image

Taratibu za kumiliki hisa na mali ya shirika

Katika Uislamu kuwa na hisa kwenye mali inaruhusiwa. Hapa utajifunza taratibu za kumiliki hisa.

Mali yenye kuchangiwa mtaji kwa hisa

Mtu akishaamua kuuza hisa (share) kwa watu wengine kwa ajili ya mali fulani katika sheria ya Kiislamu anapoteza umilikaji wa mali wa mtu mmoja. Kuuza hisa kwa wengine kwa maana nyingine ni kukaribisha watu wengine kushiriki katika umilikaji wa mali ile. Nafasi ya mtu katika kumiliki mali hiyo itategemea idadi ya hisa alizonazo katika mali ile. Wenye hisa inabidi washirikiane katika faida na hasara pamoja na gharama za uendeshaji.

 

Faida anazopata atakayekuwa mwenye kumiliki mali
Zipo faida kadhaa ambazo atakayekuwa mwenye kumiliki mali huzipata kwa kufuata ushirika katika biashara, mtaji na faida (Shared Equity and rental) badala ya kupata mikopo ya biashara yenye riba. Faida kubwa atakayopata ni fadhila za Allah (s.w.) kwa kule kuepuka kwake kutoa riba kwa mkopo atakaopata. Tunajifunza katika Hadithi za Mtume (s.a.w.) kuwa laana ya Allah (s.w.) huwafikia wote wanaohusika na riba (mtoaji, mpokeaji, shahidi). Hata hivyo kuna faida nyingine ambazo anaweza kuzipata:

 


(i) Atakayekuwa mwenye kumiliki mali kwa kutochukuwa mkopo wenye masharti ya riba hujiepusha kabisa na hatari ya kunyang’anywa mali yake (aliyoweka rahani) akishindwa kutimiza masharti yake.

 


(ii)Fedha ambayo angeitoa kama riba kwa ajili ya mkopo atabaki nayo na kutumia kwa shughuli nyingine kuendeshea maisha yake.

 


(iii)Atakuwa na uhakika wa kupata sehemu halali ya faida inayotokana na mali hiyo (kama ipo). Kadhalika kama ikitokea hasara haitamlazimu kubeba mzigo wote wa hasara kwani ushirika katika biashara huhusisha vile vile umuhimu wa kugawana hasara itokeapo.

 


Faida kwa wenye kununua hisa
Mwenye kununua hisa huchangia katika mtaji. Naye huepuka ghadhabu za Allah (s.w.) za utoaji mkopo kwa riba. Zaidi ya haya hupata faida zifuatazo:

 


(i) Hupata sehemu ya faida itokanayo na mali hiyo kulingana na mchango wake kwenye biashara (idadi ya hisa alizonazo).

 

(ii) Huwa na sauti kwenye mali kwani naye pia ni mwenye kumiliki mali ile mpaka atakapouza hisa zake. Isitoshe hutoa kiwango kidogo kujipatia haki ya kumiliki ukilinganisha na mtaji mzima.

 


Kwa ujumla jamii nzima itanufaika kwa kuacha mfumo wa mikopo kwa riba na kuhimiza watu kufanya ushirika katika biashara. Ilivyo waliokopeshana kwa riba hawawi katika uhusiano mzuri kiroho. Aliyekopeshwa ilimbidi kufanya hivyo kutokana na shida aliyokuwa nayo. Kutoa kwake riba anakufanya kwa kuwa anafahamu hatari za kutofanya hivyo (kupoteza mali yake) ingawa kitendo hicho kinamuuma sana rohoni. Hivyo urafiki kati ya mkopeshaji na mkopeshwaji huwa ni wa kinafiki. Jambo hili ni wazi sana katika jamii ya dunia ya sasa. Hebu fikiria athari za mikopo hii kwa nchi masikini duniani. Ni mara nyingi nchi masikini zimekuwa zikipiga kelele aidha kupunguziwa au kufutiwa kabisa baadhi ya madeni yao. Sehemu kubwa ya madeni hayo ni limbikizo la riba la miaka mingi.

 


Hivyo Uislamu unapiga vita riba kutokana na madhara yake kibinafsi, kitaifa na kimataifa. Aidha Uislamu unahimiza ushirikiano katika biashara kama ufumbuzi wa tatizo la riba.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 749


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Hadhi na Haki za Mwanamke Ulaya chini ya kanisa hapo zamani
Soma Zaidi...

Namna ya kuhiji, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...

Sharti za kutoa zaka
Masharti ya Utoaji wa Zakat na Swadaqat Utoaji katika njia ya Allah (s. Soma Zaidi...

Ni zipi sifa za imamu wa swala?
Soma Zaidi...

Haki za binadamu kwa ujumla (basic human rights)
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Usitamani kifo hata ukiwa mchamungu mno ama muovu mno
Katika uislamu imekatazwa kutamani kufa hata kama utakuwa ni mtu muovu sana ama mchamungu sana. Soma Zaidi...

Haki na wajibu wa mke kwa mumewe na familia
Soma Zaidi...

sadaka
Soma Zaidi...

Kumuandaa maiti punde baada ya kufariki dunia
Soma Zaidi...

Utaratibu wa kuzika, hatua kwa hatua, na namna ya kusindikiza jeneza
4. Soma Zaidi...

Ni nini maana ya twahara na kujitwaharisha?
Posti hii inakwendabkukujiulisha maana ya twahara na jinsi ya kujitwaharisha. Soma Zaidi...

Ni nini maana ya swala
Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu maana halisi ya ibada ya swala. Soma Zaidi...