimba?
Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla ya kupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12 nyuma, kisha toa siku 4 mnyuma ndani ya siku nne zizi ndizo yai hutolewa. siku hizi ndizo moja wapo yai hutolewa. Kwa mfano:--
1.Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla ya kuingia hedhi (21 - 12 = 9) kisha toa nne nyuma (9-4=5) basi mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 5 na 9 katika siku zake.
2.Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kabla ya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku nne tena nyuma (20-4=16) kwa hiyo mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 16 mpaka 20
Tumia mfano huu kwa kuitafuta siku yako ya kupata ujauzito. Kama utakuwa na maoni na maswali wasiliana nasi hapo chini.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Posti hii inahusu zaidi uzazi wa mpango kwa njia ya kumwaga shahawa nje, hii ni njia mojawapo kati ya njia za uzazi wa mpango ambapo mwanaume humwaga nje mbegu ili asimpatie Mama mimba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kupasuka kwa mfuko wa uzazi hasa mama anapokalibia kujifungua.
Soma Zaidi...Maumivu ya tumbo nakiuno kwa mwanamke yanahitaji uangalizi wakina. Kwani kuna sababu nyingi ambazo zinawezakuwa ni chanzo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi sababu za kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, kuna wakati mtoto anapozaliwa anaweza kuvunjika kwenye sehemu mbalimbali kwa sababu zifuatazo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Ute unaotoka wakati wa ujauzito, kwa kawaida wakati wa ujauzito Kuna Ute ambao utoka na ni tofauti na kawaida pale mwanamke akiwa Hana mimba.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa maji yaliyomo kwenye mfuko wa mtoto akiwa tumboni. Ni maji ambayo kwa kitaalamu huitwa (Amniotic fluid)
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa hedhi zaidi ya mara moja kwa mwezi mmoja, mara nyingi kuna Watu ambao huwa wanalalamika kwa sababu ya kupata hedhi za mara kwa mara kwa mwezi mmoja.
Soma Zaidi...Uchungu wa uzazi hutokana na kubana nakuachia kwa misuli hii husababishwa kufunhuka kwa mlango wa tumbo la uzazi pamoja na shingo ya kizazi na kumuongezea mama uchungu wakati wa kujifungua(during labour) Pia kubana na kuachia huanza polepole wakati wa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango kwa mama aliyejifungua kuanzia miezi sita mpaka mwaka mmoja.
Soma Zaidi...