Vipimo muhimu wakati wa ujauzito

Post hii inahusu zaidi vipimo muhimu wakati wa ujauzito ni vipimo ambavyo vinapaswa kupimwa na Mama ili kuangalia mambo mbalimbali katika damu au sehemu yoyote, pia vipimo hivi umsaidia sana Mama kujua afya yake.

Vipimo muhimu wakati wa ujauzito.

1. Upimaji wa damu ili kuangalia kiwango cha damu kilichomo mwilini, kwa kawaida mjamzito kabla ya kujifungua anapaswa kuwa na damu ya kutosha kwa sababu wakati wa kujifungua Mama utoa damu nyingi sana kwa hiyo kila mwezi mama uchukua dawa za follic ili kuweza kuongeza damu na pia akina Mama uambiwa kula vyakula muhimu vya kuongeza damu kwa hiyo wajawazito wote nwanapaswa kupima na kuangalia kiasi cha damu kilichomo mwilini mwa Mama.

 

2. Upimaji wa damu ili kuangalia group la Mama na baba kama zinaendana, mara nyingi Watu wengi wameoana tu na hawajui magroup yao ya damu hali hii uleta shida kwa mtoto wakati wa kujifungua kwa sababu pengine ya kuwepo kwa RH ambayo usababisha kutokwa kwa mimba na kwa upima magroup yao ya damu kila mtu anaweza kujua watu gani anapaswa kuwapatia na mtu gani atapokea kutoka kwake.

 

3. Pia Mama mjamzito anapaswa kupima kaswende kwa sababu ugonjwa huu ni hatari pindi akiwa tumboni kwa hiyo wazazi wote wanapaswa kuudhulia kliniki kwa mara ya kwanza ili waweze kupima maambukizi ya kaswende, kama wote wanayo wanapaswa kutibiwa ili kuepu kujifungua mtoto mwenye ugonjwa huu maana ni hatari.

 

4. Pia Mama mjamzito anapaswa kupima  maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na hatimaye kumwepusha mtoto kuzaliwa akiwa na Maambukizi, na pia kujua afya ya Mama  ili kuweza kuwa makini wakati wa kujifungua na kuepusha kuendelea kumpatia huduma na kuendelea vizuri, pia  Baba na Mama wote wanapaswa kujua hali zao na kuendelea na matibabu.

 

5.Mama mjamzito anapaswa kupima Malaria.

Tunajua kubwa Malaria ni tishio kwa Mama wakati wanapaswa kupima ugonjwa wa Malaria, kwa kuwa Mama mara nyingi upewa dawa za SP ili kuweza kuzuia Malaria kwa Mama mjamzito na mtoto kwa hiyo ni jambo la muhimu kupima Malaria na kuepuka shida yake mbalimbali.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/01/13/Thursday - 12:53:55 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1124


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Wajibu wa mjamzito katika utaratibu wa uleaji wa mimba
Posti hii inahusu zaidi wajibu wa Mama mjamzito katika kileo mimba sio yeye tu Bali na wote waliomzunguka wanapaswa kuhakikisha kuwa mama mjamzito anapaswa kufanyiwa huduma zote Ili kuweza kujifungua salama na bila shida yoyote. Soma Zaidi...

Kupima ujauzito kwa kutumia chumvi, sukari na sabuni
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupima mimba kwa kutumia chumvi sukari na sabuni Soma Zaidi...

Ugumu wa choo na tiba yake kwa wajawazito
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa ugumu wa choo na tiba yake kwa wajawazito, ni ugonjwa unaowapata sana akina mama wajawazito na uisha tu pale Mama anapojifungua kwa hiyo tunapaswa kujua wazi sababu za ugumu wa choo na tiba yake kwa wajawazito. Soma Zaidi...

Faida na hasara za Kufunga kizazi kwa Wanaume
Posti hii inazungumzia Faida, hasara, na madhara ya Kufunga kizazi kwa Wanaume. Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia kwa mama ili apate huduma endelevu.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na huduma kwa mama wajawazito na waliojifungua. Soma Zaidi...

Mambo muhimu kwa wanawake kabla ya kubeba mimba
Posti hii inahusu zaidi mambo muhimu kwa wanawake kabla ya kubeba mimba,Ni mambo ya kuzingatia ili mama akija kubeba mimba awe mzima kimwili, ki afya na kisaikolojia na hivyo hivyo Mtoto atakayezaliwa atakuwa salama. Soma Zaidi...

Mwanamke mwenye HIV akiwa mjamzito ama ananyonyesha
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mwanamke mwenye HIV akiwa mjamzito ama anaenyonyesha Soma Zaidi...

kunauwezekano wa darri ya kchefuchefu ictokee kabsa kwa mjauzito
Kichefuchefu ni moja katika dalili za mimba za mapema, Lucinda je upo uwezekano kwa mwanamke kuwa na ujauzito bila hata ya kuwa na kichefuchefu? Soma Zaidi...

Habari, naomba kuulizia, nimadhara gani atayapata mwanamke akitolewa bikra bila kukusudia
Je unawaza nini endapo bikra itatolewa bila wewe kukusudia, je imetolewa kwa njia ya kawaida yaani uume ama ilikuwa ni ajali? Soma Zaidi...

Malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama.
Posti huu inahusu zaidi malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama, ni huduma muhimu ambazo zimetolewa kwa akina Mama ili kuweza kuepuka hatari mbalimbali zinazowakumba akina Mama wakati wa ujauzito, kujifu na malezi ya watoto chini ya miaka mitano. Soma Zaidi...

Huduma kwa mwenye maumivu ya tumbo la hedhi
Posti hii inahusu msaada kwa mwenye maumivu ya tumbo la hedhi, hizi ni huduma ambazo utolewa kwa wale wenye maumivu ya tumbo la hedhi. Soma Zaidi...

Damu, uteute na maji yanayotoka ukeni kipindi cha ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu damu, uteute na maji yanayotoka ukeni kipindi cha ujauzito Soma Zaidi...