Posti hii inahusu zaidi ushauri kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba, kabisa ya kubeba mimba akina Mama na wachumba wanapaswa kufanya yafuatayo.
Ushauri kwa wachumba na akina Mama kabla ya kubeba mimba.
1.Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa kabla ya kubeba mimba tunapaswa kuwa na maandalizi ili kuepuka kupata watoto wenye ulemavu ambao watafanya tuishi kwa shida na kutumia gharama nyingi ikiwa watapata Magonjwa ambayo yataweza kupatikana kwa kutofuata mashariti au ushauri kabla ya kubeba mimba.
2.Mama au wachumba wanapaswa kula vyakula vyenye mlo kamili kama vile vyakula vya wanga, vyakula vya mafuta, vyakula vya protini, vyakula vyenye madini na vitamini mbalimbali kwa kufanya hivyo pia Mama anapaswa kuwa na damu ya kutosha na kupima Malaria kabla ya kubeba mimba na pia kutumia vidonge au vyakula vya madini ya chuma kwa kufanya hivyo nakuhakikishia kuwa mtoto atakayezaliwa atakuwa salama.
3.Pia Mama anapaswa kuepukana na vitu kama vile matumizi ya madawa ya kulevya kwa sababu usababisha mimba kutoka, kuzaliwa mtoto kabla ya wakati, mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo au mtoto mlemavu. Kwa hiyo akina Mama kama wanatumia madawa ya kulevya kabla ya kubeba mimba waache kabisa ili waweze kupata watoto wa kawaida wasio na matatizo yoyote.
4. Pia wanapaswa kuacha kabisa matumizi ya sigara na vileo vikali kwa sababu usababisha mimba kutoka, kuzaa mtoto mfu, Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati, mtoto kuzaliwa akiwa na umri mdogo na mimba kutoka kwa hiyo akina mama na wachumba kabla hamjabeba mimba hakikisha unaacha kuvuta sigara na matumizi ya vileo vikali.
5.pia Mama na wachumba kabla hawajaanza kubeba mimba wanapaswa kufanya mazoezi ya kiasi sio mazoezi makali kwa sababu yanaweza kusababisha mimba kutoka na pia Mama anapaswa kujiepusha na vitu vyetu mionzi, kwa kufanya hayo tutaweza kupata watoto wenye akili tmamu na magonjwa kwa watoto yatapungua sana.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi faida za dawa za NMN maana yake ni Nicotinamide mononucleotide ni dawa ambazo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali kama vile.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya mucolytic katika kutibu kikohozi kwa watu wazima na watoto.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya ampicillin, ni mojawapo ya dawa za kutibu maambukizi ya bakteria kwenye mwili wa binadamu ba pia ni dawa ambayo IPO kwenye kundi la penicillin kundi hili kwa kitaa huitwa broad spectrum penicillin
Soma Zaidi...Post hii Inahusu zaidi dawa za kutibu maambukizi yoyote Yale yanayosababishwa na bakteria dawa hizi kwa kitaamu huiitwa antibiotics Kuna dawa mbalimbali zinazotibu maambukizi ya bakteria leo tutaanza na dawa ambayo inaitwa penicillin.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala za vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna au njia ya kufanya Ili kuweza kutumia tiba hii ya jino, kwa sababu ya mchanganyiko ambao umekwisha kuwepo kwa hiyo unachumua mchanganyiko unafanya kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya Acetohexamide kwa matibabu ya sukari, kama tulivyoona katika post iliyopita kwamba kuna kipindi ambacho kongosho linatoa insulini lakini seli haziko tayari kupokea hiyo insulini.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa aina ya ketoconazole ni dawa inayotumika kutibu fangasi za kwenye koo.
Soma Zaidi...