Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

VIATU VYA AJABU VYAONDOKA NA MKONO WANGU

Aliponieleza sifa za viatu anavyotaka nikamsogelea kwa ukaribu na kumkazia macho kama nataka kumpiga vile kisha nikamuuliza “wewe ni nani, na ni nani amekutuma, vina nini hasa viatu hivi” alibakia kimya kwa muda kidogo kisha aksema “baba anakutafuta, anakuhitaji uende nyumbani”. nikamuahidi kuwa nitakwenda siku ya ijumaa. Basi akaniahidi kuwa atakuja na ndugu yake kesho kuja kunielekeza nyumbani kwao.

 

Kesho yake nikaandaa pale ndani chumba kingine kitupu. Nikaweka vyakula na vinywaji. Alipokuj tukaendelea kuburudika na wageni wangu watatu wenzie wamefunika sura zao. Mmoja kati yao alitoka nje, kisha baada ya muda akarudi. Basi kumbe alikwenda chukuwa dawa bila ya sisi kujuwa akiweka kwenye kinywaji na tukalewa, na kuja kuamka ni usiku na nilipowasha taa nikakuta pembeni yangu kuna kichwa cha yule binti wa siku zote aliyetaka viatu. Sikuweza kuwaona wenzie wawili.

 

Nilishituka sana kuona binti amekufia kwangu, nikafunga duka na kuchimba shimo uwani nikamfanyia maiti yake maandalizi yote na kumzika kwa siri. Usiku huohuo niliondoka na kurudi misri. Nikawa kila baada ya miezi 6 nalipa pesa ya ada ya kile chumba. Nilikaa misri kwa muda wa miaka mitatu hata nikajiridhisha kuwa huwenda mpaka sasa wakawa wamesahau kilichotokea. Nikaamuwa kurudi tena Yemeni ili nikamalize kazi yangu ya kuwatafuta wale watu. Pia kukutana na yule mzee aliyenitafutaga.

 

Nilifika Yemeniwakati wa usiku, nikaingia dukani kwangu na kuanza kusafisha, alama za michirizi ya damu zilikuwa zikionekana. Nilisafisha, sasa nilipokuwa naamsha viti ndipo nikaokota pete. Pete ilikuwa na picha ya kichwa cha mamba kwa juu. Picha ya kichwa cha kunguru na kambale kwa upande wa pembeni kulia na ushoto. Nikaamuwa kuiuza pete ile nipate pesa za kuanzia maisha. Nikaenda kwa sonara wa kwanza akasema hanunui pete ila maana ni ya thamani sana.

 

Nikaenda kwa sonara mwengine akaniambia nisubiri. Akaondoka kidogo na kwenda alikokwenda kisha akarudi. Akanieleza kuwa hawezi kununua. Kume aipotoka alikwenda kutoa taarifa kuwa pete iliyoibiwa imeonekana. Usiku askari wakanifamia na kunibambikia kesi ya wizi vinginevyo nitaje jinsi nilivyoipata pete ile. Mbele ya kadhi nilishindwa kueleza ukweli nikiamini kuwa nikieleza ukweli ndio nitauliwa. Nikamueleza niliiba kwa binti mmoja.

 

Baada ya hapo kadhi akanipa hukumu ya kukatwa mkono wangu. Nilishukuru kukatwa mkono ili kunusuru kichwa changu. Walinikata mkono, nilipata maumivu makali sana, damu ilitoka na nikapoteza fahamu. Nilipokuja kushituka nikajikuta nipo kwenye kitanda. Nilijiuguza pale kwa muda wa siku tatu. Siku ya nne akaja mzee mmoja mrefu mwenye sura ya heshima. Kwa kumuangalia utajuwa kuwa ni mchamungu, pia ni tajiri. Akaniambia “mwanangu, najua hii pete hukuiiba, naelewa fika hii pete haiwezi kuibiwa, hivyo basi nieleze historia yako na hadi likatokea hili la kutokea”. nikaanza kumueleza mpaka mwisho, kuanzia wageni wa baba, hata nikafika Yemeni na haliyotokea.

 

Nilipomaliza kusimulia yule mzee alikuwa akitokwa na machozi kisha akaema kwa hakika umesema vyema kwa hakika hukudanganya. Nilitambua historia yako hata kabla hujaitaja. Nilitaka kuthibitisha ukweli wa maneno yale, yaliyonenwa na wageni wale, yapata miaka 10 iliyopita. Mwananfu kuwa na amani hapa ulipofika ni kwenu, na jihisi upo kwa baba yako. Natambua yaliyomkuta baba yako, mwanangu na wewe. Nitakueleza kuanzia tafsiri ya waliyoyatenda wageni wale kwenu, na maswali mlioyashindwa kuyajuwa kuhusu wageni wale



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-07     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 761


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kutokana kwenye kisima mpaka kuwa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Kwanini dirisha moja?
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sita
Post hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sehemu ya sita.sehemu hii inaonyesha jinsi bibi alivyo ndumila kuwili na hapendi kuonekana mbaya. Soma Zaidi...

Aladini na binti wa mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu Soma Zaidi...

Siku ya sita ya wageni
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hadithi ya tabibu wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Jaribio la tatu la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Safari saba za sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Hadithi ya chongo wa pili mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Mafundisho kutokana na hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mafundisho ambayo tunayapata kutoka kwa binti mfalme, tunapotoa hadithi sio kusoma na kufurahia tu ila kuna mafundisho muhimu katika maisha yetu. Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa pili wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Alif lela ulela
Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...