image

Ugumu wa choo na tiba yake kwa wajawazito

Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa ugumu wa choo na tiba yake kwa wajawazito, ni ugonjwa unaowapata sana akina mama wajawazito na uisha tu pale Mama anapojifungua kwa hiyo tunapaswa kujua wazi sababu za ugumu wa choo na tiba yake kwa wajawazito.

Ugumu wa choo na tiba yake kwa wajawazito.

1. Kwanza  kabisa ugumu wa choo ni hali inayotokea kwa wajawazito ambapo choo ushindwa kutoka nje au kwa wakati mwingine utoka nje kwa kutumia nguvu kubwa hii ni kwa sababu kuna mabadiliko kwenye mfumo wa umengenywaji ambapo usababisha maji kuisha kwenye kinyesi na kusababisha ugumu wa kinyesi na pengine hali huu usababishwa na kubadilika kwa homoni za mimba hasa hasa progesterone homoni.

 

2. Kwa hiyo kwa sababu ya kuwepo kwa tatizo hili la choo kuwa kigumu, Mama wajawazito wanapaswa kunywa maji mengi ili kurainisha chuo na pia wanapaswa kutumia aina mbalimbali za matunda kama vile mapapai, maparachichi, maembe na matunda mengine mbalimbali ambayo ufanya kinyesi kuwa kiraini, pia wanapaswa kutumia mboga mboga za majani kwa wingi, na chakula chenye mlo kamili ili kuweza kupunguza hali huu ya kinyesi kuwa kigumu.

 

3. Kuna njia nyingine ambayo ni  kunywa maji asubuhi kabla haujala chochote na hali hii pia upunguza ugumu wa choo, na pia akina Mama wajawazito wanapopata tatizo kama  hili wanapaswa kuachana na vyakula ambavyo kwa asili yake ufanya kinyesi kuwa kigumu kama vile vyakula vya mtama na vyakula vingine ambavyo vinaweza kuongeza tatizo zaidi.

 

4. Na pia wanawake wajawazito wanapaswa kufanya mazoezi mengi hasa hasa kutembea walau kwa dakika thelathini kila siku ili kuweza kulifanya tumbo kubwa laini na kinyesi kupunguza ugumu wake, na baada ya kufanya mazoezi akina Mama wanapaswa kunywa maji ya kutosha. Na pia wauguzi na wataalam wa afya wanapaswa kuwaeleza wazi wajawazito kubwa huu ni ugonjwa ambao upo na uisha tu baada ya kujifungua.

 

5. Kwa kawaida kuna jamii nyingine ambazo uwa na imani potovu na kufanya vitendo ambavyo ki afya hairuhusiwi kwa Maana mama mjamzito akipatwa na tatizo la ugumu wa kinyesi wanachukua mti wanamkalisha mama na kuanza kuchokonoa kinyesi ili kitoke taratibu hii ni hatari kwa sababu wanaweza kuharibu na sehemu mbalimbali kwa sababu ya kuchokonoa na mti kwa hiyo elimu inapaswa kutolewa kwa jamii nzima ili kuepuka udhalilishaji wa kijinsia na kusababisha uharibifu kwa akina Mama.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1541


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kupima ujauzito kwa kutumia chumvi, sukari na sabuni
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupima mimba kwa kutumia chumvi sukari na sabuni Soma Zaidi...

Njia za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha.
Posti inahusu zaidi njia maalum za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha,Ni njia za uzazi ambazo wanaonyesha wanatumia kwa sababu kuna njia nyingine zikitumiwa na wanaonyonyesha zinaweza kuleta matatizo kwa watoto au kusababisha maziwa kutokuwa na vitamini v Soma Zaidi...

Je mwanamke anaweza kujijuwa ni mjamzito baada ya muda gani.
Mdau anauliza ni muda gani mwanamke anaweza kujijuwa kuwa amepata ujauzito. Soma Zaidi...

Mabadiliko ya Matiti kwa Mama mjamzito
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye Matiti kwa Mama mjamzito, hali hii utokea pale ambapo mama akibeba mimba Kuna mabadiliko kwenye Matiti kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Namna ya kuangalia kama mtoto aliyezaliwa anapumua
Posti hii inahusu zaidi mbinu za kuangalia kama mtoto anapumua pindi anapozaliwa,tunajua kabisa ili kujua na kuelewa kama mtoto yuko hai ni lazima kuangalia upumuaji wa mtoto,ambapo tunaitambua pale anapolia tu. Soma Zaidi...

Fahamu mtoto aliyetanguliza matako wakati wa kuzaliwa
Posti hii inahusu zaidi mtoto aliyetanguliza matako wakati wa kuzaliwa, kwa kawaida tunajua kwamba mtoto wakati wa kuzaliwa ni lazima atangulize kichwa ila Kuna kipindi mtoto anatanguliza matako, kuna aina nne za mtoto kutanguliza matako. Soma Zaidi...

Huduma za msingi kwa mama mjamzito na mtoto.
Posti hii inahusu zaidi huduma muhimu anazopaswa kupewa mama mjamzito wakati akiwa na mimba, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua yaani ndani ya masaa ishirini na manne, tunajua wazi kuwa Mama akiwa mjamzito anaweza kupata matatizo mbalimbali kwa h Soma Zaidi...

Nikila tumbo linauma, mdomo mchungu, matiti yanauma na hedhi sijapata, je ni dalili za mimba?
Mdomo kuwa mchungu ni halia mabayo haiashirii ishara mbaya za kiafya. Mdomo unaweza kuwa mchungu kutokana na vyakula. Pia hutokea ikawa ni ishara ya baadhi ya maradhi, ama ni matokeo ya baadhi ya shda za kiafya. Je vipi kuhusu maumivu ya matiti na tumb? Soma Zaidi...

Vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba
Posti hii inahusu zaidi vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba,ni vipimo vya moja kwa moja kutoka maabara na vingine sio vya maabara. Soma Zaidi...

Faida na hasara za kutumia uzazi wa mpango
Tunaposema uzazi wa mpango, tunamaanisha ile hali ya kuachanisha muda kutoka mtoto hadi mwingine. Inatakiwa angalau mtoto na mtoto wapishane miaka miwili. Uzazi wa mpango ni maamuzi kati ya mama na baba. Soma Zaidi...

Dalili za tezi dume na sababu za kutokea kwa tezi dume.
dalili za ugonjwa wa tezi dume, na sababu za kutokea kwa tezi dume, maana ya tezi dume na athari zake Soma Zaidi...

Ni ipi hasa siku ambayo nitafute ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kutafuta ujauzito Soma Zaidi...