Kusimamisha Swala.
Kusimamisha Swala.
Maana ya Kusimamisha Swala Kusimamisha swala ni tofauti na kuswali. Kuswali ni kufanya vitendo vya swala kama vile kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, n.k.
Kusimamisha swala ni kuitekeleza swala kwa kuchunga na kutekeleza kwa ukamilifu yafuatayo:
(i) Sharti zote za swala.
(ii) Nguzo zote za swala.
(iii) Kuwa na khushui (unyenyekevu) wakati wote wa kutekeleza sharti na nguzo za swala.
Mtu akiswali bila ya kuzingatia na kutekeleza kwa ukamilifu mambo haya matatu, ataonekana kuwa kaswali, lakini atakuwa hajasimamisha swala na atastahiki kuadhibiwa vikali na Mola wake kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:  Basi adhabu kali itawathibitikia wanaoswali, ambao wanapuuza swala zao (kwa kutozisimamisha), ambao hufanya ria (107:4-6).
 Kupuuza swala ni pamoja na kutotekeleza ipasavyo sharti za swala, nguzo za swala, na kutokuwa na unyenyekevu wakati wa kutekeleza sharti na nguzo za swala. Hivyo, swala inayokubalika mbele ya Allah (s.w) ni ile iliyosimamishwa kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo: Hakika wamefuzu waumini ambao katika swala zao ni wanyenyekevu. (23:1-2) Na ambao swala zao wanazihifadhi. (23:9) Kuhifadhi swala ni kutekeleza kwa ukamilifu sharti na nguzo zote za swala.
    
    
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inakwenda kukujuza kuhusu swala za qabliya, baadiya na tahiyatul masjid.
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kuswali, zijuwe aina za swala na ujifunze masharti ya swala, kwa nini swala hazijibiwi? nini kifanyike?
Soma Zaidi...Post hii itakujuza jinsi ya kiswali swala ya tahajudi. Pia utajifunza jinsi ya kuswali swala za usikubyaanibqiyamublayl
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza mambo ambayo ni haramu kwa mwanamke aliye na hedhi na nifasi
Soma Zaidi...Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii.
Soma Zaidi...Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...