Tembo

Posti hii inakwenda kukupa sifa za mnyama tembo

TEMBO

 

picTembo ni katika wanyama wa porini na ndiye mnyama mkubwa kuliko wote.Tembo anaweza kufika urefu wa mita tatu (3) mpaka mita 4 yaani fkuanzia futi 10 mpaka 13. Tembo anaweza kufika uzito wa kilo elfu saba (kg 7000) yaani tani saba. Mimba ya tembo inaweza kuchukuwa miezi 20 mpaka 22 yaani miaka miwili kasoro miezi miwili.

 

Tembo mtoto ananyonya mpaka kufikia miaka mitatu mpaka minne. Tembo mtoto akiwa na umri wa miaka 10 uzito wake unaweza kufika kilo 900 mpaka 1,300. Tembo anaweza kuishi zaidi ya miaka 60.Inakadiriwa kuwa idadi ya tembo wote waliopo duniani leo ni kati ya laki nne mpaka tano (400,000 - 500,000). Tembo majike huwa wanaishi kwenye makundi. Kundi hili la tembo lina watoto na wakee wanawake pamoja na mashangazi. Kiongozi wa kundi hili la tembo ni yule mkubwa kuliko wote. Watoto wa kiume wa tembo wanapofika umri wa miaka 6 hujitenga na kundi hili na kutembea pekee. Tembo majike hukutana na tembo matume unapofika muda wa kupata watoto.

 

picTembo ni katika wanyama wenye nguvu kwani anauwezo wa kuweza kung’oa mti pamoja na mizizi yake. Wataalamu wa sayansi wanashangazwa na uwezo wa nguvu za tembo. Kwani anauwezo wa kunyanyua vitu vikubwa na pia kwa mkinga wake anaweza kunyanyua vitu vyepesi kama tunda au majani. Wataalamu wa sayansi wametengeneza vifaa kama magreda kwa kuiga nguvu za tembo lakini bado vifaa vyao ijapokuwa vinanyanyua vitu vizito lakini havina uwezo wa kunyanyua vitu vyepesi.

 

Tembo anaweza kufundishwa na kutumika kwa shughuli kama kunyanyua mizigo ama usafiri. Tembo ana uwezo wa kusikia kwa umbali mrefu sana. Tembo hutumia mkonga wake wa ajili ya kuzungumza na wezie, kuwaonya na kuita mkutano. Pia hutumia mkonga wake kwa ajili ya kulia chakula, kuhifadhi maji ama kuoga. Tembo hutumia meno yake yaani mapembe kwa ajili ya kujilinda na kulinda familia yake dhidi ya wanyama walao nyama.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Mengineyo Main: Jifunze File: Download PDF Views 1973

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

WELCOME TO OUR LIBRARY

Karibu sana Kwenye Maktaba Yetu Sasa umefika kwenye maktaba ya vitabu.

Soma Zaidi...
Bongoclass

Bongoclass ni darasa la kushiriika akili na maarifa kutoka kwa watu mbalimbali katika kutumia fursa zilizopo ili kuzalisha kipato na kuleta maendeleo katika jami

Soma Zaidi...
Books

Vinjari ukiwa na vitabu vyetu ukiwa kwenye maktaba yetu

Soma Zaidi...
MAAJABU YA VIUMBE

MAAJABU YA VIUMBE Dunia ina maajabu sana lakini viumbe wana maajabu pia.

Soma Zaidi...
Cheetah

Posti hii inakwenda kukupa sifa za mnyama cheetah

Soma Zaidi...
Subscribe

Ingiza taarifa zako hapo chini uweze kupata Update zetu.

Soma Zaidi...
MAAJABU YA VIUMBE

MAAJABU YA VIUMBE Dunia ina maajabu sana lakini viumbe wana maajabu pia.

Soma Zaidi...