Mtume alipoanza kulingania uislamu na changamoto alizokumbana nazo kutoka kwa maadua wa uislamu

7.3Mtume (s.a.w) Kuulingania Uislamu Makkah kwa siri.
- Mtume (s.a.w) alianza kulingania familia yake, kisha rafiki zake na jamaa zake wa karibu walio rafiki.- Mtume (s.a.w) alianza kulingania Uislamu kwa siri kwa muda wa miaka mitatu kwa kukutana na waislamu waliosilimu mwanzo kabisa katika nyumba ya bwana Arqam bin Arqam – maarufu kama Darul-Arqam.


Mtume (s.a.w) kuutangaza Uislamu Makkah kwa jamii nzima.
- Baada ya miaka mitatu ya kuulingania Uislamu kwa siri, aliamrishwa kuutangaza sasa hadharani kwa jamii yote inayomzunguka.- Mara tu baada ya Mtume (s.a.w) kuutangaza ujumbe wa Uislamu hadharani, alikumbana na Upinzani dhidi ya ujumbe wake huo kutoka kwa Makafiri wa Kiqureish wa Makkah.Sababu za Makafiri wa Kiqureish kuupinga ujumbe wa Uislamu.
i.Walihofia kupinduliwa mfumo wao wa utawala kandamizi na kusimama mfumo wa Uislamu unao simamia haki na uadilifu.

ii.Walihofia kupoteza maslahi yao kupitia njia kandamizi, nyonyaji na haramu katika jamii zao.

iii.Walihofia kukosa wafuasi ambao ndio ilikuwa rasilimali pekee katika kuendeleza na kuimarisha unyonyaji wao.

iv.Walihofia kupoteza nafasi yao katika kuiongoza jamii kama fursa pekee ya kunyonya, kudhulumu na kulinda maslahi yao.

v.Walihofia kupoteza umaarufu na nafasi ya ibada (itikadi) zao za kishirikina ambazo ndizo nyenzo pekee za mapato yao.