image

Usitamani kifo hata ukiwa mchamungu mno ama muovu mno

Katika uislamu imekatazwa kutamani kufa hata kama utakuwa ni mtu muovu sana ama mchamungu sana.

 


 

KATU USIYATAMANI MAUTI

 

UTANGULIZI

Kifohutisha sana na ni chenye maumivu makali yasiyoweza kuelezeka. Kwa hakika kifo kinatisha sana kwani utakapokufa katu hutoweza kurudi tena duniani. Ukweli ni kwamba watu wengi wanaogopa kufa, ijapokuwa wapo ambao inafikia hatua hawaogopi kifo kabisa, lakini pia inaweza kufikia hatua kwa baadhi ya watu mpaka wakakiomba kifo. Hii huwenda ni kutokana na shida na taabu walizo nazo. Lakini katika uislamu IMEKATAZWA KATU KUTAMANI KIFO. Makala hii ni darsa la Hadithi linalokwenda kukueleza yale ambayo Mtume (s.a.w) ameyasema kuhusu kutamani kifo, na ikifikia hatua bora mtu afe kwa shida alizo nazo ana kwa namna nyingine nini aseme.

 

Makala imeandika wa  Al-Ustadh Rajabu Athumani na kusambazwa kwako katika tuvuti hii ya bongoclass. Unaweza kushea Elimu hii ya bure, iwe kama sadaka kwako na kuonyesha juudi zako katika kusambaza elimu ya dini. Kabla ya kuendelea na Darsa hii ningependa kukutangazia kwamba, darsa hizi ni za bure na unaweza kupata kitabu cha darsa hizi ukijisajili kwenye maktaba yetu. Pia tembelea tovuti hii kuna darsa nyingi za dini zinakusubiri.

 

SABABU ZA KUTAMANI MAUTI

Sifa njema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, sala na amani zimfikie kipenzi wa umma Mtume Muhammad(s.a.w). yeye na sahaba zake. Darsa letu hili tutaanzia na hadithi iliyopokewa kutoka kwa Mtume na Abuu huraira kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Asitamani mmoja wenu Mautu (kifo) ima akiwa ni mwema kwani huenda akazidisha heri ama akiwa ni muovu huenda akatubia.

عنْ أبي هُريرة رضيَ اللَّهُ عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قالَ : » لا يَتَمَنَّ أَحَدُآُمُ المَوْتَ إِمَا مُحسِناً ، فَلَعَلَّهُ يَزْدادُ ، وَإِمَّا مُسِيئاً فَلَعَلَّهُ يَسْتَعْتِبُ « متفقٌ عليه، وهذا لفظ البخاري

 

Kutokana na mafunzo ya hadithi hii kwa nza tunapata kujuwa kuwa:-

 

Mafunzo ya hadithi hii yapo wazi kabisa. Kwani kwa hakika swala la kutamani mauti sio jambo jema katika dini. Na katika mapokezi mengine hadithi hii imesema kuwa:

لا يَتَمَنَّ أَحَدُآُمُ المَوْتَ ، وَلا يَدْعُ بِهِ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَأْتِيَهُ ، إِنَّهُ إِذا ماتَ انْقَطَعَ عَمَلُهُ ، وَإِنَّهُ لا يَزيدُ المُؤْمِنَ عُمْرُهُ إِلاَّ خَيرا

Mtume s.a.w amesema “asitamani mmoja wenu mauti na wala asiyaombe mauti kabla hayajamjia kwani hakika pindi atakapokufa, amali zake zote zinakatika, na kwa hakika hautamzidishia muumini umri wake isipokuwa heri”.

 

Hadithi hii inazidi kutupatia funzo zaidi kuwa tusitamani kufa na si kutamani tu bali hata tusithubutu kufa, kwani kama tutapewa uhai zaidi na tukiwa wema huenda uhai wetu ukawa ni chachu ya sisi kuzidisha wema. Na kama tukiwa ni waovu huenda tukatubu. Hadithi zote mbili hizi zinatujulisha kuwa kifo hakitakiwi kukitamani wala kukiomba.

 

Kuna kitu kingine hapa kimeelezwa kuwa pindi tu mtu akifa amali zake zote zinakatika. Yaani kama ni muovu na hajatubia madhambi yake kwa Allah basi hatoweza tena kutubia, na kama ni mwema hatoweza kufanya tena mambo mema. Katika hadithi nyingine Mtume wa allah ameeleza kuwa”atakapokufa mwanadamu amali zake zote (matendo) hukatika isipokuwa matendo ya (amali) aina tatu SADAKA YENYE KUENDELEA, ELIMU YENYE KUPATISHA MANUFAA AU MTOTO MWEMA ATAKAYEMUOMBEA DUA”. haya ni katika matendo ambayo yataweza kutupatisha faida pindi tutakapo fariki.

