Usaliti unaanza hapa

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

USALITI UNANZA HAPA

Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani. Ndugu zake na Zubeidah kumbwe hawakupendezwa na mafanikio ya ndugu yao. Hali hii iliwafanya kuwa na wifu na kijicho. Basi zubeidah akaongea na ndugu zake na kuwapa mali zile zote na kuwambia mimi shida yangu ni kufika salama na huyu kijana ambaye kwa sasa ni mchumba wangu na tutaoana punde tu tufikapo nyumbani. Mali zile wakagawana ndugu wawili hawa.

 

Hili pia halikutosha wakataka na wawaue kabisa, na kawafanya hivyo katika majira ya usiku. Waliwachukuwa wawili hawa na kuwatia baharini. Anakuja kushituka zubeida yupo baharini anakunywa maji ya chumvi na hatimaye kupoteza fahamu na asijue nini kiliendelea. Basi kwa furaha ndugu wale wakaanza kugawana tena mali zile.

 

Kwa upande wa Zubeidah alopokuja kupata fahamu ilikuwa ni wakati wa jioni na akajikuta amezungukwa na kundi la wananwke wenye sura nzuri za kuvutia waliojipamba vizuri sana. Mbele yake kuna kiti kirefu sana kilichopamba na magodoro yaliyochovywa kwenye dhahabu nyekundu. Miguu ya kiti hicho ni meno ya tembo yaliyopambwa vizuri. Kwa hakika kiti hicho kilikuwa na kila aina ya mapambo mazuri. Aliponyanyua kichwa akaona amekaa juu ya kiti hicho mzee wa heshima mwenye ndevu ndefu zilizo kaa vyema.

 

Zubeida kwa mshangao alionekana kufurahia mazingira yale na asijuwe nini kinaendelea. Alikuja msichana wa makamo hivi aliyependeza sana na akampaka maji ya marashi yaliyochanganywa na misk na kutiwa manukato mazuri sana. Zubeidah akarudisha kumbulkumnbu zake zote na akajuwa kwa mara ya mwisho alitumbukia kwenye maji sasa akawa anajiulia yupo wapi?. Yule mzee akamwambia “mwanangu furahia uwepo wako hapa kwa hakika hupo peponi wala kuzimu, hapa upo chini ya bahari na mbele yako ni mfalme mkuu wa majini yaendayo baharini na nchi kavu. Mzee yule akaagiza kuwa Zubeidah afanyiwe kila kinachostahiki kufanyiwa kisaha akatoweka.

 

Kwa shauku Zubeida alikuwa na maswali mengi sana, wakaja mabinti watatu waliokuwa na sura nzuri sana hata Zubeidah akajiona yeye si lolote wala si chochote, wakamchukuwa na kwenda nae bafunu. Huko maji yaliyo na umoto kwa mbali yalikwisha andaliwa. Kwa mara ya kwanza Zubeidaha anakwenda kuoga maji yaliyotiwa marashi pamoja na misk nyekundu, manukato mablimbali yenye kuvutia. Zubeidah alijihisi yupo ulimwengu wa raha. Kwa maringo na madaha wakamvua ngu Zubeidah na kumtumbukiza kwenye bafu lile na kuanza kumsuguwa.

 

Wakaendelea kumsuguwa kwa visugulio vyenye rangi ya silva vilivyochovywa kwenye marjani. Kwakweli utasema mwili wa Zubeidah umekuwa lulu iliyohifadhiwa vizuri. Uchafu wote mwilini mwa Zubeidah uliondoka hata akawa kama akawa kama aliyofanyiwa scrub na kumbakisha kama mtoto alozaliwa. Ngozi laini na nyusi za kupendeza. Hawakuishia hapo wakaendelea kumpmba na kumpaka manukato. Nguo safi za hariri zenye mapindo yalochovywa kwenye dhahabu, hakika siwezi kuelezea zaidi urembo walomchaguli a



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1260


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Hatima ya kijana mchonganishi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Ndoa ya Siri yafanyika
Posti hii inakwenda kukuendelezea hadithi kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

Mshenga wa aladini mbele ya mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Hadithi ya aliyekatwa vidole gumba
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Dalili za vidonda vya tumbo
Vidonda vya tumbo no tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda,hutokea baada ya ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaitwa mucus kuharibika. Vidonda vya tumbo (peptic ulcers) imegawanyika katika ma Soma Zaidi...

USALITI (sehemu ya tatu)
Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya ukweli ambayo imetokea siku sio nyingi jinsi Moses alipoacha kumwoa Rhoda naye akachanganyikiwa takribani miaka kama mitano hivi. Soma Zaidi...

WAKATI WA KUFUMBUKA
Post hii ni mwendelezo wa hadithi inayohusu Kufumbuka ambapo , John anaonekana kama sio mtoto wa Mzee maganga kwa sababu na miungu imekili kwa sababu chakula chote kimeliwa na kuisha. Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi yeye mwenyew
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa kwanza wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi. Soma Zaidi...

Historia ya zamani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sita
Post hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sehemu ya sita.sehemu hii inaonyesha jinsi bibi alivyo ndumila kuwili na hapendi kuonekana mbaya. Soma Zaidi...