Ujio wa wageni wa baraka

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

UJIO WA WAGENI WA BARAKA.

Kama nilivyokueleza kuwa mama alikuwa ni mchamungu na mpendwa na watu. Alikuwa akisaidia anaowajuwa na asiowajuwa, wageni na wenyeji. Basi sikumoja walikuwa wageni wakitokea nchi ya Uhabeshi huko Yemeni. Wageni wale walikuja Misri na kukutana na baba. Hakuwa akiwafahamu wala hawakuwa wakimjuwa. Walipokuja walianza kutafuta nyumba za wageni lakini hawakufanikiwa kupata vyumba. Jumla walikuwa ni watu watatu. Vijana wawili wenye maumbo ya kawaida na mzee mmoja wa makamo, aliyekuwa na ndevu nyeupe zilizolala vyema.

 

Umri wa vijana hawa naweza kuufananisha kati ya miaka 20 hadi 25. hawakuwa wenye ndevu nyingi ndio sasa masharubu yalikuwa yakionekana kama kipara ninachoota ywele. Wageni walipokutana na baba baada ya kuelekezwa na watu wakaomba hifadha. Walitaka kufadhiliwa kwa muda wa masiku 7 tu. Walikuja kutafuta mali ili wakauze nchini kwao. Basi baba akawaruhusu kwa sharti kuwa hawatasababisha uharibifu wowote ndani ya mji wala katika mali za wananchi zilizopo mjini ama mashambani.

 

Baada ya makubaliano baba aliwapa karatasi wasaidi na iwe ni kumbukumbu. Pia wageni wakaongeza kuwa sisi tutakuwa tukiwinda na kuvua. Kwa kila tutakachokipata wewe tutakupatia kichwa. Sharti hili lilionekana la utata sana lakini baba alikubwali. Maana ya sharti hili ni kuwa wakivua samaki baba atapewa vichwa vya samaki, na wakiwinda mnyama baba atapewa kichwa. Baba aliweka saini na akaichukuwa karatasi na kuipeleka kwa kadhi wa mji naye akaweka saidi na kuihifadhi.

 

Wageni waliweza kulala nyumbani kwa siku tatu bila hata ya kufanya kazi yeyote na hata kutoka nje. Tulipokuwa tukiwapelekea chakula walisema wanachochakula chao na wakatuonyesha nyama kavu iliyokaushwa. Tulipowapelekea maji ya kunywa wakasema wanamaji yao na wakatuonyesha viriba vya ngozi, wakidai ndimo wamehifadhi maji yao. Watu wa mtaani hawakuweza kuwajuwa wageni wetu japo walisikia kuwa baba amepokea wageni.

 

Wasichana wa mtaani walikuwa wakija myumbani wakidai kuomba chumvi mara sukari mara moto ilimradi waone sura za wageni wetu, ila bila ya mafanikio hawakupata chochote. Siku ya nne baada ya alfajiri kuisha wageni walimfata baba ni kumuomba akawaonyeshe sehemu mto ulipo. Wakamwambia awaelekeze kwenye matope ambapo samaki aina ya kambale wanapatikana.

 

Baba akawaelekeza sehemu karibia na maporomoko ya maji yalipo ambapo kuna dimbi mbele lina matope mengi na maji machache sana. Hapo kuna kambale wengi wanaojificha kwenye matope. Wale mabwana wakachukuwa kipande cha shuka waliopewa wajifunike kisha wakashika wawili kila mmoja kashika upande mmoja. Kisha yule mzee akaingia kati na kuanza kushakia samaki waende kwenye ile chuka.

 

Kitu cha ajabu walipokuwa wakivua samaki tofauti na kambale walikuwa wakimwacha. Na wanapovua kambale mdogo walikuwa wakimwacha na wakisema “Mwenyezi Mung ampe umri mrefu samaki huyu”. hapa nikagundua kuwa hawa ni wachamungu sana. Lakini hikujua sababu ya yale waliokuwa wakiyafanya. Basi walipotimiza idadi ya kambale 11 wakaondoka. Kisha wakasema “Asiyeshukuru kidogo hata akipewa kingi hawezi kushukuru”.

