Quran (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Sura za Makkah |
Sura za Madinah |
1. Walengwa. Walengwa walikuwa waumini waliosimu mwanzo wa Utume. |
Zililenga Maadui wa Dola ya Kiislamu Madinah wakiwemo; Wanafiq, Washirikina, Wayahudi na Wakristo. |
2. Ujumbe. Sehemu kubwa ya ujumbe ni kujenga imani juu ya Mwenyezi Mungu (s.w), Malaika, Vitabu, Mitume, Siku ya Mwisho na Qudra yake. |
Ujumbe ulilenga ujenzi wa Dola na jamii ya Kiislamu Madinah kupitia sheria na hukumu mbali mbali. |
3. Muundo wa sura. Sura nyingi ni fupi na zina aya fupi fupi zenye lengo moja. |
Sura nyingi ni ndefu na zina aya ndefu zenye ufafanuzi zenye lengo la utekelezaji wa sheria.. |
4. Mbinu Zimetumia lugha fupi ya mchomo kwa walengwa kwa kutumia viapo, historia ya watu waliopita, kuwahofisha na kuwakatisha tamaa maadui wa Uislamu na kuwatia moyo na kuwaliwaza waumini katika kutekeleza ujumbe wa Qur’an. |
Zimetumia lugha ya sheria na ufafanuzi katika ujenzi wa Dola ya Kiislamu Madinah, kwa kutumia historia ya Mitume ili kuwaliwaza waumini kupigania Dini na kuwakatisha tamaa maadui wao wakiwemo; makafiri, washirikina, wanafiq na Wakristo. |
Umeionaje Makala hii.. ?
Surat al Baqarah ni katika sura ambazo tunapaswa tuwe tunasoma mara kwa mara. Post hii itakufundisha kuhusu fadhila za sura hii.
Soma Zaidi...Tarqiq ni kuisoma herufi kwa kuipa wepesi na tqfkhim ni kuisoma herufi kwa kuipa uzito.
Soma Zaidi...Sura hii imekuja kukata rai ya Makafiri wa Makka kuhusu ibada ya ushirika. Hivi leo tungesema kuhusu dini mseto.
Soma Zaidi...