Allah hutumia maandishi kuwafundisha wanadamu. Mfano mzuri ni nabii Musa ambaye alipewa vibao vya maandishi.
(e) Njia ya Maandishi: Njia nyingine anayoitumia Allah (s.w) katika kuwasiliana na waja wake ni njia ya maandishi, yaani maandishi yaliyoandikwa tayari. Nabii Mussa (a.s) aliletewa ujumbe kutoka kwa Allah (s.w) kwa maandishi yaliyoandikwa tayari katika mbao kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
“Na tukamwandikia katika mbao kila kitu mawaidha (ya kila namna) na maelezo ya kila jambo. Basi yashike kwa imara na uwaamrishe watu wako wayashike vema haya…” (7:145)
“Na Musa zilipotulia ghadhabu zake, aliziokota zile mbao. Na katika maandiko yake (hizo mbao) ulikuwamo uwongofu na rehema kwa wale wanaomuogopa Mola wao”. (7:154). Kwa ujumla tumeona kuwa chanzo cha elimu ni “Allah (s.w).
Lolote tunalolifahamu tumefunzwa na Allah kwa njia mojawapo katika njia tano tulizoziona.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao: "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho"; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini.
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hichi tutajifunza makundi ya dini za watu. Na makundi hayo ni matatu.
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa.
Soma Zaidi...Njia ambazo Allah hutumia kuwasiliana na wanadamu nakuwafundisha elimu mbalimbali. (Edk form 1 dhana ya Elimu)
Soma Zaidi...Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...