Siku za kupata mimba.
Kupata mimba ni majaaliwa kama waswahili walivyozoea kusema. Lakini unaweza kufanya jitihada binafsi ili kuonyesha uhitaji wako. Je na wewe ni muhanga wa tatizo hili la kutopata ujauzito? Makala hii ni kwa ajili yako, hapatutaona njia za kuweza kuzijuwa siku za kupata mimba. Pia tutaona dalili za siku hizo.
Mimba huweza kuingia siku ambayo yai litakutana na mbegu ya kiume kwenye mirija ya falopia kwenye tumbo la uzazi la mama. Yai la mwanamke kuzalishwa kwenye ovari. Mwanamke ana ovari mbili, moja upande wa kulia na nyingine kushoto. Hizi mbili hupeana zamu ya kutoa mayai. Yaani kama mwezi huu limetoa hili na nyingine itatoa mwezi ujao.Tafiti zinaonyesha kuwa yai huweza kuanza kukomaa kuanzia siku ya 10 toka kupata hedhi mpaka siku ya 14. hii ni kwa wanawake wengi. Ila si wote. Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla ya kupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12 nyuma, kisha toa siku 4 mnyuma ndani ya siku nne zizi ndizo yai hutolewa. siku hizi ndizo moja wapo yai hutolewa.Kwa mfano:--
1.Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla ya kuingia hedhi (21 - 12 = 9) kisha toa nne nyuma (9-4=5) basi mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 5 na 9 katika siku zake.2.Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kabla ya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku nne tena nyuma (20-4=16) kwa hiyo mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 16 mpaka 20.3.Mwanamke mwenye siku 28: 28-12 = 16 kisha toa siku 4 nyuma 16 - 4 = 12. hivyo siiku ambazo yai hukomaa kwa mwenye siku 28 ni kati ya 12 mpaka 16.Sasa baada ya kuzijua siku hizi ambazo yai hukomaa, inabidi ufahamu kuwa yai la mwanamke huweza kuishi kati ya masaa 12 mpaka 24 toka kukomaa (ovulation). kwa upande mwingine mbegu za kiume huisho kati ya siku 3 mpaka 5. hivyo ujauzito unaweza kutungwa kwa mbegu ambayo ilikuwepo toka siku tatu zilizopita.
Mimba hutokea pindi mbegu ya kiume (sperm) inapokutana na yai la mwanamke (ova) na kuungana kwa pamoja kutengeneza selli moja iitwayo zygote. Seli hii hukuwa na kujakuwa mtoto kamili. Kawaida kitendo hiki hufanyika ndani ya masaa 12 toka yai kukomaa na kuletwa kwenye mirija ya falopian. Baada ya mimba kutungwa itabakia pale kwa masaa kama matatu, kisha huanza kusafirishwa na kupelekwa kwenye tumbo la mimba ambapo huku litabakia mpaka mtoto kuzaliwa.Mwanamke hutoa yai moja kila mwezi kutoka katika ovari moja. Kuna wakati mwanamke huenda akatowa mayai zaidi ya moja, hali hii si kawaida. Yai hili linaweza kuwa hai ndani ya masaa 12 mpaka 24. hutokea pia likaweza kuwa hai mpaka masaa 48. ndani ya muda huu yai ni lazima likutane na mbegu ya kiume ili mimba itungwe. Kipindi hiki kitaalamu kinajulikana kama fertile window.Mbegu ya mwanaume huweza kudumu kuwa hai ndani ya siku 5, ndani ya siku hizi mbegu hizi huwa zipo hai hivyo zinaweza kurutubisha yai. Mwanaume huto zaidi ya mbegu milioni 300 ejaculation moja. Katika mbegi hizi mbegu moja ndio hutakiwa kuungana na yai.Siku za mwanamke kuweza kuwa kati ya 21 mpaka 35 inategeme na mwanamke. Kikawaida walio wengi siku zao ni 28. katika siku hizi zipo siku 6 tu ambazo mwanamke anaweza kupata ujauzito. Siku hizi huanzia siku ya 11,12,13,14,15 na 16. katika siku hizi siku ya 14 ndio ambayo huaminika zaidi kuwa yai hutolewa ziku hii. Ni vyema kukutana kimwili katika siku hizi kwa wanaotafuta ujauzito. Sio lazima pia kufululiza inawezekana kuruka ila nivyema kutoikosa siku ya 13 na 14.
NI IPI HASA SIKU AMBAYO NITAFUTE UJAUZITO?
Kama ulipojifunza hapo juu kuwa zipo siku maalaumu ambazo yai hukomaa. Katika siku hizo mojawapo yai huletwa kwenye mirija ya falopia. Baada ya kukokotoa siku zako hapo juu sasa itakubidi kuongeza siku moja ama mbili nyuma. Hii ni kwa sababu makadirio ya siku hutofautiana. Na si lazima kkutafuta toto katika siku zote hizi. Unaweza kuruka kwa siku moja moja.Jitahidi kufanya tendo la ndoa hasa katika siku hizo nne ulizozipata baada ya kukokotoa. Katika siku hizo jitahidi kufanya tendo siku ambayo itakuwa na sifa zifuatazo:-1.Majimaji ya mwanamke ukeni yatakuwa ni mengi kuliko siku zilizopita. Mwanamke mwenyewe anaweza kujichunguza hali hii na kuigundua ila taabu. Anaweza kutumia kidole ama kitambaa safi kuchunguza uwepo wa majimaji haya katika ukeni kwake. Kumbuka hali hii isiambatane na shida nyingine za afya kama PID. Wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kuchunguza hasa kwa wale wanaotumia uzazi wa mpango hasa hasa kwa kutumia vidonge vya homoni.2.Joto la mwanamke litakuwa ni kubwa kuliko siku nyingine. Joto hili sio homa, na lisiambatane na sababu nyingine kama maumivu ya kichwa, ama kutokana na kulala sana, ama misongo ya mawazo. Kikawaida siku ambayo yai hutolewa joto la mwanamke linakuwa kubwa hivyo akishiriki siku hii ujauzito ni rahisi kuingia.3.Siku ambayo mwanamke atakuwa na hamu sana ya kushiriki tendo. Wakato ambapo yai hutolewa kuna homoni huzalishwa kwa wingi. Homoni hizi zinaweza kusababisha mwanamke kutamani sana kushiriki tendo zaidi ya siku nyingine.Pindi mwanamke atakapojigundua kuwa siku hii ameipata basi ni vyema kushiriki tendo ndani ya siku hii ama siku itakayofata haraka iwezekanavyo, maana yai la mwanamke linaweza kufa ndani ya muda mchach masaa 12 mpaka 24.Kuna baadhi ya wanawake wanapata changamoto kutokana na kuwa na shida ya homoni katika mfumo wao wa uzazi. Hawa ni wale ambao siku zao hawazipati katika mpangilio sawa. Ni vyema wakafika kituo cha afya kupata matibabu ya tatizo hilo.