Sababu za mdomo kuwa mchungu
Hapa utajifunza sababu zinzopelekea mdomo kubadilika ladha na kuwa mchungu, ama mchachu.
KWA NINI MDOMO UNAKUWA MCHUNGU?
Umeshawahi kuamka asubuhi ukiwa na ladha chungu sana ya mdomo, na je hali hii ulishawahi kudumu nayo kwa muda wa masaa kadhaa?. bila shaka ungependa kujuwa sababu inayopelekea kutkea hali hii. Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa nitakujuza sababu kuu za kuwa na ladha chungu ya mdomo, na nini kifanyike. Endelea kusoma makala hii hadi mwisho. Ila ningependa utambuwe kuwa mdomo kuwa mchungu mara nyingi sio shida sana ya kiafya kiasi cha kuhitaji dawa ama kumuona daktari. Endapo shida itaendelea hapo fanya maamuzi ya kuonana na daktari
Mdomo kuwa mchungu mara nyingi sio maradhi. Hali hii hutokea na kuondoka yenyewe ndani ya masaa machache. Mara nyingi hutokea wakati wa asubuhi ama unapotoka kulala. Hali hii pia huwapata wagonjwa. Hali hii wakati mwingine inakuwa ni dalili ya maradhi. Kama utaona mdomo wako unaendelea kuwa mchungu kwa muda mrefu onana na daktari kwa uchunguzi zaidi.
Ni nini husababisha mdomo kuwa mchungu?
1.Mdomo kutokuwa msafi. Hii ni kawaida wakati umelala mdomo bakteria waliokuwa wapo mdomoni wanaendelea kufanya kazi yao, kula mabaki ya chakula na kuendelea kuzaliana. Kumbuka mate yana kazi ya kusafisha mdomo,lakini wakati umelala mate hayawezi kufanya kazi hii kwani huwezi kuyatoa. Hivyo uchafu huendelea kujizalisha bila ya kutolewa. Hali hii inaweza kusababisha mdomo kuwa mchungu unapoamka.
Vyema usile kitu muda huu, kabla ya kupiga msaki. Safisha kinywa vyema ladha ya mdomo itarudi sawa ndani ya muda mchache. Pia kama ulitoka kulala baada ya kutema mate kwa muda mchache yaani baada ya mdomo kujisafisha hali hii inaweza kuondoka bila ya wasi wala hakuna ulazima wa kupiga mswaki, kwani mdomo una sifa ya kujisafish awenyewe kwa kutumia mate.
2.Matumizi ya madawa ya antibiotics au antidepressants. Dawa hizi pindi mdu anapozitumia hufyonzwa ndani ya mwili na kutolewa kwa kupitia mate na kusababisha mate kuwa machungu. Mfano wa dawa hizi ni:-
A. Tetracycline
B.Gout medication kama allopurinol na lithium
C.Madawa yanayotumika kutibu maradhi ya moyo.
Baada ya kuacha kutumia dawa hizi ladha ya mdomo itarudi sawa ndani ya siku chache. Pia unaweza kunywa juisi ya vitu vichachu kama hali itaendelea kukusumbuwa.
3.Ujauzito, hali ya mdomo kuwa mchungu ama kuwa na ladha ya chuma kwa wajawazito ni kawaida na hali hii kutaalamu hufahamika kama dysgeusia ama metallic taste. Hutokea kwa uda wa siku kadhaa kisha huondoka. Baadhi ya wajawazito wanapata ladha ya pesa, yaani kama ulishawahi kuweka mdomon hela ya sarafu, ile ladha unayoipata ndio ambayo huwapata baadhi ya wajawazito.
4.Kama unatumia dawa za kuongeza vitamini, unaweza kupata ladha hii. Kuna baadhi ya dawa za vitamini zina madini mengi ya metali. Madini hayokama zinc, shaba, chuma na chromium. Kama dawa hiyo ina madini haya inaweza kubadili ladha ya mdomo na kuwa chungu
5.Ni dalili ya maradhi ya ini. Kama ini lako halifanyi kazi vyema ama lina matatzo, mwili utakuwa na kiasikikubwa cha ammonia ambayo ni sumu. Hatimaye kubadili ladha ya mdomo.
6.Mashambulizi ya kwenye mfumo wa upumuaji. Wakati mfumo wa upumuaji unapokuwa katika mashambulizi ya bakteria ama virusi au fangasi, inaweza kuathiri ladha ya mdomo.
7.Kama umecheuwa, hali hii inaweza kupelekea kubadilika kwa ladha ya mdomo
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 ai web app 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Mambo yanayosababisha kiuno au mgongo kuwa na maumivu
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo yanayoweza kusababishwa mgongo wAko au kiuno kwa na maumivu, Mgongo ukiwa na maumivu makali Sana yanaweza kusababishwa shida kubwa ata utakapokaa au ukilala au ukitumia bado maumivu yanakuwepo.
Soma Zaidi...Sababu za Kutokwa na Damu Mwanzoni mwa Mimba:
Kutokwa na damu katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito ni hali inayoweza kuleta hofu kubwa kwa mama mjamzito. Makala hii inachambua sababu za kawaida za hali hii, inapopaswa kuwa na wasiwasi, na hatua muhimu za kuchukua ili kulinda afya yako na ya kiumbe kilichopo tumboni.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa pepopunda kwa watoto
Pepopunda ni ugonjwa hatari wa kutishia maisha unaosababishwa na sumu inayojulikana Kama tetanospasmin inayotolewa kwenye majeraha yaliyoambukizwa. Bakteria ya pepopunda huingia kwenye mwili wa mtoto mchanga kupitia kisiki cha kitovu ambacho kimekatwa na
Soma Zaidi...Jinsi ya Kumsaidia Mtoto Mwenye Kikohozi
Kikohozi ni njia ya asili ya mwili kujisafisha, lakini kwa mtoto, inaweza kuwa chanzo cha usumbufu mkubwa na wasiwasi kwa wazazi. Post hii inatoa mbinu salama na za nyumbani za kumsaidia mtoto kupata nafuu, huku ikielekeza dalili za hatari zinazohitaji msaada wa kitabibu haraka.
Soma Zaidi...Ugumba (Infertility): Je, tatizo huanzia wapi kwa mwanamume na mwanamke?
Ugumba hufafanuliwa kama hali ya kutoweza kupata ujauzito baada ya kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara bila kutumia njia zozote za uzazi wa mpango kwa kipindi cha mwaka mmoja (au miezi sita kwa wanawake walio na umri wa zaidi ya miaka 35). Ni tatizo linalogusa pande zote mbili; takwimu zinaonyesha kuwa katika visa vya ugumba, karibu theluthi moja inatokana na mwanamume, theluthi moja inatokana na mwanamke, na theluthi iliyobaki ni mchanganyiko wa pande zote mbili au sababu zisizojulikana.
Soma Zaidi...Madhara ya minyoo
Posti hii inaonyesha kiufupi kabisa madhara ya minyoo kwenye mwili wa binadamu. Yafuatayo Ni madhara ya minyoo;
Soma Zaidi...