Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba
Nini kilichangia ongezeko la uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba.
Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A.H
Hiki ni kipindi cha wafuasi wa Masahaba wa Mtume (s.a.w) katika karne ya pili Hijiriyyah 101-200 A.H. Katika kipindi hiki walitokea wanazuoni wengi waliojizatiti katika kazi ya ukusanyaji wa Hadith kutoka katika vituo mbali mbali vya mafunzo (Centres of Learning).
Wafuatao ni baadhi ya wanazuoni wa Hadith (Muhaddithina) waliojitokeza kutoka miji mbali mbali. Ma'mar bin Rashi wa Baghdadi; Said bin Abi Ubadah na Rabia bin Sabin wa Basra; Ibn Harith wa Baghdad; Abdul Malik bin Juraiji wa Makka; Walid bin Mubarrak wa Khurasan; Abu Bakr Shyaban wa Kufa na Sufyan bin Uyaina wa Madina.
Japo wanazuoni hawa walijitahidi sana katika hii kazi ya ukusanyaji Hadith, kazi zao bado hazikuwa zenye kutosheleza; isitoshe sehemu kubwa ya vitabu vyao ilihusu ripoti ya vituo vyao. Baada ya kazi hizi, kilitokea kitabu cha "al-Muwatta" cha Imam Malik bin Anas aliyeishi Madina kati ya 95 A.H na 179 A.H. Kazi ya Imam Malik ndiyo ya kwanza iliyowekwa katika mpango mzuri na kuwa kitabu cha kutegemewa na Umma. Imam Malik alifutu mas-ala ya Uislamu kwa kutegemea Qur-an na Hadith tu. Alianzisha umoja wa "Ahli Hadith" ambao kazi yake ilikuwa ni kukusanya Hadith na kuzitekeleza katika matendo.
Katika wakati huo huo alitokea Imam Abu Hanifa al-Numan bin Thabit (80-150) aliyefutu mas-ala mbali mbali ya Kiislamu kwa hoja na Qiyasi (deductions) baada ya kuzingatia Qur-an, Hadith na Ijma'i (makubaliano ya wanavyuoni). Hakuandika kitabu chochote cha Hadith lakini alikuwa mwanazuoni mkubwa wa "Qur-an na Hadith na alikuwa Muj-tahid na Mcha-Mungu.
Katika kipindi hiki hiki palitokea Maimamu wengine wawili mashuhuri. Imam Muhammad bin Idris al-Shafii (150-240 A.H.) aliyezaliwa Palestine mji wa Ghazza, na mwingine ni Imam Ahmad bin Hambal (164-241 A.H.) aliyezaliwa Baghdad na kujulikana sana kwa kitabu chake cha Isnad ya Ibn Hambali kilichokuwa na Hadith zaidi ya 30,000 alizokusanya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Madrasa kiganjani ๐2 kitabu cha Simulizi ๐3 web hosting ๐4 Simulizi za Hadithi Audio ๐5 Dua za Mitume na Manabii ๐6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Dua Sehemu ya 02
Zijuwe nyakati ambazo dua inakubaliwa kwa haraka zaidi. Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hitakubaliwa.
Soma Zaidi...TANZU ZA HADITHI
Tanzu za Hadith(1) Tanzu ya UsahihiKulingana na kiwango cha usahihi wa Hadith, Hadith zimegawanywa katika makundi makuu manne:(a) Sahihiย (b) Hasan/Nzuri.
Soma Zaidi...Dua ya wakati wa kuvaa nguo
Mtume Muhammad (s.a.w) ametufundisha maneno ya kuyasema (Dua) wakati unavaa nguo.
Soma Zaidi...Muombe Allah wakati unapokuwa na furaha.
Amesimulia Abuuhurairah ุฑุถูุงููู ุนูู kuwa mtume ุตููู ุงููู ุนููู ูุณููู amesema "โ ู ููู ุณูุฑูููู ุฃููู ููุณูุชูุฌููุจู ุงูููููู ูููู ุนูููุฏู ุงูุดููุฏูุงุฆูุฏู ููุงููููุฑูุจู ููููููููุซูุฑู ุงูุฏููุนูุงุกู ููู ุงูุฑููุฎูุงุกู โ" โ โmwenye kutaka kujibiwa dua yake wakati akiwa na shida basi azidishe kumuomba Allah wakati wa rahaโ. (amepokea Tirmidh kwa isnad gharib).
Soma Zaidi...