Uvutaji wa sigara

Somo Hili linakwenda me kuhusu madhara ya uvutaji wa sigara

.UVUTAJI WA SIGARA"uvutaji wa sigara ni hatari kwa afyaTafiti mbali mbali kuhusu sigara zinaonesha kuwa watu wameanza kuvuta sigara zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Historia zinaonesha kuwa misafara ya kibiashara na isiyo ya kibiashara imeshangia kueneza uvutaji wa sigara duniani. Inadaiwa cristopher columbas miaka ya 1492 aliwakuta watu maeneo ya America wakavuta sigara. Kutoka hapa sigara ikaenea maeneo ya ulaya kwa kupitia misafara hii.Mwanzoni iliaminika kuwa sigara hutibu baadhi ya magojwa. Dhana hii ilienea sana miaka ya 1600 ambapo watu wengi walijikita katika uvutaji wa sigara. Mnamo miaka ya 1800 viwanda vya kutengeneza sigara vilianzishwa japo sigara ilikuwa na bei kubwa.Miaka ya 1940 tafiti mbalimbali za kisayansi zilianzwa kufanya kuhusu sigara. Na hili lilitokea pale ambapo madaktari walipoanza kuhisi uhatari wa sigara kwa afya. Hapa wakaanza kuhusanisha sigara na saratani ya ini na mapafu. Mpaka kufikia miaka ya 1964 ripoti za kisayansi katika fani ya madaktari ziliwasilishwa marekani zikionesha uhatari wa sigara kwa afya ya watu.Kuanzia hapa maonyo mbalimbali yakaanzisha kuwaonya watu na uvutaji wa sigara. Kwanzia hapa ikaanzwa kukatashwa rasmi uvutaji wa sigara kwenye ndege, mikusanyiko ya watu, hospitali na maeneo mengine ya maofisi. Maonyo mengine yakawekwa kwenye pakti ya sigara.Sigara zinatengenezwa na tumbaku, huu ni mmea ambao unapatikana karibia dunia nzima. Tafiti za kisayansi zinaoneshakuwa tumbaku lina zaidi ya kemikali 400, ambapo nikotin ndio maarufu zaidi. Kwa ujumla kemikali hizi ni hatari kwa maisha ya mtu na afya ya jamii. Katika kemikali hizi nikotini ni sumu zaidi.Nikotini inapotumiwa huweza kuamsha mfumo wa neva, na kusababisha mapigo ya moyo kuenda kwa kasi zaidi. Nikotini ina hali ya kuwa addictive. Yaani mtu akisha izoea hawezi kukaa bila ya kuipata, nah ii ndio maana ni vigumu kuacha uvutaji wa sigara.Miongoni mwa hatari ambazo uvutaji wa sigara humletea mvutaji ni saratani ya mapafu. Tafiti zinzonesha kuwa sigara huenda ikawa ndio chanzo kikubwa cha saratani ya mapafu kuliko vyanzo vingine. Wavutaji wa sigara wapo hatarini kupata saratani ya mapafu kwa mara 20 zaidi ya wasiovuta. Pia sigara ni chanzo za aina zingine za saratani."hateful to the nose, harmful to the brain, and dangerous to the lungs." This was the view of England's king James I in 1604



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021/11/11/Thursday - 12:12:20 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1216


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Zijue kazi za ovari
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa ovari kwenye mwili wa mwanamke. ovari ni sehemu ambapo mayai ya mwanamke hutunza, kwa hiyo kila mwanamke huwa na ovari ambayo husaidia kutunza mayai. Soma Zaidi...

Kushiriki ngono na mtu aliye na vvu na ukimwi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kushiriki-ngono-na-mtu-aliye-na-vvu-na-ukimwi Soma Zaidi...

Namna ya kumsaidia mgonjwa aliye na Maambukizi kwenye milija na ovari
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia wagonjwa waliopata maambukizi kwenye milija na ovari, ni wagonjwa waliopata maambukizi kwenye milija na ovari. Soma Zaidi...

Imani potofu kuhusu kifua kikuu
Posti hii inahusu zaidi imani potofu waliyonayo Watu kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu, hizi ni imani ambazo uwepo kwenye jamii na pengine uweza kuaminika lakini si za ukweli. Soma Zaidi...

Huduma ya kwanza kwa mtu aliyekula sumu
Post hii inahusu zaidi kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyekula chakula chenye sumu, kula sumu ni kitendo Cha kula kitu chochote kama dawa,pombe, kemikali na chakula kichafu. Soma Zaidi...

Vipimo vya minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vipimo vya minyoo Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa aliyepatwa na presha ya kushuka
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na presha ya kushuka Soma Zaidi...

Kazi ya chanjo ya kifua kikuu
Posti hii inahusu kazi ya chanjo ya kifua kikuu kwa kitaalamu huitwa BCG. Ni chanjo ambayo uzuia kifua kikuu na ukoma. Soma Zaidi...

Njia ambazo maradhi huambukizwa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo maradhi huambukizwa Soma Zaidi...

Upungufu wa vitamin
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vitamin Soma Zaidi...

Zijue kazi za ini
Post hii inahusu zaidi kazi za ini, ni kiungo muhimu kwenye mwili ambacho Kina umuhimu sana, bila ini maisha ya mwanadamu yanaweza kuishia pabaya Soma Zaidi...

Huduma ya kwanza kwa mwenye uchafu kwenye sikio.
Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kqa mgonjwa aliyeingiliwa na kitu au uchafu kwenye sikio. Soma Zaidi...