Suratul-takaathur (102) imeteremshwa makkah Ina aya nane
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
- Suratul- Takaathur (102): Imeteremshwa Makkah, Ina Aya Nane.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
- Kumekughafilisheni (katika) kutafuta wingi (wa mali na jaha na watoto na kujifakharisha kwayo).
- Hata mmeingia makaburini (mmekufa kabla ya kufanya kheri yeyote).
- Sivyo hivyo! Karibuni hivi mtajua (kuwa sivyo hivyo).
- Kisha (nasema) sivyo hivyo karibuni hivi mtajua (kuwa sivyo hivyo).
- Sivyo hivyo! Lau kama mnajua ujuzi wa yakini (kuwa sivyo hivyo msingefanya hivyo).
- Hakika mtauona moto wa Jahiym.
- Kisha (nasema) mtauona (moto) kwa yakini.
- Kisha kwa hakika mtaulizwa siku hiyo juu ya neema mlizopewa (mlizitumiaje).
Mafunzo kwa Ufupi.
- Pupa katika kutafuta anasa za dunia ndizo hupelekea mtu kumuasi Mwenyezi Mungu (s.w).
- Kuchuma mali na kuhangaikia watoto sio jambo baya, bali lisitusahaulishe katika kumtumikia Mwenyezi Mungu (s.w).
- Kuwepo siku ya mwisho ni jambo lisilo na shaka ili kila mtu akaulzwe juu ya jinsi alivyotumia neema alizopewa.
- Kutumia vibaya neema na vipawa tulivyonavyo hupelekea kumuasi Mola wake na hivyo kustahiki adhabu.
- Neema na vipawa tulivyonavyo ni dhamana kwetu na tutaulizwa siku ya Kiama.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Share follows: 0 |
Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 ai web app 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
👉1 ai web app 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Sababu za kushuka sural Masad (tabat haraka)
Sura hii inazungumzia kuhusu hali ya Abulahab namke wake wakiwa kama Watu waovu. Ni moja katika sura ambazo zilishuka mwanzoni toka Mtume alipoamrishwa kulingana dini kwa uwazi.
Soma Zaidi...Kitabu Cha Darsa za Quran
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...ASBAB-NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN
ASBAB NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN Quran imeteremka kwa muda wa miaka 23 kidogokido.
Soma Zaidi...