picha

Jinsi macho yanavyoweza kuzungumza kuhusu afya yako ya kimwili na kiakili

Jinsi macho yanavyoweza kuzungumza kuhusu afya yako ya kimwili na kiakili

MACHO YANAFAFANUA KUHUSU AFYA:


Macho ya mwanadamu yanaweza kuwa ni malango wa kufahamu afya ya mtu kiakili na kimwili. Kupitia macho p[olisi na wapelelezi wanaweza kufahamu mhalifu ni nani. Kupitia macho daktari anaweza kufahamu matatizo kadhaa katika afya ya mtu. Makala hii itakwenda kukufahamisha ni kwa namna gani macho yako yanaweza kuweka wazi kuhusu afya yako. Hapa tutakwenda kuona macho katika nyanja hizi:-
A.Umbo
B.Rangi
C.Michubuko
D.Na kama kuna vinyama vilivyoota kwenye macho.



Baada ya kusoma makala hii utaweza kufanya uchunguzi kuhusu afya yako wewe mwenyewe kabla hujakwenda hospitali. Unaweza kutumia kioo ama mtu aliye karibu nawe. Makala hii sio kipimo cha mwisho, hakikisha kuwa majibu kuhusu afya yako utayapata kwa daktari.



1.Mzunguruko wa macho. Kama kwenye mzunguko wa macho yako kwa nje kuna uvimbe hii inaweza kuashiria kuwa mtu huyu atakuwa anasumbuliwa na aleji. Pia inaweza kuwa ama infection (mashambulizi ya bakteria) kwenye machi yake. Hali hii pia inaweza kuashiria matatizo kwenye figo. Hali hii inaweza kuandamana na dalili kama macho kuwa mekundu, miwasho kwenye macho, kuvimba kwa macho. Daktari ataweza kupima mkojo wako ili kupata taarifa juu ya afya ya figo.


2.Kope; kope inaweza kuwa ni kioo cha kuonyesha afya ya mtu. Kama kwenye maoteo ya kupe kuna rangi nyekundu huashiria kuwa huwenda mtu anasumbuliwa na ugonjwa wa naemia (upungufu wa damu). dalili kuu ya ugonjwa huu ni kupauka kwa ngozi ya ndani ya kope. Kama mtu atashindwa kufunga na kufunguwa kope zake vyema itaweza kuashiria shida kwenye mfumo wa neva.



3.Mijongeo ya macho; misuli inayotumika katika mijongeo ya macho, (kwenda kulia, kushoto, juu na chini) ina mahusiano moja kwa moja na mfumo wa neva yaani mfumo wa fahamu hivyo kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na ubongo. Sasa endapo mfumo wa fahamu na ubongo utakuwa na matatizo huweza kuathiri misuli hii na kusababisha mtu ,ushindwa kujongesha macho yake kwa ufasaha. Kwa mfamo mtu anaweza kushindwa kupeleka jicho lakoe upande mmoja kama wa kulia ama kushoto.



4.Mahala lilipo jicho lako; jicho lipo kwenye sehemu yake maalumu na linafiti vyema hapo. Sasa wakati mwingine jicho la mtu unaweza kuliona kama limeingia ndani sana ama wengine utaliona limetokeza nje sana. Sasa endapo mtu anasumbuliwa na upungufu wa maji mwilini utakuta macho yeke yameingia ndani. Na endapo macho yake yametokeza nje sana huwenda mtu uyu anasumbuliwa na shida ya tezi ya thyroid.



5.Mboni ya jicho lako; Mara nyingi utaona madaktari wanamulika jicho lako. Kinachoangaliwa ni namna ambavyo mboni ya jicho lako itafanya nini baada ya kumulikwa. Kikawaida mboni inatanuka na kusinyaa kulingana na mwanga ulioifikia. Hivyo endapo jicho lako litashindwa kufanya haya itaonyesha shida kwenye mfumo wa fahamu unaoungana kwenye macho.



6.Ndani ya jicho lako; ndani ya jicho kuzungukia hilo jiduara jeupe unalolioa ambalo ndio jicho kuna vimishipa vingi sana vya damu vimelishikilia. Kwa watu wenye hali mbaya ya shinikizo la juu la damu na wale wenye kisukari huweza kuathiri jisho na kusababisha uoni hafifu. Kufanya uchunguzi wa kina juu ya swala hili kunahitaji ujuzi zaidia, wakati mwingine datkari hutumua kimiminika maalumu ili kulegeza jicho. Dakatari ataweza kuchunguza zadi mpaka sehemu yenye makutano ya neva zinazopelekea taarifa kwenye ubongo



Kama kutakuwa na presha kubwa kwenye fuvu huwenda kutokana na stoke, uvimbe wa ubongo ama maradhi mengine, sehemu ya makutano ya mishipa ya neva (disc) kutakuwa na rangi ya mpaiko na vijimishipa vya damu vitakuwa na rangi ya utofauti.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Huduma Main: Afya File: Download PDF Views 1878

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 ai web app    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Kazi za vitamin B na makundi yake

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kazi za vitamin B na makundi take

Soma Zaidi...
Malengo ya kumsafisha mgonjwa nywele.

Posti hii inahusu zaidi malengo ya kumsafisha mgonjwa nywele zake, ni sababu ambazo upelekea kumsafisha mgonjwa nywele kama tutakavyoona hapo chini.

Soma Zaidi...
Mbinu za kuponyesha majeraha

Posti hii inahusu zaidi mbinu ambazo hutumika kuponyesha majeraha kwa haraka zaidi,tunajua majereha utokana na kupona kwa vile vidonda au kupona kwa sehemu ambayo imekuwa na majeraha kwa hiyo ili kuponyesha majeraha hayo tunapaswa kufanya yafuatayo.

Soma Zaidi...
Njia za kukabiliana na minyoo

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na minyoo

Soma Zaidi...
Madhara ya kutumia dawa bila ushauri wa kitaalamu.

Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutumia dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu, madhara haya uwapata watu wengi kwa sababu hawajui taratibu za matumizi ya dawa.

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa aliyeungua

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa aliyeungua

Soma Zaidi...
Faida za kusafisha vidonda.

Posti hii inahusu zaidi faida za kusafisha vidonda, ni faida ambazo Mgonjwa mwenye vidonge uzipata kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Namna ya kumwosha Mgonjwa vidonda

Posti hii inahusu zaidi njia za kutumia unapotaka kumwosha Mgonjwa vidonda, ni njia muhimu ambazo ni lazima kuzipitia unapotaka kumwosha Mgonjwa vidonda.

Soma Zaidi...
Viwango vitatu vya kuungua.

Posti hii inahusu zaidi viwango vitatu vya kuungua. Ili tuweze kujua mtu ameunguaje Kuna viwango vitatu vya kujua kiasi na namna mtu alivyoungua

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa mtu anayetokwa na damu ya pua

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu anayetokwa na damu ya pua

Soma Zaidi...