 

Walikusanyika sehemu moja na kunza kuosha samaki wake kisha mkubwa wao akasema “wala hatabeba mtu kubeba mzigo wa mwengine” baba akiwa akiwaangalia vyema yule mdogo kuliko wote akachukuwa kishu na kuanza kukata vichwa vya samaki wale. Akisha anayefata kwa ukubwa akaanza kupasua matumbo ya samaki wale na kuyaweka kwenye mfuko. Kika akarudia kauli ile “ asiyeshukuru kwa kidogo hata kwa kingi hatashukuru kisha akanikabidhi mfuko wa vichwa vya samaki”. Wakamueleza kuwa vichwa vyote kula ila hiki kihifadhi mpaka siku ya miadi yetu” waamuonyesha kichwa hicho na kunieleza “hakupata hasara mwenye kusubiri n akufata maelekezo”

 

Alistaajabishwa sana na watu hawa. Hawakuwa watu wa maneno mengi wala kupiga stori. Vitendo vyao vilikuwa ndio maneno yao. Na walizungumza maneno machache ambayo ni mistari kutoka kwenye vitabu vya dini Alivyowahi kusomaga. Akafata maelekezo na kuondoka na wageni wake. Alipofika nyumbani akamkabidhi mama vichwa vile na akamueleza apike supu. Kisha kichwa kile akaenda kukihifadhi sehemu salama.

 

 

Asubuhi ya siku ya pili wageni hawakwenda kuvua ila mmoja kati yao akatoka na kuchukuwa ule utumbo wa kambale akaenda kwenye uwanja wa michezo. Wakati hue wenzake wawili wakaanza kukausha samaki wale uwani nyumbni kwetu. Walikuwa na jiko lao na mafuta yao ya kuwashia moto. Hawakuhitaji kitu chochote. Kama kawaida hawakuwa na maneno mengi na maneno yao machache yalikuwa ni mistari kutoka vitabuni. Nikaelekea uwanjani nikaone anachofanya yule mwenzao mwengine.

 

Alikaa katikati ya uwanja na kuanza kupiga winja wa ajabu sana. Katu sijapatapo kusikia winja kama huo. Sikujuwa hasa ni ni anakusudia. Haukupita muda wakaja kunguru na ndege wengine wa porini pamoja na mabata maji. Alianza kutoa utumbo wa samaki waliovua jana na kuanza kuwapa wale ndege. Nikiwa naangalia kwa ukaribu nini kinaendelea, nikashhudia anatoa kisu chake. Wale ndege walikuwa Ini kama wake waliweza kumsogelea sana. Alizungumza maneono kadhaa sikupata kuyasikia maana nilikuwa mbali.

 

Basi akamkamata kunguru mmoja na kumchinja kisha akakamata baa maji na kulichinja. Kisha akamaliza utumbo alio nao na kurudi nyumbani. Alimpatia baba kichwa cha kunguru na kumueleza akihifadhi mpaka siku na miadi na kile cha bata maji akamueleza akitumie kwa chakula. Sikuweza kujuwa kabisa maana ya haya mambo waliokuwa wakiyafanya. Wana siku tano sasa. Wamebakiwa na siku mbili. Walisema kuwa siku ya saba ndiyo wataondoka mapema asubuhi hivyo wamebakiwa na siku moja tu.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-07     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1093


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

NIMLAUMU NANI (sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi kijana Frank anayelazimishwa kuolewa na Amisa yeye hayuko tayari ila kwa sababu ya maisha kuwa magumu anaamua kulala na Amina na kumbebesha Mimba ya watoto mapacha. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sita
Post hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sehemu ya sita.sehemu hii inaonyesha jinsi bibi alivyo ndumila kuwili na hapendi kuonekana mbaya. Soma Zaidi...

Hadithi ya waziri aliyeadhibiwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Chemsha bongo na bongoclass
Jipime uwezo wako wa kufikiri pamoja nasi. Soma Zaidi...

Alif lela ulela
Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

SAFARI YA MUUJIZA ( SEHEMU YA PILI)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi ya safari yenye muujiza ,ni pale mtoto ya Mungu mengi anafika kwenye kituo Cha ntonga na kuona yake mazingira na kufahamu njia ya kwenda kule. Soma Zaidi...

NIMLAUMU NANI ( sehemu ya tano)
Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya Nimlaumu nani ambapo juma anapanga na madaktari wanaopima DNA ili kuweza kutambua kwamba mtu mimba ni ya kwake na sio ya Frank kwa hiyo tuendelee kusikiliza mpaka tutakapoona mimba itakuwa ya Frank au juma. Soma Zaidi...

Hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu Soma Zaidi...

Kila kitu ambacho wanaume wanatakiwa kufahamu kuhusu wanawake.
Hii ni siri kubwa kuhusu wanawake. Hapa utajifunza jinsi ya kumfanya mwanamke asikuache. Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa pili wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Kutokana kwenye kisima mpaka kuwa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Kujiandaa kwa ajili ya kumuona daktari
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya mambo ya kujiandaa kwa ajili ya kumuona daktari Soma Zaidi...