Uandishi wa Hadithi wakati wa Matabiina

Uandishi wa Hadithi wakati wa Matabiina

Historia ya uandishi wa hadithibwakati wa Matabiina, yaani wafuasi wa maswahaba

Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A.H
Hiki ni kipindi cha wafuasi wa Masahaba wa Mtume (s.a.w) katika karne ya pili Hijiriyyah 101-200 A.H. Katika kipindi hiki walitokea wanazuoni wengi waliojizatiti katika kazi ya ukusanyaji wa Hadith kutoka katika vituo mbali mbali vya mafunzo (Centres of Learning). 

Wafuatao ni baadhi ya wanazuoni wa Hadith (Muhaddithina) waliojitokeza kutoka miji mbali mbali. Ma'mar bin Rashi wa Baghdadi; Said bin Abi Ubadah na Rabia bin Sabin wa Basra; Ibn Harith wa Baghdad; Abdul Malik bin Juraiji wa Makka; Walid bin Mubarrak wa Khurasan; Abu Bakr Shyaban wa Kufa na Sufyan bin Uyaina wa Madina.

Japo wanazuoni hawa walijitahidi sana katika hii kazi ya ukusanyaji Hadith, kazi zao bado hazikuwa zenye kutosheleza; isitoshe sehemu kubwa ya vitabu vyao ilihusu ripoti ya vituo vyao. Baada ya kazi hizi, kilitokea kitabu cha "al-Muwatta" cha Imam Malik bin Anas aliyeishi Madina kati ya 95 A.H na 179 A.H. Kazi ya Imam Malik ndiyo ya kwanza iliyowekwa katika mpango mzuri na kuwa kitabu cha kutegemewa na Umma. Imam Malik alifutu mas-ala ya Uislamu kwa kutegemea Qur-an na Hadith tu. Alianzisha umoja wa "Ahli Hadith" ambao kazi yake ilikuwa ni kukusanya Hadith na kuzitekeleza katika matendo.

Katika wakati huo huo alitokea Imam Abu Hanifa al-Numan bin Thabit (80-150) aliyefutu mas-ala mbali mbali ya Kiislamu kwa hoja na Qiyasi (deductions) baada ya kuzingatia Qur-an, Hadith na Ijma'i (makubaliano ya wanavyuoni). Hakuandika kitabu chochote cha Hadith lakini alikuwa mwanazuoni mkubwa wa "Qur-an na Hadith na alikuwa Muj-tahid na Mcha-Mungu.

Katika kipindi hiki hiki palitokea Maimamu wengine wawili mashuhuri. Imam Muhammad bin Idris al-Shafii (150-240 A.H.) aliyezaliwa Palestine mji wa Ghazza, na mwingine ni Imam Ahmad bin Hambal (164-241 A.H.) aliyezaliwa Baghdad na kujulikana sana kwa kitabu chake cha Isnad ya Ibn Hambali kilichokuwa na Hadith zaidi ya 30,000 alizokusanya.

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Views: 2257

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 ai web app     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zinazofanana:

Mzazi na msafiri na mwenye kudhulumiwa dua zao hujibiwa kwa haraka

Wapo watu kadhaa ambao waliomba dua hazirudi. Hapa nitakueleza wawili ambao ni mzazi na msafiri.

Soma Zaidi...
Dua Ambazo Hazirudi: Dua Zenye Kujibiwa kwa Haraka Zaidi

Katika dini ya Kiislamu, kuomba dua ni ibada kubwa na njia ya moja kwa moja ya kuwasiliana na Allah (S.W.T). Hata hivyo, kuna nyakati, mazingira, na hali za watu fulani ambazo Mtume Muhammad (صلى الله عليه وسلم) ametuhakikishia kuwa dua zao hazirudi nyuma na ni zenye kujibiwa kwa haraka sana.

Soma Zaidi...
TANZU ZA HADITHI

Tanzu za Hadith(1) Tanzu ya UsahihiKulingana na kiwango cha usahihi wa Hadith, Hadith zimegawanywa katika makundi makuu manne:(a) Sahihi (b) Hasan/Nzuri.

Soma Zaidi...
DUA 113 - 126

DUA ZA WAKATI WA SHIDA Dua ya wakati wa taabu “LAA ILAAHA ILLA-LLAHUL-’ADHIMUL-HALIIMU.

Soma Zaidi...