SWALA YA WITIRI NA FAIDA ZAKE, NA JINSI YA KUISWALI


image


Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya witiri na faida zake kwa mwenye kuiswali.


3. Swala ya Witri
Witri maana yake ni namba isiyogawanyika kwa mbili kama vile 1, 3, 5, 7, 9, 11 n.k. Sunnah ya witri huswaliwa katika kipindi cha usiku baada ya swala ya Al-Isha na kabla ya kuingia swala ya Al-Fajiri. Lakini ni bora kuichelewesha Witri na kuiswali katika theluthi ya mwisho ya usiku, baada ya swala ya kisimamo (tahajjud).

 


Mtume (s.a.w) alikuwa akiswali Witri pamoja na swala ya Tahajjud (Swala ya Usiku) na wakati mwingine alikuwa akiswali Witri mara tu baada ya Al-Ishaai. Ni vema kuswali witri baada ya al-Isha kama hakuna uhakika wa kuamka Usiku. Mtume (s.a.w) ameikokoteza sana swala ya Witri kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo:

 


Buraydah (r.a) amesimulia, Nimemsikia Mtume (s.a.w) akisema; Witri ni haq (wajibu). Asiyeswali si miongoni mwetu. Witri ni wajibu”. (Abu Da udi)

 


Witri ina swaliwa kwa rakaa tatu. Huswaliwa kwa rakaa mbili na kutoa Salaam, kisha hukamilishwa na rakaa moja.

 


Namna ya Kuswali Swala ya Witri
1. Katika rakaa ya kwanza utasoma Sura ya Al-A’alaa (Sabbihisma) baada ya Suratul-Faatiha.

 

Katika rakaa ya pill utasoma Suratul-Kaafiruuna baada ya suratul-faatiha..

 


Katika rakaa moja ya mwisho. baada ya kusoma Suratul-Faatiha, utasoma Suratul- lkhlas, AI-Falaq na An-naas. Kuleta Qunut (dua) katika rakaa ya mwisho katika ltidali.

 

Dua tunayoileta katika Qunut ni hii ifuatayo:

 

Allahumma ihdidaa fii man hadaita "Ewe Mola n[ongoze kama wale uliouxiongoza"

 


Wa `aafinaa fiiman `aafaita "Na unininusuru kama hao uliowarursuru"

 


Watawallanii fiiman tawaffaita "Na unitawalishe pamoja na wale ulio watawalisha

 


wabaarik lii fii maa a'atwaitanii "Na unitilie pataka katika vile ulivyonipa

 


Waqinii sharra maa gadhwaita "Unikinge na shari ulizonikadiria"

 

Tabaarakta rabbanaa wata’aalaita "Ni nyingi kabisa juu yetu baraka zako na umetukuka kweli kweli"

 

Ni muafaka kuleta dua nyinginezo vile vile kulingana na haja ya mwenye kuswali.

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    5 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    6 Magonjwa na afya    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Taratibu za mirathi katika zama za ujahilia
Kabla ya kuhubiriwa uislamu watu wa Maka walikuwa na tarayibu zenye dhuluma ndani yake katika ugawaji wa mirathi. Soma Zaidi...

image Swala ya witiri na faida zake, na jinsi ya kuiswali
Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya witiri na faida zake kwa mwenye kuiswali. Soma Zaidi...

image Dhana ya kumiliki raslimali katika uislamu
Ni ipi raslimali ya halali kuimiliki katika uislamu. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa
Post hii itakufundisha taratibu za kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...

image Taratibu za kuchaguwa mchumba katika uislamu
Hapa utajifunza hatuwa kwa hatuwa za kuchaguwa mchumba kulingana na sheria za kiislamu. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kuoga josho la kiislamu ( janaba, hedhi na nifasi)
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kuoga josho kisheria. Soma Zaidi...

image Taratibu za eda ya kufiwa katika uislamu
Hapa utajifunza taratibu za kukaa eda kwa mwanamke ambaye amefiwa na mume. Soma Zaidi...

image Yajuwe masharti ya udhu yaani yanayofanya udhu kukubalika
Posti hii itakufundisha masharti yanayohitajika kwa mwenye kutaka kutia udhu. Soma Zaidi...

image Kwa nini waislamu wanaoa mke zaidi ya mmoja
Post hiibitakugundisha hekima ya kuruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja katika sheria za kiislamu. Soma Zaidi...

image Umuhimu wa uchumi katika uislamu
Post hii itakufundisha faida na umuhimu wa kijenga uchumi katika jamii ya kiislamu. Soma Zaidi...