Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo

Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo.

Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo

Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo.


Makafiri wanadai kuwa kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) ni ububusa na kufuata mkumbo bila ya udadisi na kutumia akili. Dai hili sio la kweli kwa sababu zifuatazo;


Kwanza, Mwenyezi Mungu (s.w) ametuma Mitume mbali mbali kwa wanadamu ili kuwafundisha na kutoa dalili za kuwepo kwake bila ya shaka yeyote kwa dalili za wazi ili kumfahamu na kuweza kumuabudu ipasavyo.
Rejea Qur'an (4:165).



Pili, Vipawa, ufahamu na akili alivyopewa mwanaadamu ni kumuwezesha kumtambua Muumba wake na kuweza kumuabudu inavyostahiki. Hivyo kutotumia akili katika kumtambua Mwenyezi Mungu kupitia ishara mbali mbali ni kustahiki adhabu.
Rejea Qur'an (3:190), (30:21), (7:179), (8:22) na (12:105).



Tatu, Mitume wa Mwenyezi Mungu pamoja na kuwafundisha wafuasi wao juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu, hawakuwataka kuamini na kufuata bila ya hoja na dalili za wazi bali walionyesha ishara na miujiza kuthibitisha ujumbe wao.



Nne, Msisitizo wa Elimu katika Qur'an kuwa faradhi ya kwanza kama nyenzo pekee ya kumuwezesha mwanaadamu kumjua na kumuabudu Mola wake na kuweza kuyamudu mazingira yanayomzunguka na kuweza kusimamisha Ukhalifa ardhini.



Tano, Maana ya neno 'imani' ambalo lina maana ya 'kuwa na yakini moyoni pasina shaka' yeyote juu ya jambo fulani kwa kuwa na ujuzi nalo na pia kupitia dalili na ishara za kutosha za kuonyesha kuwepo kwake.



                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 415


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Mambo gani ni Haramu kwa mwenye janaba?
Hadathi ya kati na kati (Janaba). Soma Zaidi...

ADABU ZA KUOMBA DUA
ADABU ZA KUOMBA DUA. Soma Zaidi...

Ushahidi juu ya kosa la Uzinifu
Ushahidi wa kuthibitisha kutendeka kwa kosa la uzinifu unapatikana kwa namna tatu zifuatzo: (i)Kushuhudia tendo hilo likifanyika kwa wakati mmoja watu wanne Mukalafu (Walio baleghe na wenye akili timamu), wakiwa ni Waislamu waadilifu. Soma Zaidi...

Imam Ibn Majah na Sunan Ibn Majah
Soma Zaidi...

Athari na faida za kumuamini Allah katika maisha ya mwanadamu duniani na akhera
Athari za Kumuamini Mwenyezi Mungu (s. Soma Zaidi...

Ibrahiim(a.s) Aomba Kupata Kizazi Chema
Nabii Ibrahiim na mkewe Sarah walikaa mpaka wakawa wazee bila ya kupata mtoto. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA IDGHAM
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

ADABU ZA KUSOMA QURAN
Adabu wakati wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...

kujiepusha na uongo na sifa za uongo
Uwongo ni kinyume cha ukweli. Soma Zaidi...

Maadili katika surat luqman
Soma Zaidi...

HARAKATI ZA DINI WAKATI WA MATABIINA NA TABII TABIINA
Soma Zaidi...

Upeo wa Elimu waliyokuwa nayo Mitume
Soma Zaidi...