Posti hii inahusu zaidi tiba ya awali kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID, tunaita tiba ya awali kwa sababu baada ya kupima na kugunduliwa kwamba una tatizo au changamoto ya PID ni vizuri kutumia tiba hiii baadae ndipo utumie dawa.
1. Kwanza kabisa napaswa kusisitiza kwamba hii tiba sio kwamba ni dawa ya kuponyesha bali ni maandalizi ya kutumia dawa ya PID kwa hiyo unapopatwa na tatizo la PID unapaswa kutumia tiba hii ndipo baadae unaweza kuendelea na dawa ulizoagizwa kufanya.
2. Unapaswa kuandaa tangawizi vipande vitatu na unaviosha vizuri kabisa ili kuondoa uchafu na wadudu wengine pia unazikuna kama hauna kikunio unaweza kuzitwanga na ziwe kama mfano wa unga hivi .
3. Baada ya kupata tangawizi zilizotwangwa unaandaa kitunguu swaumu punje kama kumi na tano hivi nazo uzitwange ziwe laini kama ilivyofanya kwa tangawizi .
4. Baada ya maandalizi ya vitunguu saumu andaa vitunguu maji vikate Kaye kwa vipande vidogo vidogo na hakikisha vimeoshwa kwa maji na kutakata vizuri.
5. Baada ya maandalizi ya tangawizi, kitunguu swaumu na vitunguu maji changanya vyote kwa ujumla weka maji ya moto na pia unaweza kuweka maji ya baridi , weka kiasi cha lita moja funika vizuri acha ikae kwa masaa sita baada ya hapo chuja vizuri unaweza kutunza kwenye jagi au kifaa chochote kile.
6. Tumia hayo maji kwenye glasi changanya na asali mbichi vijiko viwili tumia glasi moja asubuhi,moja mchana na nyingine jioni kwa mda wa siku moja baada ya hapo mwili utakuwa tayari umeuandaa vizuri kwa ajili ya kutumia dawa.
7. Pia tiba hii isitumiwe mara kwa mara na watu wenye matatizo ya vidonda vya tumbo kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha asidi.
8. Na kama nilivyotangulia kusema hii tiba sio kwa sababu ya kutibu PID bali ni kwa sababu ya maandalizi ya kuanza kutumia dawa za PID kwa hiyo ukitumia mchanganyiko huu unakusudia na kukupa maandalizi mazuri ya kutumia dawa za PID
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inaelezea kiufupi kabisa kuhusiana na Dalili za hatari kwa mama aliyejifungua.
Soma Zaidi...Tezidume ni moja ya magonjwa hayari yanayotokea katika mwili wa mwanaume.Hapa nimekuandalia sababu za kutokea kwa tezi dume.
Soma Zaidi...PEP Ni dawa ambazo utumiwa na watu wanaojamiiana na watu wenye virus vya ukimwi ila wenyewe hawawezi kupata kwa sababu ya kutumia dawa hizo.
Soma Zaidi...Hii ni hali inayowapata wanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Inatakiwa angalau nafasivkati ya mtoto na mtoto wapishane miaka miwili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea kwa sababu ya kuziba kwa mishipa ya uzazi, ni baadhi ya dalili ambazo ujitokeza kwa sababu ya kuwepo kwa tatizo la kuziba kwa mishipa ya uzazi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu msaada kwa mwenye maumivu ya tumbo la hedhi, hizi ni huduma ambazo utolewa kwa wale wenye maumivu ya tumbo la hedhi.
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukuletea orodha ya vyakla vinavyoaminika kuongeza nguvu za kiume.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba,ni vipimo vya moja kwa moja kutoka maabara na vingine sio vya maabara.
Soma Zaidi...