UMUHIMU WA KUTUMIA DAWA ZA ARV


image


Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia dawa za ARV kwa wathirika wa virusi vya ukimwi .pia tutangalia kwa undani mambo ya kuzingatia kwa wathirika wanaotumia ARV .pamoja na kujali watu wanaotumia dawa hizo .


 Umuhimu wa kutumia dawa za " ARV" kwa wathirika wa VVU.

  1. Kutokana tulivyoeleza apo juu kuhusu umuhimu au matumizi kwa watu wanaotumia dawa za "ARV" .ambazo ni dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi .dawa hizi utakuwa kutumia kwa usahihi.mtu anayeishi na virusi vya ukimwi hutumia dawa hizi kwa maisha yake yote.Endapo mwathrika ataacha kutumia dawa hizo ,anaweza kupata madhara zaidi kama vile kufhoofu kiafya ,magonjwa nyemelezi na kifo  ARV haziui virusi bali hufubaza virusi na kupunguza kasi ya kuongezeka.dawa hizi ufanya kinga ya mwili kuimarika.jukumu la kumwanzishia mwathrika dawa za kupunguza makali ya VVU ni  la kitabibu mkwa hiyo,kuna umuhimu wa kupinda afya ili kukua hali halisi ya afya zetu.     
  2. Huwaondolea wathirika wa VVU mateso ya kushambuliwa na maradhi nyemelezi ..maradhi   nyemelezi ni kama .saratani ,kifua kikuu,fangasi,kuharisha na homa kali ya mapafu
  3. Huimarisha afya za wanaoishi na VVU.   Kutokana na ilo watu wenye virusi vya ukimwi afya zao huwa vizuri kama vile watu wasio na ugonjwa wa UKIMWI. Hivyo hivyo mtu anaetumia hizi dawa inabidi awe anafanya sana mazoezi ya mwili .ili kuweza kulinda seli zake ziweze kufanya kazi.
  4. Wathirika wa VVU wanaweza kuishi maisha ya kawaida na kushiriki shughuli zao za kiuchumi na kukiongizia kipato.kutokana na hilo watu wanaotumia hizi dawa wanauwezo wa kuongoza maisha yao ya kila siku 

        5. Hupunguza kasi ya kuzaliana kwa wingi kwa VVU.hata hivyo hurefusha maisha.

      .  Mambo ya kuzingatia kwa waathrika wanaotumia "ARV"

Kama tulivyoona apo mwanzo wathirika wa VVU ni kundi linaloitaji kuishi kwa kufuata taratibu zilizoainishwa na watahalamu wa afya.mambo ya kuzingatia ni kama yafuatayo.

1.waathirika ni lazima wafuate ushauri wa kitaalamu wa kitibabu au watahalamu wa afya.

2.waathrika wanapaswa kutumia ARV kwa dozi sahii na kwa muda sahii .dawa zitumike kama ilivyoelezwa na daktari au mtaalamu wa afya .hii itasaidia kuboresha afya na kupunguza uwezekano wa VVU kuwa sugu kwa dawa zinazotumika.

3.waathrika wachukue tahadhari kwa kujikinga ili wasipate maambukizi mapya na kuambukiza wengine.ili kuondoa idadi ya maambukizi katika jamii.

4.mwathirika asiache kutumia dawa kwa muda na kisha kurudia tena  dawa hizo bila ushauri wa daktari au mtaalamu wa afya.

5.waathirika wa VVU watoe taarifa kwa daktari au watoe huduma kuhusu matatizo na athari za "ARV" endapo zitajitokeza.

6.waathirika waepuke kufuata imani na mila potofu za jadi au za dini zinazozuia kuwa mfuasi mzuri wa ARV 

7.waathirika wafuate ratiba ya kwenda kiliniki ya dawa za "ARV" bila kukosa ili kupata ushauri nasaa.

8.waathrika wazingatie ushauri kanuni za afya kwa mfano ,kuzingatia usafi wa mwili,lishe bora na mazingira safi.

9.waathirika wanashauriwa kuendelea kuishi kwa matumaini na wasikate tamaa .

10.mtumiaji wa "ARV" harusiwi kishirikiana dawa zake na mtu mwingine.

      jinsi watu wanaotumia dawa za "ARV"

1. Wathirika wa VVU wanaotumia ARV wanahitaji kuthaminiwa katika jamii zao na kuwaona kama watu wengine bila kuwabuguzi na kuwatenga.ili kuwajali watu wanaotumia dawa hizo.ni muhimu sana kuwasaidia pale wanapoitaji msaada.

