UMUHIMU WA UCHUMI KATIKA UISLAMU


image


Post hii itakufundisha faida na umuhimu wa kijenga uchumi katika jamii ya kiislamu.


2. Umuhimu wa uchumi katika Uislamu
Mwanaadamu ameumbwa na mahitajio mengi ambayo hana budi kuyapata ili aweze kuishi kwa furaha na amani hapa ulimwenguni. Kwa kuwa mwanaadamu ni mchanganyiko wa mwili na roho, pia mahitajio yake yamegawanyika, ana mahitajio ya kiroho na kimwili. Mahitajio ya kiroho ambayo humuwezesha mwanaadamu kuishi maisha ya utulivu yenye furaha na amani, hupatikana kwa kufuata kwa utii na unyenyekevu mwongozo wa Allah (s.w).

 


Mahitajio ya kimwili kama vile chakula, mavazi, vipando na njia ya uchumi hupatikana kwa kuchapakazi chini ya mazingira yatokanayo na itikadi sahihi yenye kusimamiwa na viongozi wanaozingatia haki itokayo kwa Muumba. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Allah (s.w) amejaalia mali anayoichuma mwanaadamu iwe ndiyo inayoboresha maisha yake: “Wala msiw ape w apumbavu mali zenu ambazo Mw enyezi Mungu amezijaalia kwa ajili ya maisha yenu …” (4:5)

 

Kutokana na aya hii, kuchuma mali si jambo la hiari kwa mwanaadamu kwani kwa namna Allah (s.w) alivyokadiria, maisha ya mwanaadamu kwa hapa ulimwenguni hayawezekani pasi na kuchuma. Ni kweli kwamba vitu vyote vilivyomzunguka mwanaadamu katika ulimwengu huu vimeumbwa kwa ajili yake kwa ushahidi wa Qur-an: “Yeye ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi…” (2:29).

 


Lakini mara nyingi vitu hivi haviko katika hali ya kutumiwa na mwanaadamu moja kwa moja. Bali mwanaadamu analazimika kutumia elimu yake, Maarifa yake, juhudi zake na vipawa vyake vingine ili ayabadilishe mazingira yake yaweze kumtumikia na kukidhi haja zake.
Kwa mtazamo huu Uislamu unatuamrisha kuchuma kama unavyotuamrisha kusimamisha Swala, kutoa Zakat na kutekeleza Ibada nyingine maalumu kama hizi:

 

Na itakapokwisha swala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi, ili mpate kufaulu. (62:10)
Tunajifunza kutokana na aya hii kuwa, kuchuma ni wajibu unaompasa Muislamu mara tu baada ya kutekeleza Ibada maalum. Hili linabainishwa katika Hadithi ifuatayo:
“Abdullah bin Mus ’ud ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Kutafuta chumo la halali ni faradhi baada ya kutekeleza faradhi nyingine.” (Baihaqi).
Pia Mtume (s.a.w) amebainisha wazi ubora wa kujizatiti katika kutafuta chumo la halali kwenye Hadith ifuatayo:

 


“Miqdam bin Ma ’ad Yakrab ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Hapana mmoja wenu aliyekula chakula kizuri kuliko kile alichokula kutokana na kazi ya mkono wake mwenyewe. Na Daud, Mtume wa Allah, alikuwa anakula kutokana na kazi ya mikono yake.” (Bukhari)

 


Kwa upande mwingine Uislamu unalaani uvivu na kuwategemea wengine pasi na sababu au dharura maalum kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
“Jubair bin Awam ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Mmoja wenu kuchukua kamba na kisha akaja na mzigo wa kuni akiwa amebeba mgongoni mwake na akauuza, na kwakufanya hivyo Allah akailinda hadhi yake, ni bora kwake kuliko kuomba omba watu, wakimpa chochote au wasimpe (Bukhari.)

 


Mpaka hapo tumejifunza kuwa kwa mtazamo wa Uislamu, uchumi ndio msingi wa maisha ya mwanadamu hapa ulimwenguni na Uislamu umewajibisha kuchuma kwa kila mwenye uwezo. Ni makosa katika Uislamu mtu mwenye uwezo na afya kubweteka na kuwategemea wengine katika kukidhi mahitaji yake.

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    2 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    5 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    6 Magonjwa na afya    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Hukumu ya talaka iliyotolewa kabla ya tendo la ndoa
Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii. Soma Zaidi...

image Namna ya kutayamamu hatuwa kwa hatuwa
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkutayamamu. Soma Zaidi...

image Mambo yanayotenguwa udhu
Post hiibinakwenda kukufundisha mambo ambayo yanaharibu udhu. Soma Zaidi...

image Kugungisha ndoa ya kiislamu hatuwa kwa hatuwa
Hapa utajifunza jinsi ya kuozesha hatuwa kwa hatuwa. Pia utajifunza masharti ya kuoa na masharti ya kuolewa. Soma Zaidi...

image Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawa mirathi
Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu. Soma Zaidi...

image Je mahari inashusha hadhi ya mwanamke katika jamii
Unadhani mwanamke kupewa mahari kitendo hiki kinaweza kushusha hadhi yake? Soma Zaidi...

image Namna ya kurithisgha hatuwa kwa hatuwa.
Hspa utajifunza sasa jinsi ya kugawa mirathi kutokana na viwango maalumu. Soma Zaidi...

image Wafundisheni kuswali watoto wenu
Mtume amemfundisha kuwa watoto wafundishwe kuswali wakiwa na miaka saba na waadhibiwe wakiacha wakiwa na miaka 10 Soma Zaidi...

image Jinsi ya kuoga josho la kiislamu ( janaba, hedhi na nifasi)
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kuoga josho kisheria. Soma Zaidi...

image Hizi ndio nyakati za swala tano na jinsi ya kuchunga nyakati za swala.
Posti hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkuchunga nyakatibza swala tano. Soma Zaidi...