 

IKIWA HUNABUDI ILA NI KUFA UFANYE NINI

Wakati mwingine mwanadamu anapata taabu na shida kama maradhi. Maradhi kama ya saratani na mengineyo. Inatokea mpaka mwanadamu kwa maumivu ayapatayo na maradhi yake si yenye kutarajiwa kupona basi kwa taabu na shida anaamuwa kuomba bora afe. Hili pia limekatazwa kwenye uislamu. Lakini mtua akiwa a hali kama hii ama hali ambazo zinafanana na hii na akiwa hana budi isipokuwa ni kufa na akawa anatamani bora afe, basi Mtume s.a.w ametufundisha amaneno ambayo tunatakiwa kuyasema:

وعن أنسٍ رضي اللَّه عنه قال : قالَ رسولُ اللَّه صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : لا يَتَمَنَّيَنَّ أَحَدُآُمُ المَوْتَ لِضُرٍّ أَصَابَهُ فَإِنْ آانْ لابُدَّ فاعِلاَ ، فَلْيَقُل : اللَّهُمَّ أَحْيِني ما آانَتِ الحَياةُ خَيْراً لي ، وتَوَفَّني إِذا آانَتِ الوفاةُ خَيراً لي « متفقٌ عليه

Katia hadithi iliyopokewa na Anas kutoka kwa Mtume (s.a.w) kuwa Amesema Mtume (s.a.w) kuwa “asitamani mmojawenu mauti kutokana na madhara yaliyompata, na ikiwa hanabudi (ila ni kufa ama kutamani mauti ) basi na aseme “ALLAHUMMA AHYINII MAA KANAT ALHAYAAT KHIRAN LII, WATAWAFFANII IDHAA KAANAT ALWAFAAT KHAIRAN LII” (“Ewe Mwenyezi Mungu nipe uhai ikiwa uhai ni bora kwangu na unifishe ikiwa kifo ni bora kwangu”

 

Hadithi hii inatufundisha maneno ambayo mtu ayaseme kumwambia Allah ikiwa hanabudi isipokuwa ni kuomba kifo. Ukiiangalia vizuri hadithi hii maneno haya yamegawanyika katika vipengele vitatu na kila kipengele kimebeba ujumbe mzito sana. Hebu tuangalie kwa ufupi kabisa hadithi hii vipi tuielewe kwa kupitia vipengele hivi:-

 

KWA NINI IMEKATAZWA KUOMBA MAUTI (KIFO)?

Kama ukiangalia vyema hadithi tajwa hapo juu ni dhahiri kuwa kuomba mauti kumekatazwa kwa sababu kuu zifuatazo:-

  1. mtu akifa amali zake na matendo yake hukatika hivyo ni bora asiombe kifo ili aendelee kufanya amali.
  2. Mtu muov akiwa hai huenda akatubu
  3. Mwenye matatizo na taabu huenda kwa rehma za Allah akaondokewa na matatizo yake pindi akiwa hai
  4. Mtu mwema huenda akaendelea kufanya heri na kupandisha darja yake pindi akiwa hai
  5. Shida na taabu ni mitihani ya allah, huenda ukafaulu mitihani hiyo na kupandishwa daraja mwele ya Allah.
  6. Kukimbia tatizo sio njia njema, kinachotkiwa na kupambana na tatizo na si kuomba kufa ili kulikimbia tatizo.
  7. Huenda uhai ukawa bora zaidi kwako kuliko kifo.

 

MWISHO

Kwa kufunga darsa ni kuwa uislamu umekatiaza kuomba umauti, kujiuwa ama kuuwa. Leo hii kuna watu wanazidi kutumia dawa za kuuwa watu wakidai eti wanawapunguzia machungu ya maisha. Kuna madaktari wanathubutu hata kumaliza maisha ya wagonjwa kwa kigezo kuwa mgonjwa hatapona na akiendelea kuishi atakuwa kwenye maumivu tuu. Njia hizi zote haziruhusiwi kwenye uslamu.

 

Ndugu yangu Muislamu, sisi ni waislamu tuliojitolea kwa ajili ya Allah katika kufikisha ujumbe wa Allah. Hatulipwi na yeyote na katika kufanya kazi hii. Uaweza kutuunga mkono katika kuifanya kazi hii kwa kushea elimu hii, ama kuandika makala kama hizi na kututumia, ama kutusaidia kuediti na kuondoa makosa yote ya kielimu na kitaalamu katika tovuti hii. Kazi hii hutalipwa na mtu yeyote, sote tunajitolea kwa ajili ya Allah.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 737


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

jamii
Soma Zaidi...

MAMBO YANAYOBATILISHA (HARIBU) SWALA YAKO
Lugha ya Swala Lugha ya swala,kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu. Soma Zaidi...

Taratibu za eda ya kufiwa katika uislamu
Hapa utajifunza taratibu za kukaa eda kwa mwanamke ambaye amefiwa na mume. Soma Zaidi...

Ubainifu kati ya halali na Haramu na kujiepusha na mambo yanayo tatiza
عَنْ أَبِي عَبْدِ اللَّهِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: سَمِعْت رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم يَقُ?... Soma Zaidi...

Hukumu na taratibu za ndoa katika uislamu
Soma Zaidi...

Maana ya Ndoa na Faida zake katika jamii
4. Soma Zaidi...

Maana ya hadathi na aina zake
Post hii inakwenda kukugundisha maana ya hadathi pamoja na kutaja aina za hadathi Soma Zaidi...

Mifumo ya benk na uchumi wa kiislamu
7. Soma Zaidi...

Nguzo za udhu ni sita
Post hii itakufundisha kuhusu nguzo kuu sita za udhu. Soma Zaidi...

Aina za hijjah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Namna ya kutambuwa kibla na umuhimu wa kuelekea kibla wakati wa kuswali
4. Soma Zaidi...

Kumuandaa Maiti kabla ya kufa ama kukata roho
Soma Zaidi...