Ni nini husababisha mate kujaa mdomoni, na ni yapi matibabu yake

Ni nini husababisha mate kujaa mdomoni, na ni yapi matibabu yake

Hapa tutaangalia baadhi ya sababu zinazopelekea mdomo kujaa mate na namna ya kutibu tatizo la kujaa kwa mate mdomoni

Ni nini husababisha mate kujaa mdomoni, na ni yapi matibabu yake

NI NINI HUSABABISHA MATE KUJAA MDOMONIKutokwa na mate mengi mdomoni si ugojwa ni hali inayoweza kutokea kwa mtu yeyote. Mara nyingi hali hii haihitaji matibabu wa dawa, na huondoka yenyewe. Lakini hutokea baadhi ya nyakati ikawa mate yanatoka zaidi mdomoni. Je na wewe ni miongoni mwao? Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa tutaangalia baadhi ya sababu zinazopelekea mdomo kujaa mate. Sababu hizi zipo nyingine ni kwa wanawake tu, pia zipo ambazo ni kwa watu wa jinsia zote. Tunatarajia baada ya kusoma makala hii utaweza kuzijuwa sababu zinazopelekea mdomo kujaa mate, pia utaweza kupata kujuwa nini unatakiwa ufanye kulingana na tatizo lako.


KUJAA KWA MATE MDOMONI NI NINI HASA?
Kitaalamu kitendo hiki cha kujaa kwa mate mdomoni hufahamika kama hypersalivation. Hiki ni kitendo cha mdomo kujaa mate na wakati mwengine hutokea mate yakatoka yenyewe kwenye midomo baada ya kujaa. Kitaalamu kitendo hiki sio ugonjwa ila ni dalili ya kuwepo kwa tatizo lakiafya ama kuwepo kwa jambo lililopelekea mabadiliko ya mwili na kiafya.


JE MATE NI NINI?
Mate ni kimiminika cheupe kinachopatikana mdomoni ambacho hutengenezwa kwenye tezi za mate zinazojulikana kama salivary glands. Mate yana vichochezi (enzymes) ambavyo hutumika katika mmeng'enyo wa chakula hasa chakula cha wanga mdomoni. Mate pia husaidia katika kulainisha chakula na kuweka mgomo katika hali ya usafi, usalama na ubichibichi.
Tafiti zinaeleza kuwa mtu wa kawaida anaweza kuzalisha mate yanayofikia lita moja na nusu kwa siku. mate huzalishwa kwa wingi mtu anapokula na uzalishaji huu hupunguwa pale anapolala.


MADHARA YA KUWA NA MATE KIDOGO
Kwa kuwa mate yana faida kubwa mwilini hivyo endapo uzalishaji wa mate hautakuwa wa kutosheleza madhara huweza kumpata mtu ni kama:-
1. mdomo kuwa mkavu
2. Mmeng'enyo wa chakula kutofanyika vyema mdomoni kwa vyakula vya wanga
3. Mtu anaweza kupata taabu wakati wa kumeza
4. Anaweza kupata vidonda vya mdomo
5. Mdomo utaweza kuathiriwa kwa urahisi na fangasi, bakteria na sumu na kemikali za kwenye vyakula
6. Hata kuzungumza kunaweza kuathiriwa endapo mtu atakosa mate ya kutosha


MADHARA GANI ATAYAPATA MTU KAMA ATAKUWA NA MATE MENGI ZAIDI?
Kama ilivyokuwa kuna hasara kwa mate kukosekana mwilini, halikadhalika endapo mate yatakuwa mengi zaidi pia hali hii itakuwa na madhara yake. Madhara hayo ni kama:-
1. Matatizo wakati wa kusema, yaani hatoweza kuema vyema kama mate yatakuwa yamejaa mdomoni
2. Itakuwa vigumu kuufunga mdomo
3. Pia mdomo utaweza kupata mashambulizi ya bakteria kwa urahisi.
4. Mtu atashindwa kujiamini na kukaa na watu kwa sababu ya mate yake.


NINI HUSABABISHA MDOMO KUJAA MATE?
Hizi ni katika sababu ambazo hupelekea mate kujaa mdomoni:-
1. Kuongezeka kwa uzalishwaji wa mate mdomoni
2. Kama mtu atakuwa na shida na kushindwa kumeza mate ama mdomo kuondoa mate yote wakati wa kutema
3. Kama mtu atakuwa na matatizo ya kutoweza kuufunga mdomo


NINI HUSABABISHA ONGEZEKO LA UZALISHAJI WA MATE MDOMONI
Kama ulivyoona hapo juu sababu za kuwa na mate mengi mdomoni ni ongezeko la uzalishwaji wa mate mdomoni. Sasa swali la msingi kuwa "ni nini husababisha hili ongezeko la uzalishwaji wa mate mdomoni" . Sababu gizo ni kama:-
1. Kichefuchefu
2. Homa ya asubuhi na ujauzito
3. Kama kuna maabukizi na mashambulizi ya bakteria na virusi kwenye koo, tonsil na meneo mengine ya mdomoni
4. Kama umeng'atwa na buibui mwenye sumu, ama umekula uyoga ama umeng'atwa na wadudu
5. Kama unatumia meno ya bandia
6. Kama hufanyi usafi wa kinywa kwa umakini
7. Kama una maambukizi ya T.B ama ugonjwa wa rabies
8. Kama una kiungulia cha mara kwa mara
9. Mipasuko kwenye taya ma amifupa ya taya kutojipanga vyema
10. Vidonda vywnyw mfumo wa mmeng'enye wa chakula kama mdomoni, kooni na tumboni