2.pia kuambatana nao wanapoitaji kuaindikizwa kwenda kiliniki kuchukua dawa zao.pia inabidi tuwafaliji  wajione na wenyewe kama watu wengine wanapoitaji huduma hizo.

3.tuwasaidie wanapoitaji kuelekezwa matumizi sahihi ya  " ARV" ili wasiweze kwenda kinyume badae wasije kupata athari zozote katika jamii zetu.

4.kuwapatia chakula bora na kwa wakati.pia inabidi tuwandalie chakula chenye kuwaongezea vitamin ndani ya mwili wao.ili waweze kuijenga miili ya sawa .chakula lazima kiwekwe kwenye mazingira masafi na yenye virutubisho.kifunikwe na kisiwe cha balidi sana.

5.kuwakumbusha muda sahihi wa kumeza dawa pale wanaposahau.

6.kuwahamasisha kuendelea na matumizi ya dawa.

7.kuepuka kuwanyanyapaa walioathirika na VVU.pia ni muhimu sana kuzingatia na kufuata ushauri unaotolewa na daktari au mtaalamu wa afya kwa ktumiaji hi wa ARV .

 

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    5 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    6 Maktaba ya vitabu    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Je unazijuwa dalili za Ukimwi na HIV?
Huwenda ukawa ni moja kati ya watu wanaotaka kujuwa juu ya dalili za ukimwi. Kama wewe ni katika watu hawa tambuwa kuwa kuna dalili za VVU (hiv) na dalili za ukimwi. Makala hii itakwenda kukuletea dalili kuu za mwanzo za VVU na HIV kuanzia wiki tatu za mwanzo hadi kufikia miezi mitatu. Mwisho wa makala hii utaweza kujifunza mambo yafuatayo:- Soma Zaidi...

image NI WATU GANI WALIO HATARINI ZAIDI KUPATA UKIMWI?
Post hii itakwena kukufundisha kuhusu historia fupi ya Ukimwi na matibabu yake. Ni wapi wapo hatarini kupata maambukizi na ni kitu gani wafanye? Soma Zaidi...

image Sababu za kuwepo kwa saratani ya inni.
Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali za kuwepo kwa saratani ya ini, saratani hii imekuwa tishio kwa wengi ila ni vizuri kujua baadhi ya sababu ambazo uchangia sana kuwepo kwa tatizo hili la saratani ya inni. Soma Zaidi...

image Hatua za kupambana na ugonjwa wa UTI
Posti hii inahusu zaidi hatua au mbinu za kupambana na ugonjwa wa UTI kwa sababu ugonjwa huu umekuwa tishio kubwa kwa sasa kwa hiyo tunapaswa kutumia njia mbalimbali ili kuweza kupambana na Ugonjwa huu. Soma Zaidi...

image Madhara ya maumivu kwenye nyonga na kiuno.
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa matibabu kwenye nyonga na kiuno hayatafanyika. Soma Zaidi...

image Umuhimu wa kutumia dawa za ARV
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia dawa za ARV kwa wathirika wa virusi vya ukimwi .pia tutangalia kwa undani mambo ya kuzingatia kwa wathirika wanaotumia ARV .pamoja na kujali watu wanaotumia dawa hizo . Soma Zaidi...

image Dalili za za kuwepo kwa maambukizi chini ya kitovu
Posti hii inahusu zaidi dalili za kuonyesha kuwa Kuna maambukizi kwenye kitovu hasa hasa chini ya kitovu. Soma Zaidi...

image Vinywaji vyakula salama kwa mwenye Presha ya kupanda
Je umesha wahi kujiuliza kuwa ni vinywaji vipi mwenye presha ya kupanda anafaha kutumia, Unadhani ni maji, mvinyo wa pombe, chai na kahawa. Bila shaka ungependa kujuwa zaidi kuhusu jambo hili. Makala hii ni kwa ajili yako Soma Zaidi...

image Chini ya Tumbo langu Kuna uchungu lakini si sana shinda ni ni?
Nini kinasababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu? Soma Zaidi...

image Zijue sababu za moyo kutanuka.
Posti hii inahusu zaidi sababu za moyo kutanuka, Kuna kipindi ambapo moyo utoka kwenye hali yake ya kawaida na kutanuka hali ambayo usababisha madhara kwa mwenye tatizo hilo, ila Kuna sababu ambazo usababisha moyo kutanuka kama tutakavyoona. Soma Zaidi...