image

Taasisi za kisiasa za msingi alizotumia mtume (s.a.w) katika kuanzisha dola ya kiislamu madinah

Dola ya kiislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

 

  1. Kujenga Msikiti.

-  Msikiti ulikuwa ndio Ikulu, mahakama, kituocha jeshi, ukumbi wa bunge (shura), n.k. Qur’an (3:95), (2:150).

-  Ulikuwa kituo muhimu cha kiharakati katika kusimamisha na kuendeleza Uislamu. Rejea Qur’an (22:40), (2:114), (72:18) na (9:19).

 

  1. Kujenga Ummah wa Kiislamu.

-  Mtume (s.a.w) aliwapatanisha kabila la Aus na Khazraj Madinah waliokuwa na uadui wa muda mrefu baina yao. Qur’an (3:103).

-  Mtume (s.a.w) pia aliwaunganisha udugu imara kati ya Muhajirina wa   

-    Makkah na Answaar wa Madinah na kuwa ummah mmoja. Qur’an (8:75).

-  Pia aliimarisha uchumi kwa kuunganisha ummah wa Kiislamu na kuwa kitu  kimoja. Qur’an (59:8-9).

 

  1. Kuweka Mkataba wa Madinah (Madinah Charter).

-  Mtume (s.a.w) alijieleza katika mkataba huo kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na ndiye kiongozi mkuu wa Dola ya Kiislamu.

-  Mkataba uliainisha vipengele vya amani na wajibu wa kila kundi kati ya makabila ya Mayahudi na Waarabu washirikina wa Madinah na Dola ya Kiislamu Madinah. 

-  Uliainisha nafasi, majukumu na wajibu wa waumini katika Dola.

-  Mkataba uliainisha uhuru wa kila mtu kuabudu kwa mujibu wa imani na dini zao.

           

  1. Kuweka Mikataba ya amani na Makabila ya Mayahudi na mengine yaliyokuwa pembezoni mwa Dola ya Kiislamu Madinah.

-  Makabila na koo tatu za Kiyahudi zenye nguvu zilizokuwa pembezoni mwa mji wa  Madinah yalikuwa;

 

  1. Kuunda Shura na Sekretarieti.

-  Mtume (s.a.w) aliteua washauri wake wakuu katika kuendesha Dola ambao Walikuwa Abu Bakr (r.a), Umar bin Khattab (r.a), Uthman bin Affan (r.a), Ally bin Abu Twalib (r.a) na Hamza bin Abdul-Muttalib (r.a).

 

-  Aliteua waandishi maalumu wa kuandika na kutunza mikataba, takwimu, kumbukumbu na nyaraka zote za Dola ya Kiislamu Madinah. 

 

  1. Kuandaa Ummah wa Kiislamu Kijeshi na Kiusalama.

-  Mtume (s.a.w) aliwaanda na kuwahimiza waislamu kuwa wakakamavu na hodari katika shabaha, mieleka na kutumia silaha.

-  Kila Muislam alikuwa mpiganaji na mpelelezi dhidi ya maadui wa waislamu na Dola ya Kiislamu.  Rejea Qur’an (4:71).

-  Aliunda na kuweka vikosi vya doria na ulinzi kuzunguka mipaka ya Dola ya Kiislamu Madinah. Qur’an (8:26).

 

  1. Kuimarisha Uchumi.

-  Mtume (s.a.w) aliwahimiza waislam kufanya kazi kwa bidii ili kujiimarisha Kiuchumi na kuendeleza Dola.

-  Utoaji wa Zaka, Sadaka na mapato mengine yalihimizwa na kukusanywa Kijamii na kuboresha huduma za jamii.

Rejea Qur’an (22:41).





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 891


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Nabii Ibrahiim(a.s) Kumlingania Uislamu Baba Yake
Baada ya NabiiIbrahiim(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME DHUL-KIFL(A.S)
Mtume Dhul-kifl ananasibishwa na Ezekiel anayetajwa ndani ya Biblia. Soma Zaidi...

Uasi katika dola ya kiislamu na matokeo yake
Uasi katika dola ya kiislamu na matokeo yake. Soma Zaidi...

Mji wa Makkah na kabila la kiqureish
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME YUNUS(A.S)
Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...

Kuingia Kwa Uislamu Tanzania na Afrika Mashariki
Soma Zaidi...

Watu wa Mji Waliomuua Muislamu kwa Kuwa Amewasadikisha Wajumbe wa Allah(s.w)
Katika Suratul Yassin Allah(s. Soma Zaidi...

Khalifa na Utungaji Sheria, na utiifu juu ya sheria na usimamiaji wa haki
Soma Zaidi...

Nasaba ya Mtume Muhammad S.A.W na familia yake.
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 1 Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika Surat Ar-Raad (13:19-26)
Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na hijrah ya mtume na maswahaba wake
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao
Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a. Soma Zaidi...