NINI HUSABABISHA KUSHINDWA KUMEZA MATE AMA KUTEMA MATE YOTE?
Kama tulivyoona kuwa katika sababu zinazopelekea mate kujaa mdomoni ni kushindwa kuyameza yote, ama kuyatema yote. Sasa ni kitu gani husababisha hali hii?
1. Kuwa na shida ya kiafya kwenye mfumo wa fahamu
2. Kuwa na shida ya kiafyakwenye figo


SABABU NYINGINE ZINAZOPELEKEA MDOMO KUJAA MATE
1. Mpangilio mbaya wa meno
2. Majeraha kwenye mdomo
3. Hewa mbaya
4. Upungufu wa maji mwilini
5. Matatizo kwenye mfumo wa fahamu hasa katika kuhisi ladha ya chakula
6. Kama una maradhi ya pneumonia


NINI UFANYE KAMA UNA HILI TATIZO:
1. Kwa kupitia dalili zilizotajwa hapo juu, angalia ambayo huwenda ndio sababu kwako.
2. Kawaida tatizo hili halihitaji dawa, ila kama imezidi fika hospitali kwa uchunguzi zaidi.
3. Fika kituo cha afya kwa vipimo zaidi kama hali yako itaendelea kwa muda bila kurudi nyuma.



                   

Bongoclass
Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya hapa chini kuipakua sasa!

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 17504

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces
Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces

Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces, hawa ni fangasi wanaosababisha maradhi yajulikanayo kama blastomycosis.

Soma Zaidi...
Dalili za tetekuwanga
Dalili za tetekuwanga

Tetekuwanga (varisela) ni maambukizi ya virusi ambayo husababisha kuwasha, upele kama vile malengelenge. Tetekuwanga huambukiza sana watu ambao hawajapata ugonjwa huo wala kupewa chanjo dhidi yake. Kabla ya chanjo ya kawaida ya tetekuwanga, karibu watu

Soma Zaidi...
Namna Maambukizi kwenye milija na ovari yanavyotokea
Namna Maambukizi kwenye milija na ovari yanavyotokea

Post hii inahusu zaidi namna Maambukizi kwenye milija na ovari ambayo yanatokea,Mara nyingi usababisha na bakteria wanaoweza kuingia kupitia sehemu mbalimbali.

Soma Zaidi...
Ninashida Kuna mtu anaumwa pressure Kila anap pima Iko juu il mwil aumuumi at kidg n dawa anatumia unawez kunisaidiaj
Ninashida Kuna mtu anaumwa pressure Kila anap pima Iko juu il mwil aumuumi at kidg n dawa anatumia unawez kunisaidiaj

Kama unasumbuliwa na presha post hii ni kwa ajili yako. Hapa tutakuoatia ushauri kutokana na swali alilouliza mdau wetu.

Soma Zaidi...
Dalili za fangasi uken
Dalili za fangasi uken

Posti hii inahusu zaidi dalili za fangasi uken, hizi ni baadhi ya dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la fangasi uken.

Soma Zaidi...
Mlo kwa wagonjwa wa figo wanaochujwa damu
Mlo kwa wagonjwa wa figo wanaochujwa damu

Posti hii inahusu zaidi mlo kwa wagonjwa wa figo wanaochujwa damu, ni wagonjwa ambao figo zao zimeharibika na zimeshindwa kufanya kazi au pengine kuna uchafu mwingi mwilini ambao uchujwa kwa hiyo kuna vyakula muhimu ambavyo wagonjwa wa figo wanapaswa kutu

Soma Zaidi...
Sababu za mwanamke kuumwa tumbo y chini ya kitovu.
Sababu za mwanamke kuumwa tumbo y chini ya kitovu.

Posti hii inahusu sababu za mwanamke kuumwa tumbo chini ya kitovu, ni tatizo ambalo limewapata wanawake wengi na pengine sababu ni vigumu kupata au pengine zinapatikana lakini kwa kuchelewa hali ambayo usababisha madhara mbalimbali kwenye mwili.

Soma Zaidi...
Dawa za kutibu kiungulia
Dawa za kutibu kiungulia

Somo hili linakwenda kukueleza baadhi ya dawa za kutibu kiungulia

Soma Zaidi...
ninasumbuliwa Sana na mapunye ya kichwani nimetumia dawa takribani miaka 3
ninasumbuliwa Sana na mapunye ya kichwani nimetumia dawa takribani miaka 3

Habari, samahani ninasumbuliwa Sana na mapunye ya kichwani nimetumia dawa takribani miaka 3 ila yanapona Tena baada ya Muda flani yanatokea.

Soma Zaidi...
Madhara ya minyoo
Madhara ya minyoo

Somo hili linakwenda kukuletea madhara ya minyoo

Soma Zaidi...