image

Ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea

Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

1. Dondakoo ni ugonjwa unaosababishwa na sumu ya bakteria ambaye kwa kitaalamu huitwa corynebacterium diphtheria, bakteria huyu ushambulia sehemu za pua, koo na wakati mwingine maumivu kwenye masikio hali hii upelekea mgonjwa kushindwa kupumua na wakati mwingine kushindwa kumeza, kwa sababu ugonjwa huu usababishwa na bakteria kuna dawa mbalimbali za antibiotics zinaweza kuponya ugonjwa huu, antibiotics hizo ni kama vile penicillin au erythromycin.

 

2. Ugonjwa huu ushambulia hasa watoto na unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwingine kwa njia zifuatazo kama vile  mtu akipiga chagua yale maji maji yakimgusa mtu mwingine hasa kinywani mtu huyo anaweza akapata, kwa hiyo wakati wa kupiga chafya tunapaswa kuwa makini au tunapopiga chafya tunapaswa kupigia kwenye vitambaa ili kuepuka kusambaza ugonjwa kutoka sehemu moja kwenda kwa mwingine, au kama mama au mlezi wa watoto wadogo wanapaswa kuwa makini sana wasije kuambukiza watoto.

 

3. Ugonjwa huu pia unaweza kusambaa kwa njia ya kutumia vitu vyenye bakteria kama vile kunywea maji kwenye kikombe au glass ya mtu mwenye Maambukizi, au kutumia kijiko bila kuosha kutoka kwa mtu mwenye Maambukizi kwa hiyo bakteria usambaa kutoka kwa mwenye Maambukizi kwenda kwa hasiye na Maambukizi, kwa hiyo kila mtu anapaswa kutumia vifaa vyake hasa hasa vile vinavyoongozwa moja kwa moja kinywani au ni vizuri kuosha vyombo kwa maji moto ili kuweza kuua wadudu wanaosambaza na Kuleta madhara.

 

4. Pia hawa wadudu wanaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwingine kwa kutumia vitu kwa pamoja kama vile taulo na nguo zenye jasho kutoka kwa mtu mwenye Maambukizi na vile vile watu wanaokula peni, penseli na vfutio ambavyo vimetumbukizwa kinywani na mtu mwenye maambukizi na ambaye hana Maambukizi naye akija kutumia na kuweka mdomoni anaweza kupata, kwa hiyo kila mtu anapaswa kutumia vifaa vyake hasa kwa watoto ambao wako chekechekea wanapaswa kuangaliwa kwa makini ili kuepuka kuongeza kwa Maambukizi.

 

5. Kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua kuwa ugonjwa huu upo kwenye jamii na usipotibiwa mapema unaweza kuleta madhara makubwa kwa hiyo tunapaswa kuwapeleka watoto  watoto wapewe chanjo mapema ili kuweza kuepuka madhara  mbalimbali ambayo yanaweza kutokea pia jamii inapaswa kujua Dalili zote za ugonjwa huu ili kuweza kuwahi mapema kwenda hospitalini na pia watu wajifunze kujua jinsi ugonjwa huu unavyoenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 839


Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰2 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰3 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Dalili za ugonjwa wa ngiri
Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo mgonjwa wa ngiri anaweza kuzipata, kwa hiyo baada ya kusoma na kuelewa dalili hizi mgonjwa anapaswa kuwahi hospitali mapema kwa ajili ya kupata matibabu. Soma Zaidi...

Dalili za maumivu ya uti wa Mgongo
Posti hii inahusu zaidi dalili za uti wa mgongo ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la uti wa Mgongo. Soma Zaidi...

Ulemavu wa ubongo na mfumo wa fahamu -multiple sclerosis
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dadili na sababu zinazopelekea Ugonjwa wa ulemavu wa ubongo na mfumo wa fahamu ambao kitaalamu hujulikana Kama multiple sclerosis. Soma Zaidi...

Dalili za malaria
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya dalili za maralia Soma Zaidi...

Virusi vinavyopelekea Kuharisha Sana na Kutapika Sana(norovirus)
Maambukizi ya Norovirus yanaweza kusababisha kutapika sana naร‚ย Kuhara. Virusi huambukiza sana na kwa kawaida huenea kupitia chakula au maji ambayo yamechafuliwa na kinyesi wakati wa kutayarisha. Unaweza pia kuambukizwa kwa kuwasiliana kwa karibu na mtu Soma Zaidi...

Fahamu Ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto chini ya miaka mitano
Posti hii inaonyesha mambo mbalimbali yanayoweza kusababisha Ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto chini ya miaka mitano. Soma Zaidi...

Walio katika hatari ya kupata homa ya inni
Posti hii inahusu zaidi watu walio katika hatari ya kupata homa ya ini,kwa sababu ya hali zao mbalimbali wanaweza kupata ugonjwa huu. Soma Zaidi...

Dalili za UTI
Somo hili linakwenda kukuletea dalili za UTI Soma Zaidi...

VIPIMO VYA MINYOO (UTAJUAJE KAMA UNA MINYOO)? fecal test, blood test, colonoscopy tape test X-ray, MRI na CT scan.
VIPIMO VYA MINYOO Haitoshelezi kuwa na dalili pekee ukathibitisha kuwa una minyoo. Soma Zaidi...

Dalili za Ugonjwa wa kula kupindukia
Ugonjwa wa kula kupindukia ni ugonjwa mbaya wa ulaji ambapo mara kwa mara unatumia kiasi kikubwa cha chakula na kuhisi huwezi kuacha kula. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu Ugonjwa wa ukoma
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa ukoma, ni Ugonjwa unaosababishwa na mdudu anayeitwa mycobacterium leprae, mdudu huyu kwa kawaida uathiri sana sehemu za ngozi na sehemu za Neva mbalimbali za mwili Soma Zaidi...

Walio kwenye hatari ya kupata UTI
Posti hii inahusu zaidi watu walio kwenye hatari ya kupata UTI, ni watu ambao wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa UTI kwa sababu ya mazingira mbalimbali kama ifuayavyo. Soma Zaidi...