image

Uzuri wa Benki za kiislamu

Kwa nini benki za kiislamu ni bora kuliko benki nyingine?

Uzuri wa benki za Kiislamu
Pamoja na benki za Kiislamu kutoa huduma zinazotolewa na kila benki kama tulivyoziorodhesha huko nyuma, kuna faida za ziada zinazopatikana kutokana na benki hizi kama ifuatavyo:

 


Kwanza benki za Kiislamu huiokoa jamii na uchumi wake na madhara yote yanayosababishwa na riba.

 

Pili, Benki za Kiislamu huwaingiza katika uchumi na kuwainua hata wale ambao hawana hata rasilimali yoyote kwa mtindo wa Mudharabah. Hivyo ni kwamba, benki zinazoendeshwa kwa mikopo ya riba, haziwezi kukopesha fedha zake kwa mtu yeyote asiye na rasilimali yenye thamani sawa au zaidi ya mkopo ili atakaposhindwa kulipa ifilisiwe rasilimali hiyo. Kwa mtindo huu wa mikopo ya riba, ni matajiri tu wanaopata mikopo ya benki na masikini wasio na rasilimali yoyote huachwa hivyo hivyo na umasikini wao bila ya msaada kutoka benki wa kuwainua kiuchumi.

 


Tatu, benki za Kiislamu huinua uchumi wa jamii, kutokana na umakini na tahadhari kubwa zinazochukua katika kuchagua na kuendesha miradi mbali mbali ya uchumi. Kwa kuwa benki zenyewe zinajiingiza katika uchumi, zinahakikisha kuwa miradi zitakazoichagua ni ile yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha faida kubwa na yenye uwezekano mdogo wa kusababisha hasara.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1107


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

nyakati za swala
3. Soma Zaidi...

Swala ya idil fitir na idil haji nanjinsi ya kuziswali
Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya idil haji na swala ya idil fitir Soma Zaidi...

Wanaostahiki kupewa zakat
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Tofauti kati ya zakat na sadaqat
Nguzo za Imani, tofauti kati ya sadaqat na zakat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sifa za uchumi wa kiislamu na njia halali za uchumi na umiliki mali katika uislamu
Soma Zaidi...

Hukumu ya kufinga kwa kifuata kuandama kwa mwezi
Ni muda gani unatakiwa ufunge ramadhani, je kuandama kwa mwezi kwa kiona ama hata kusiki. Soma Zaidi...

Jinsi ya kiswali swwla ya dhuha na faida zake
Post hii inakwenda kukufunza kuhusu swala ya dhuha, faida zake wakati wa kuiswali swala ya dhuha na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

Namna ya kujitwaharisha Najisi ndogo
Soma Zaidi...

Swala ya jamaa na mnamna ya kuswali swala ya jamaa, nyumbni, msikitini na kwa wanawake
Soma Zaidi...

sadaka
Soma Zaidi...

NINI MAANA YA KUSIMAMISHA SWALA, KATIKA UISLAMU (NI YUPI TARQU SWALA) yaani mwenye kuacha swala)
Kusimamisha Swala. Soma Zaidi...

Aina za tawafu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...