image

Umuhimu wa kuvaa nguo za upasuaji.

Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa nguo za upasuaji, tunajua wazi kuwa, wakati wa upasuaji tunapaswa kusafisha chumba na mazingira yake lengo ni kuhakikisha kuwa tunazuia wadudu wasisambae au kuingia kwenye mwili wa binadamu.

Umuhimu wa nguo za upasuaji.

1.Nguo za upasuaji zinaweka umbali kati ya mgonjwa na mhudumu ili kuepuka kusambaa kwa Magonjwa kutoka kwa mhudumu kwenda kwa mgonjwa na kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu kwa kufanya hivyo utaratibu na nidhamu ya upasuaji uende vizuri likiwa na lengo kuu ambalo ni kuzuia kusambaa kwa Magonjwa wakati wa upasuaji, kwa hiyo wahudumu wa afya wanapaswa kushika sheria za kuvaa nguo hizi. Ambao hawafanyi hivyo wanapaswa kuchukuliwa hatua.

 

2. Vile vile nguo za upasuaji usaidia kuzuia damu na majimaji ambayo yanaweza kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu, ikitokea kwa bahati mbaya maji yakaruka kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu spidi ya kwanza yatafikia kwenye apron na hayataweza kumfikia mhudumu, kwa hiyo wahudumu wa upasuaji wanapaswa kujikinga na magonjwa kwa kuvaa nguo za upasuaji kwa kufuata mtiririko wote kwa sababu wakati wa upasuaji chochote kinaweza kutokea.

 

3.Pia nguo za upasuaji usaidia kuzuia magonjwa na chemikali nyingine kusambaa kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu kwa mfano kama mgonjwa ana Maambukizi ya ukimwi, na homa ya ini katika kufanya upasuaji ukiwa na nguo za upasuaji unaweza kuepuka na magonjwa haya, kwa hiyo wahudumu wawe makini sana katika kutumia nguo za upasuaji ili kuepukana na magonjwa na kemikali nyingine zinazotumika wakati wa upasuaji.

 

4. Kwa hiyo baada ya kujua faida za nguo za upasuaji kila kituo cha afya wanapaswa kuwa na nguo zote za kufaa na zinapaswa kusafishwa kwa wakati na kwa utaratibu maalum na pia wanaoziandaa wanapaswa kuwa waangalifu na kuwa na ujuzi katika kazi hiyo, pia na wahudumu wanaozivaa wanapaswa kuwa na moyo wa kujali wa kutumia nguo hizo kwa wakati wake na kwa usahihi kwa sababu wasipozitumia wanaweza kuhatarisha maisha yao na wagonjwa pia.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1193


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Nini maana ya Afya
Maana ya afya ni pana sana tofauti na vile ambavyo sisi tunajuwa. Afya inahusisha mambo mengi sana. Soma Zaidi...

MAZINGIRA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

AFYA YA UZAZI (UJAUZITO, KULEA WATOTO, AFYA YA MIMBA NA MTOTO, MAGONJWA YA KINAMAMA NA WANAUME)
Soma Zaidi...

Maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

Nini hutokea unapokuwa kwenye ndoto ukiwa usingizini umelala
Ndoto ni moja ya mamba ambayo yanatokea mwanadamu na sayansi haina uelewa hasa nini hutokea. Hata hivyo yapo machache tafiti za kisayansi zinatueleza. Soma Zaidi...

dondoo 100 za Afya
Basi tambua haya;- 21. Soma Zaidi...

VIJUE VIDONDA VYA TUMBO, SABABU ZAKE NA DALILI ZAKE
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

AFYA YA UZAZI NI NINI?, PIA UTAJIFUNZA MATATIZO YA HEDHI, KUTOKUPATA UJAUZITO, ULEZI WA MIMBA NA MTOTO, TEZI DUME NA NGIRI MAJI, NGUVU ZA KIUME
AFYA YA UZAZI Afya ya uzazi huweza kufungamana na mambo mengi sana. Soma Zaidi...

KITABU CHA MATUNDA
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

Kitabu Cha Afya
Soma Zaidi...

Kujiandaa kwa ajili ya kumuona daktari
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya mambo ya kujiandaa kwa ajili ya kumuona daktari Soma Zaidi...