TEMBO NI KATIKA WANYAMA WENYE KUSHANGAZA SANA.


image


Tembo wana maajabu makubwa kama utazingatia kwa umakini umbo lake zuri.


Tembo anaweza kufika urefu wa mita tatu (3) mpaka mita 4 yaani fkuanzia futi 10 mpaka 13. Tembo anaweza kufika uzito wa kilo elfu saba (kg 7000) yaani tani saba. Mimba ya tembo inaweza kuchukuwa miezi 20 mpaka 22 yaani miaka miwili kasoro miezi miwili.

 

Tembo mtoto ananyonya mpaka kufikia miaka mitatu mpaka minne. Tembo mtoto akiwa na umri wa miaka 10 uzito wake unaweza kufika kilo 900 mpaka 1,300. Tembo anaweza kuishi zaidi ya miaka 60.Inakadiriwa kuwa idadi ya tembo wote waliopo duniani leo ni kati ya laki nne mpaka tano (400,000 - 500,000).

 

Tembo anaweza kufundishwa na kutumika kwa shughuli kama kunyanyua mizigo ama usafiri. Tembo ana uwezo wa kusikia kwa umbali mrefu sana. Tembo hutumia mkonga wake wa ajili ya kuzungumza na wezie, kuwaonya na kuita mkutano. Pia hutumia mkonga wake kwa ajili ya kulia chakula, kuhifadhi maji ama kuoga. Tembo hutumia meno yake yaani mapembe kwa ajili ya kujilinda na kulinda familia yake dhidi ya wanyama walao nyama.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    3 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    5 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya html kwa kiswahili    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Buibui hupuruka ijapokuwa hana mbawa.
Nataka nikufundishe moja katika maajabu ya mdudu Buibui kwa lugha ya kimombo spider. Soma Zaidi...

image Tembo ni katika wanyama wenye kushangaza sana.
Tembo wana maajabu makubwa kama utazingatia kwa umakini umbo lake zuri. Soma Zaidi...