Umuhimu wa kupima virus vya ukimwi kwa wajawazito na wanaonyonyesha
Post hii inahusu umuhimu wa kupima virus vya ukimwi kwa mama wajawazito na wanaonyonyesha. Ni hatua ya kupima Mama akiwa mjamzito na wakati wa kunyonyesha ili kuepuka hatari ya kumwambikiza mtoto
Umuhimu wa kupima virus vya ukimwi kwa mama mjamzito na wakati anaponyonyesha.
1. Tunajua wazi Mama akiwa mjamzito pale anapogundua kubwa ana mimba tu anapaswa kuja kliniki kupima maambukizi pamoja na mme wake, pengine Mama anaweza kuja kupima kwa Mara ya kwanza hasikutwe na virusi na akija kupimwa mara ya pili kabla ya kujifungua hasikutwe navyo lakini anaweza kuwa navyo kwa sababu ya kuwepo kwa hali mbalimbali vinaweza visionekane kwa hiyo anapaswa kupima tena akiwa ananyonyesha kwa sababu anaweza kupata ndani ya mda huo lengo ni kumzuia mtoto hasipatwe na Maambukizi.
2. Kwa kufanya vipimo vya marudio kwa mara tatu na wengine wanapima zaidi wakati wa ujauzito na kunyonyesha huweza kutambua hali ya Wazazi kwa ujumla na ikiwa Maambukizi yakiwepo ni rahisi kuanza Dawa mapema ili kuweza kufuvaza makali ya virusi vya Ukimwi kwa ajili kuimarisha afya ya mzazi na kumkinga mtoto dhidi ya Maambukizi, lakini Mama hasipoanza dawa mapema anaweza kumwambikiza mtoto na mtoto akazaliwa na Maambukizi.
3.Pia kwa kutumia dawa hizi umsaidie kuzuia magonjwa nyemelezi kwa Mama na mtoto pia kama vile ugonjwa wa kifua kikuu, Malaria, Magonjwa ya ngozi kupungukiwa na kinga ambapo upelekea Mama kubwa na mkanda wa jeshi na magonjwa mengine mengi uweza kutokea kwa sababu ya kuwepo kwa kinga ndogo ya mwili kwa hiyo Mama kama hajapima ugonjwa wa VVU na kuona magonjwa Mengi anapaswa kwenda kupima ili kujua afya yake na mtoto wake.
4. Kwa upande wa mtoto pale ikitokea Mama amejifungua mtoto huku mama ana Maambukizi mtoto anapaswa kuchukuliwa vipimo kama ifuatavyo, mtoto apimwe pale anapozaliwa, mtoto akiwa na umri wa miezi sita, pia akiwa na umri wa miezi tisa, miezi mitatu baada ya kuacha kunyonya na baada ya miezi kumi na minane, kutokana na vipimo vyote hivyo kama Mtoto hajagundulika na Maambukizi tunaweza kusema kuwa mtoto ni salama.
5. Kwa hiyo elimu inapaswa kutolewa kwa jamii nzima ili kujua umuhimu wa kupima maambukizi ya HIV ili kuepuka kuambukiza watoto hambao hawana hatia na wakati wa kwenda kliniki kwa Mara ya kwanza wazazi wanapaswa kwenda wote kupima maambukizi ili kuepuka kumwambukiza mtoto.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Mambo yanayoathiri Uponyaji was jeraha.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo yanayoweza kuadhiri Uponyaji wa jeraha.jeraha huleta maumivu makali sana, vilevile Uvimbe, kutoa usaha. Pia jeraha hutofautiana katika kupona kwa mtu mzima na Mtoto.
Soma Zaidi...Umuhimu wa uterusi
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa uterusi, ni mfuko unayosaidia kumtunza mtoto akiwa tumboni mwa mama yake.
Soma Zaidi...Nna swali mimi nimefanya Romance na mtu ambaye sijampima kbsa sasa naogopa anaeza kuwa mgonjwa na mm nkaupata
Muulizaji anauliza he kula denda, ama kumbusu ama kufanya romance na muathirika was HIV na wewe uta ambukizwa?
Soma Zaidi...Madhara ya ulevi
Poshi hii inahusu madhara ya ulevi.Utegemezi wa pombe kwa kawaida humaanisha kuwa mtu anatumia kiasi kikubwa cha pombe na kuna masuala kuhusu kupoteza udhibiti.
Soma Zaidi...