Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua.
Maana ya Swala
Maana ya Swala kilugha
(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua. Katika Qur-an tunaamrishwa kumswalia Mtume, yaani kumuombea dua Mtume (s.a.w) katika aya ifuatayo: Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Mtume (wanamtakia Rehema). Basi, enyi mlioamini mswalieni (muombeeni au mtakieni Mtume) Rehema na muombeeni amani (33:56)
Vile vile katika Hadith, Mtume (s.a.w) anatuambia: Yule atakayealikwa kwenye karamu ya harusi aitikie wito huo, kama hataweza kuitika amswalie (amuombee dua) aliyemkaribisha. (Muslimu).
Maana ya swala Kisheria:
(b) Kisheria Katika sheria ya Kiislamu, swalaa ni maombi maalumu kwa Allah (s.w) yanayofanywa kwa kufuata utaratibu maalumu uliowekwa na Allah (s.w) na kufundishwa kwa matendo na Mtume wake. Katika maombi haya maalumu mwili mzima huhusika katika maombi haya kwa kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, kukaa na kuzingatia yale yote anayosema katika kuleta maombi haya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutawadha kama vile ambavyo alitawadha Mtume
Soma Zaidi...Maana ya TalakaTalaka ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa waliofunga mume na mke wakati wa kufunga ndoa mbele ya mashahidi wawili.
Soma Zaidi...Aina za Swala za Sunnah.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuhusu taratibu za ibada ya itiqaf yaani kukaa msikitini kwa ajili ya ibada.
Soma Zaidi...