Ujue ugonjwa wa tauni
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa tauni ambao kwa kitaalamu huitwa plague ni Ugonjwa unaosababishwa na wadudu ambao huitwa kitaalamu huitwa yersinia pestis ambao ukaa ndani ya panya.
Ujue ugonjwa wa tauni.
1.Kwanza kabisa tunapaswa kufahamu kuwa ugonjwa wa tauni ni Ugonjwa unaosababishwa na wadudu wanaoitwa kwa kitaalamu yersinia pestis wadudu hawa uishi ndani ya panya na viroboto ambao ufyonza damu kwenye panya ufyonza pamoja na wadudu hawa, na pia viroboto uweza kung'ata binadamu na kuingiza wadudu wanaoitwa yersinia pestis ambao usababisha ugonjwa wa tauni ambao uwatesa watu wengi na kusababisha madhara mbalimbali kwenye jamii.
2. Ugonjwa huu umeenea katika sehemu mbalimbali za Afrika, Asia, na Amerika inavyokadiriwa ni kuwa kuanzia mwaka elfu moja mia tisa tisini na nne mpaka elfu mbili na tatu watu elf mbili mia nane na hamsini wameripotiwa na shirika la WHO, asilimia tisini waliokuwa wameugua ugonjwa huu ni waafrika ukilinganisha na mataifa mengine ,kwa hiyo na Tanzania mpaka sasa kuna sehemu ambapo ugonjwa bado upo na unaowasumbua watu sehemu ambazo zinapatwa na Ugonjwa huu ni sehemu zenye unyevunyevu kwa wingi ukilinganisha na sehemu nyingine.
3. Ugonjwa huu kwa ujumla unaweza kutibiwa na kupotea kabisa kwenye jamii kwa sababu watu wanapaswa kuzingatia usafi ili kuepuka kuwepo kwa panya ambao wanatunza hawa wadudu na pia kwenye kipindi cha mavuno watu wanapaswa kuwa makini ili kuweza kuepuka kuongezeka kwa panya ambao ndio chanzo cha Ugonjwa huu,kwa wakati mwingine dalili za Ugonjwa huu uchanganya watu na kuwa kama Dalili za kawaida kama vile homa na mwili kuishiwa nguvu ila zinabadilika kadri ugonjwa inavyoongezeka.
4.Dalili nyingine ambazo zinaweza kujitokeza ni kama vile miwasho kwenye mwili, maumivu ya kichwa ambayo yanaweza kuanza taratibu na ukitumia dawa yanaisha na baadae yanaanza tena maumivu kwenye mwili, kichefuchefu na kutapika, kuwepo kwa vipele kwenye kwapa, na Dalli hizi utofautiana na kuongezeka kadri siku na mda unavyoenda.
5.Kwa hiyo jamii nzima inapaswa kuelimishwa kuhusu Ugonjwa huu na kujua Dalili zake kwa sababu wakati mwingine Dalili hizi ufanana na magonjwa mengine ya kawaida kwa hiyo ni lazima kuzijua kwa uhakika ili kuweza kupata huduma sahihi na kuepukana na madhara mengine makubwa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Dalili kuu za Malaria mwilini
Malaria husababishwa na vijidudu vidogo parasite wanaojulikana kama plasmodium. Vijidudu hivi hubebwa na mbu aina ya anophelesi. Kuna ina nyingi za plasmodium lakini aina 5 tu ndizo husababisha malaria
Soma Zaidi...Dalili za saratani ya ini
Posti hii inahusu zaidi dalili za saratani ya ini, ni baadhi ya Dalili ambazo zinaweza kujitokeza na kuona kwamba mtu fulani ana saratani ya ini.
Soma Zaidi...DALILI ZA MIMBA BAADA YA TENDO LA NDOA
Je unahitaji kujuwa kama umepata ujauzito baada ya kufanya tendo la ndoa? hakika sio rahisi ila kama utakuwa makini utaweza.
Soma Zaidi...HPV (Human Papillomavirus): Chanjo na saratani ya shingo ya kizazi.
​Virusi vya Human Papillomavirus (HPV) ni kundi la virusi vinavyoambukiza ngozi na utando wa ndani wa mwili. Ingawa maambukizi mengi ya HPV hupona yenyewe, aina fulani za virusi hivi zinaweza kusababisha mabadiliko ya seli yanayoendelea na kuwa saratani, hasa saratani ya shingo ya kizazi. Makala hii inachambua uhusiano kati ya HPV na saratani, umuhimu wa chanjo, na hatua za kinga ambazo kila jamii inapaswa kuzichukua.
Soma Zaidi...