IJUWE FIGO NA MARADHI YAKE NA NAMNA YA KUJIKINGA NA MARADHI YA FIGO:

Figo ni katika viungo muhimu sana katika mwili wa mwanadamu. Ijapokuwa kila kiungo ni muhimu kwenye mwili wa binadamu, lakini katika mfumo wa kutoa mkojo na kuchuja damu figo ni muhimu zaidi. maradhi ya figo yamekuwa yakiongezeka kuliko ilivyokuwa hapo zmani, ijapokuwa kasi yake sio sawa na maradhi mengine. Makala hii itakwenda kukueleza ni nini hasa hizi figo, na ni yapi maradhi yake na ni kwa namna ggani utaweza kujilinda na maradhi ya figo.


Kila mtu ana figo mbili kwenye mwili wake, ukubwa wa figo unakadiriwa kufukia ukubwa wa ngumi yako. Katika mwili wako figo hupatikana karibia na katikati ya mgongo chini kidogo ya mbavu. Ndani ya kila figo kuna mamilioni ya vichujio vya kuchuja damu vinavyojulikana kama nephron. Kazi yake kubwa ni kuchuja damu, kuondoa uchafu kwenye damu na kuondoa maji ya ziada kwenye damu na kupata mkojo ambao ni mchanganyiko wa majina na uchafu uliotoka kwenye damu. Baadaye maji haya ya mchanganyko yanakwenda kwenye kibofu na kuhifadhiwa kama mkojo.Kati ya maradhi mengi ya figo huanza kuathiri hizi nephone. Na endapo hizi nephrone zikiharibiwa zinapelekea figo kuathirika na kushindwa kufanya kazi vyema na kushindwa kuondoa uchau kwenye damu. Katika sababu za tatizo hili la kuathirika kwa nephone inaweza kuwa matatizo ya kurithi, majeraha, ama matumizi ya madawa ambayo athari yake yanaweza kuathiri figo.Unaweza kuwa hatarini sana kama una maradhi ya kisukari, ama kama una shinikizo kubwa la damu ama una ukaribu wa kifamilia na watu ambao wana tatizo hili. Maradhi hatari ya figo ni yale ambayo huathiri nephone kipolepole na huwenda hii kuchukuwa miaka kadhaa hadi kuja kuumwa. Matatizo mengine yanayoweza kuathiri figo ni kama saratani ya figo na vijiwe vya kwenye figo.Katika njia za kulinda figo yako dhidi ya maradhi ni pamoja na kunywa maji mengi angalau glasi 8 kwa siku. Fanya mazoezi na punguza kula vyakula vyenye chumvi sana. Nenda chooni kila unapohisi kukojoa wacha kubana mkojo kwa muda mrefu. Hizi ni baadhi tu ya njia ambazo zitakusaidia kulinda figo zako dhini ya maradhi.