UFUPISHO WA ALIFU LELA ULELA KITABU CHA KWANZA


image


Posti hii inakwenda kukisimulia kuhusu hadithi za alifu lela ulela KITABU CHA KWANZA


UFUPISHO WA ALIFU LELA ULELA KITABU CHA KWANZA

Katika nchi za China, Hindi, Uarabuni na Uajemi alikuwepo mfalme aliyefahamika na kuheshimika sana kwa uhodari wake na utawala wake mzuru. Mfalme huyu alikuwa na watoro wawili ambao ni Shahariyar na Shahzaman. Watoto hawa walikuwa mahodari na walifahamika sana. Alipofariki baba yao mtoto mkubwa alitawala kiti cha baba yake kuanzia makao makuu na mdogo wake akaendelea kutawala maeneo ya Samarqand.

 

Baada ya kutengena kwa muda ndugu wawili hawa walipanga kukutana. Makutano yao yalifanikiwa kupangwa na hatimaye wakakutana. Katika wakati kama huu wa kukutana kwa ndugu wawili hawa kulitokea hali za kusalitiwa na wakezao. Shahariyar alikuwa na mkewake aliyempenda sana na hakuamini kuwa inaweza kutokea siku akasalitiwa na mkewe. Baada ya usaliti huu aliamini kuwa hakuna tena mwanamke mkweli duniani kote. Hivyo akaweka nadhiri ya kuoa mke mpya aliye kigori na kumuuwa kila ifikapo asubuhi.

 

Kiapo hiki cha Sultani huyu kilikuwa kweli na alikuwa akifanya hivyo yaani anaowa jioni na asubuhi anauwa. Hali ilikuwa ngumu kiasi kwamba watu wakawa wanawakimbiza mabinti zao mjini. Sifa zote nzuri za Sultani huyu zikaanza kuwa mbaya kwa kitendo chake cha kuuwa watoto wa kike. Kazi yote ya kutafuta mabinti wa kuolewa na mfalme pamoja na kazi ya kutekeleza ahadi ya mfalme kuwauwa mabinti hawa alipewa mmoja katika mawaziri wa Sultani huyu.

 

Sultani huyu alikuwa na mabinti wawili ambao ni Schehrazade na Dinarzade. Mabinti hawa walikuwa ni wazuri sana na walipendana na hata hivyo walipata upendo mkubwa sana kutoka kwa mbaba yao. Schehrazade ambaye ndiye mkubwa alikuwa ni mrembo zaidi na alikuwa na taaluma mbalimbali na alikuwa na elimu za mambo mengi hata ya kisayanzi na masimulizi ya fasihi. Watu wa nchi hii waliamini kuwa uzuri alonao Schehrazade anafaa kuilewa na mfalme au mtoto wa mfalne na si mtu mwingine.

 

Sikumoja katika mazungumzo ya kifamilia kati ya waziri na watoto wake Schehrezade alitowa ombi la kushangaza kwa baba yake na kumwambia kuwa anatakakukomesha tabia ya mfalme ya kuuwa mabinti hivyo anataka siku ifiataya aolewe yeye. Waziri alishangaa na kumuonya mwanae lakini hakusikia. Akajaribu kumtisha na akamsimulia hadithi ya mfugaji na mkewe lakini msmamo wake hauku badilika. Basi harusi ikafanyika na Shehrazadw akapanga mpago na Dinarzade juu ya kutaka kukomesha tabia ya Sultani.

 

Usiku nyumbani kwa mfalme Dinarzade alisikika akimuamsha dadayake Schehrazade ambaye anatarajiwa kuuliwa ifikap asubuhi. Dinarzade alimwambia dada yake apigie hadithi nzuri iwe kama ndio mazungumzo ya kuagana. Schehrazade aluimtaka idhini mfalme na kukubaliwa. Akaanza kumsimulia hadithi ya mfanya biashara na jini. Masimulizi ya hadithi hii yalionekana kumvutia na Sultani pia. Schehrazade kwa ufundi wake wa kusimulia hadithi aliikata hadithi hii na kumwambia Sultani akimuongeza siku zaidi ya kuishi ataimaliza.

 

Sultani alimpa siku zaidi Schehrazade ili amalizie hadithi zake. Utamu uliendelea kumpanda Sultani na kila siku hadithi zilikuwa zinaishia patamu. Hivyo Schehrazade akaendelea kupata muda zaidi wa kuishi. Dada huyu alisimulia hadithi ya mvuvi na jini, hadithi ya chongo watatu na mabinti wa baghadad na nyinginezo hata akafikia kwenye hadithi ya Sinbad. Dada huyu alipomaliza hadithi hii akabakiwa na kuelezea yalotokea kwa mtoto wa Sinbad.

 

Basi siku ilofata baada ya kuisha kwa hadithi ya Sinbad Scheherazade akaanza kusimulia kilichotokea kwa mtoto wa Sinbad alozaliwa na bint ‘Aisha mtoto wa mfalme. Scheherazade akamueleza kuwa atahaya ya msimulia hadithi nzuri zaidi ya ile a mtoto wa Sinbad. Hapo Sulltani akamwambia asimulie hiyo hadithi nzuri zaidi ya mtoto wa Sinbad. Hapo Scheherazade akaanza kusimulia hadithi ifuatayo.



Sponsored Posts


  πŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani       πŸ‘‰    2 Mafunzo ya html kwa kiswahili       πŸ‘‰    3 Mafunzo ya php       πŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       πŸ‘‰    5 Hadiythi za alif lela u lela       πŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image NIMLAUMU NANI (sehemu ya sita)
Post inahusu zaidi hadithi ya NIMLAUMU NANI ambayo ni sehemu ya sita, katika kipengele hiki tunaenda kumwona msichana Amina anapambana na hatimaye anafunga ndoa ya kiserikali na Frank Soma Zaidi...

image NIMLAUMU NANI ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya kijana Frank na Amisa pia na wapenzi wawili ambao ni James na Amina. Soma Zaidi...

image Nani muuaji?
Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu muuaji wa mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

image Hadithi ya binti wa kwanza na mbwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Safari ya nne ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image Hadithi ya mvuvi na jini
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili,ambapo Mama yake na Jackie pamoja na jack wakiwa hospital na jack anaendelea kumwita Julius kila mara. Soma Zaidi...

image Hadithi katika kijiji cha burugo
Β Posti hii inahusu zaidi jinsi ya watu walivyoishi katika kijiji cha burugo .tunajuwa hadithi ni sehemu mojawapo ya kubirudisha na kujifunza kitu flani kutoka kwenye jamii . Soma Zaidi...