image

Swala ya Istikhara na jinsi ya kuiswali

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya Istikhara

Istikhaarah maana yake ni kuomba uchaguzi au aumuzi katika jambo. Na Swalaah ya Istikhaarah hakika ni zawadi kubwa tuliyopewa sisi Umma wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani ina faida kubwa sana kwetu kwani hatuamui jambo letu tunaloliomba katika Swalaah hii, ila baada ya kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atuongoze Yeye hilo jambo kama lina kheri na sisi Atufanikishe nalo na kama ni la shari Atuepushe nalo. Yeye Pekee Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Mwenye kujua ya ghayb yaani yatakayotokea siku za mbele.

 

 

Na ndio ilivyokuja katika Du'aa kuwa tunasema:

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْتَخيـرُكَ بِعِلْمِك، وَأسْتَقْـدِرُكَ بِقُـدْرَتِـك، وَأَسْـألُـكَ مِنْ فَضْـلِكَ العَظـيم، فَإِنَّـكَ تَقْـدِرُ وَلا أَقْـدِر، وَتَـعْلَـمُ وَلا أَعْلَـم، وَأَنْـتَ عَلاّمُ الغُـيوب، اللّهُـمَّ إِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ (وَيُسَـمِّي حاجته) خَـيْرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، عَاجِلِهِ و آجِلِه , فَاقْـدُرْهُ لي وَيَسِّـرْهُ لي ثـمَّ بارِكْ لي فيـه، وَإِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ شَـرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، عَاجِلِهِ و آجِلِه فَاصْرِفْـهُ عَنّيِ وَاصْرِفْني عَنْـهُ وَاقْـدُرْ ليَ الخَـيْرَ حَيْـثُ كانَ ثُـمَّ أَرْضِـني بِـه.

Ee Allaah hakika mimi nakutaka (muongozo) unichagulie kwa ujuzi Wako, na nakuomba Uniwezeshe kwa uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako kubwa, hakika Wewe Unaweza, nami siwezi, Nawe unajua nami sijui, Nawe ni Mjuzi wa ya ghayb. Ee Allaah, iwapo jambo hili kutokana na ujuzi Wako (utalitaja jambo lako) lina kheri na mimi katika Dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu, katika Dunia yangu na Aakhirah yangu, basi nakuomba Uniwezeshe nilipate, na Unifanyie wepesi, kisha Unibariki. Na iwapo Unajua kwamba jambo hili ni shari kwangu katika Dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu, katika Dunia yangu na Aakhirah yangu, basi liepushe na mimi nami niepushe nalo, na nipangie jambo jengine lenye kheri nami popote lilipo, kisha niridhishe kwalo. [Al-Bukhaariy]

 

 

Kwa hiyo inampasa Muislamu awe anaitumia sana Swalaah hii kwa kila jambo lake, likiwa ni dogo au kubwa kwani juu ya kupata faida ya kwamba unamuachia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Mwenye Ujuzi na Mwenye Hikma kutuongoza, pia unapata thawabu za kuswali Raka'ah mbili.

 

Lakini haifai kuswali Swalaah hii kwa ajili ya maasi na maovu au hata katika ‘ibaadah za fardhi. Mfano mwizi haimpasi kuiswali Swalaah hii ili atake uamuzi kama akaibe au la. Au mwanamke asiiswali Swalaah hii ikiwa yuko katika wasiwasi wa shaytwaan unaotaka kumpelekea kufanya zinaa na kadhalika.

Vile vile asiswali mtu Swalaah hii katika kutimiza fardhi; mfano katika kutoa Zakah au jambo la kheri kama swadaqah na kadhalika, kwani huo ni wasiwasi wa shaytwaan kukuzuia kutenda hayo yanayopasa kutendwa.

 

 

Swalaah hii inaweza kutumika katika mambo yanayofaa mfano unataka kwenda safari, au umeomba kazi katika shirika fulani, au unataka kuoa au mwanamke amekuja kuposwa na kadhalika.

 

Vile vile unapokuwa na uamuzi wa mambo mawili na hujui jambo lipi mojawapo ni lenye kheri, mfano unayo akiba yako ya fedha na kuna fursa ya kufungua mojawapo ya biashara za aina mbili, sasa hujui biashara gani katika hizo ndio yenye kheri na wewe, hapo utaswali ili upate mwongozo wa biashara itakayokuwa na kheri na wewe.

 

Kisha baada ya kuswali Swalaah hii kwa mambo yanayofaa kuiswalia, inakuwa umeshamuachia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akuongoze, kwa hiyo vyovyote utakavyoamua itakuwa ndio mwongozo Wake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na itakuwa ndio kheri yako.

 

 

Si lazima mtu aote ndoto kama wanavyofikiria baadhi ya watu baada ya kuswali Swalaah hii.

 

 

Swalaah hii haiswaliwi kwa niyyah kuomba haja kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) unapotaka kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) haja yoyote, ni kuomba Du'aa mwenyewe kama kawaida ikiwa ni katika Swalaah au nje ya Swalaah

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1230


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Njia za kudhibiti riba
Ufumbuzi wa tatizo la ribaRiba imeenea na kuzoeleka duniani kwa kiasi ambacho watu wengi wanadhani kuwa bila riba hakuna shughuli yoyote ya uchumi inayowezekana. Soma Zaidi...

walioruhusiwa kufungua (kula) mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

Je matapishi ni hadathi ndogo? Au hayatengui udhu
Asalaam alaikum. Soma Zaidi...

Mwenendo wa mwenye kunuia hijjah na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mambo yenye kufunguza swaumu (funga)
Soma Zaidi...

Tofauti kati ya fiqh na sheria
Kipengele hichi tutajifunza tofauti kati ua fiqh na sheria. Soma Zaidi...

Namna ya kujitwaharisha mkojo wa Mtoto mdogo Najisi Hafifu
Soma Zaidi...

Ni zipi nguzo za swaumu na masharti ya Swaumu
Soma Zaidi...

Hii ndio namna ya kuswali kama alivyoswali Mtume s.a.w
Mtume (s. Soma Zaidi...

Hatua za kinga za ugumba na Utasa.
Ugumba ni “ugonjwa wa mfumo wa uzazi unaofafanuliwa kwa kushindwa kupata ujauzito baada ya miezi 12 au zaidi ya kujamiiana bila kinga mara kwa mara. Utasa  kutoweza kwa kiumbe hai kufanya uzazi wa ngono au kutoweza kupata mimba au kuchangia mimba. Soma Zaidi...

Utaratibu wa kuzika, hatua kwa hatua, na namna ya kusindikiza jeneza
4. Soma Zaidi...

maana ya Eda na aina zake
Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine. Soma Zaidi...