image

Utajuaje Kama simu au kompyuta yako Ina virus

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kujua Kama simu yako ina virus

UTA JUAJE KAMA SIMU AU KOMPYUTA YAKO INA VIRUSI?Katika post hii vip utaweza kujuwa kuwa kifaa chako kina virusi.Malware ni pamoja na virusi worm na trojan. Wote hawa hwanaweza kuharibu mafaili katika kifaa chako. Ila jambo ya kujuwa ni kuwa huwa wana baadhi ya sifa za kufanana wanapokuwa wanadhuru kifaa chako.Kwa kutumia mfanano huo utaweza kugunduwa uvamizi katika kifaa chako.         

  NJIA ZA KUTAMBUWA VIRUSI KATIKA KIFAA CHAKO:

1.Kifaa chako kutokuwa na kasi katika ufanyaji kazi (slow); Hapa inaweza ikatokea unabonyeza batani lakini inachelewa kufanya kazi. Wakati mwengine unaweza ukabonyeza batani ya kuangalia meseji lakini ikachelewa kufunguka mpaka unasubiria kwa muda kidogo.Ijapokuwa tatizo la kifaa chako kuwa slow linaweza kusababishwa na mabo mengine kama vile RAM, kuwepo kwa Spyware, na kujaa kwa hard disk, lakini kuwepo kwa virusi huwa ni chanzo kikubwa kama RAM na Hard disk ikawa safi yaani ikawa na uwezo wa kutoshelezea mahitaji yako.kuweza kutatuwa tatizo hili tulisha eleza katika baadhi ya post zetu, ila kwa ufupi hakikisha kifaa chako kina nafasi ya kutosha katika memory yake au hard disk. Hkikisha mstari mwekundu wa kuonesha kuwa memory au Hard disk imejaa haupo, Hakikisha kompyuta yako ina RAM ya kutosha kwa mahitaji ya kifaa chako. Skann virusi kwa kutumia ant virus iliyo madhubuti na iliyo up to date.

2. Kuchelewa kufunguwa internet, Hapa huwa kifaa chako unapofunguwa intanet kinachelewa kuload. inatokeaa unabonyeza batani ya kusearch lakini unasubiria muda mrefu. Unapokuwa unadownload kifaa chako kinachelewa sana kudawnload. Kwa ufupi intanet kuwa slow husababishwa na kuwepo kwa virusi kwenye kifaa chako.Ijapokuwa zipo sababu zingine zinazosababisha kifaa chako kuwa slow kwenye intanet kama vile netwprk kuwa kidogo. HIvyo kabla haujajiridhisha kuwa kifaa chako kina virusi kwanza hakikisha kuwa unamtandao wa kutosha kwenye kifaa chako. Pia hakikisha umeruhusu 3G au 4G katika kifaa chako. Kama itakuwa bado slow anza taratibu za kuondowa virusi katika kifaa chko.3. Program kujifunguwa zenyewe; Hapa inatokeya baadhi ya program katika kifaa chako ziajifunguwa zenyewe bila ya kuruhusiwa. Hiki ni kiashiria kimojawapo cha kuwepo kwa virusi katika kifaa chako. Jambo la kufanya hapa ondowa proram hizo zinzojifunguwa zenyewe kisha skan viruri katika kifaa chako.Tatizo la kuwa na virusi katika vifaa vya kielectronoc ni lakawaida, na ni vigumu kuliepuka kabisa. Jambo la kufanya ki kuwa na utaratibi wa kutazama kifaa chako kila wakati kama kuna athari yoyote. kuwa na utaratibu wa kuskani kifaa chako. Au ruhusu auto scan. yaani kifaa chako kiwe kinajiskani chenyewe kulingana na muda utakaotaka. Jambo la kuzingatia zaidi hapa ni kuhakiisha ant virusi uliyo nayo ipo vizuri kwa kufanya kazi hii.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1430


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Tofauti ya Trojan na virusi
Posti hii inakwenda kukupa tofauti za trojani na virusi Soma Zaidi...

Nini Chanzo
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

JINSI YA KUDOWNLOAD VIDEO YOUTUBE
NJIA RAHISI YA KUDOWNLOAD VIDEO YOUTUBE Teknolojia ya mawasiliano ni muhimu katika kuhakikisha kuwa ulimwengu unafikika kama kijiji kimoja na hapa ndipo unapata maana halisi ya neno UTANDAWAZA yaani kwa lugha ya kimombo ni globalization. Soma Zaidi...

Je nitumie simu yangu wakati inachaji?
Somo hili linakwenda kujibu swali la je nitumie simu yangu wakati inachaji Soma Zaidi...

teknolojia
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Kutuma sms ndefu
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

Muda wa kuchaji simu yako
Posti hii itakwenda kukujuza juu ya kuda mzuri wa kuchaji simu yako Soma Zaidi...

SIRI
Hii ni game ya maandishi bila ya kutumia vioneshi (graphics). Soma Zaidi...

Kipi kingine utafanya ukiwa Facebook
Somo hili linakwenda kukueleza Mambo mengne unayoweza kuyafanya ukiwa Facebook Soma Zaidi...

KULINDA AKAUNT YAKO YA FACEBOOK DHIDI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO
Watu wengi wanalalamika kuwa akaunti zao za facebook zimehakiwa, yaani zimeshambuliwa na wahalifu wa kimtandano. Soma Zaidi...

Matumizi ya OCR katika simu yako
Somo Hili linakuleteq mafunzo ya OCR katika simu yako Soma Zaidi...

TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO
Soma Zaidi...