Kuanzishwa kwa Polisi na magereza kati uislamu wakati wa Makhalifa

Kuanzishwa kwa Polisi.

Kuanzishwa kwa Polisi na magereza kati uislamu wakati wa Makhalifa

Kuanzishwa kwa Polisi.



Kuanzishwa kwa Polisi Wakati wa ukhalifa wa Umar ilikuwa hatua nyingine ya kupunguza makosa na kusimamia haki katika jamii. idara hii iliitwa Ahdath na mkuu wake aliitwa Sahib Al-Ahdath (mkuu wa Polisi) Maafisa kadhaa waliteuliwa katika sehemu kadhaa ili kudhibiti makosa; kwa mfano kudhibiti vipimo na mizani, usalama wa barabara kama kutojenga nyumba barabarani, kuzuia kuwabebesha mizigo mikubwa wanyama, kuzuia uuzaji wa pombe, nakadhalika. Wakati wa Makhalifa wanne polisi hawakuendesha mashitaka mahakamani.



Kuanzishwa kwa Magereza



Sambamba na kuwepo kwa polisi yalianzishwa magereza (jela) wakati wa Khalifa wa pili. Mwanzoni makosa ya jinai tu ndiyo yaliyowapeleka watu jela. Lakini siku zilivyosogea hata makosa kama kurudiarudia pombe yaliwapelekea walevi kufungwa badala ya kuchapwa bakora.


Masuala mengi kuhusiana na Dola kama vile kupanga mishahara ya wanajeshi, kuanzisha idara mbali mbali, kuwapa vibali wageni kufanya biashara katika Dola ya Kiislamu na kiwango cha kodi wanachotakiwa kulipa, n.k. yaliamuliwa na Khalifa baada ya kushauriwa na kamati yake ya utendaji. Kamati hii ilikuwa ikikutana kila siku katika msikiti wa Mtume (s.a.w). Taarifa za wilayani na mikoani zilizowasilishwa kwa Khalifa zilijadiliwa na kupitishiwa maamuzi.


Baadhi ya wanakamati wa kamati hii ya utendaji walipewa nyadhifa mbali mbali; kwa mfano – Abubakar alimteua β€˜Umar kuwa Jaji Mkuu na msimamizi wa kugawa zaka. Ali aliteuliwa kuwa mkuu wa mawasiliano; kusimamia wafungwa wa kivita, fidia yao na n.k.


Mbali ya shura teule, makhalifa wote walitumia shura ya watu wote msikitini kama chombo cha kusaidia uendeshaji. Uteuzi wa majaji, wakuu wa mikoa, n.k. ulifanywa hadharani (msikitini) ili kama kuna upinzani wowote juu ya mteuliwa, raia walikuwa huru kupinga kwa hoja wazijuazo. Si hivyo tu hata kama kiongozi ameteuliwa bado raia walikuwa na fursa ya kuwasilisha malalamiko dhidi ya kiongozi muhusika.


Ili kujua ukweli na malalamiko ya watu na kufanya uchunguzi, Tume ya kufuatilia malalamiko ya raia dhidi ya viongozi wao iliundwa. Malalamiko yalipomfikia Khalifa,aliitwa kiongozi muhusika kwa kuhojiwa au tume ilimuendea.


Chombo kingine cha utawala kilikuwa mkutano wa watendaji wote wa Serikali waliokuwa wanakutana baada ya Hija. Wakati huu Khalifa alikuwa anamsikiliza kila mwenye malalamiko dhidi ya Serikali. Kwa namna hii kila mwananchi alihusika na uendeshaji.


Si hivyo tu bali Khalifa Uthman alianza utaratibu wa kusikiliza malalamiko ya wananchi kila Ijumaa. Jambo lingine muhimu katika uendeshaji ni kuwa Serikali ilitoa mishahara iliyokidhi mahitaji ya watendaji ili kuzuia rushwa na mambo yanayolingana.


Kama ilivyokuwa wakati wa Mtume(s.a.w) kuitawala Dola iligawanywa kwenye majimbo na wilaya. Idadi ya majimbo na wilaya ilitegemea kupanuka kwa mipaka ya Dola. Kila jimbo au wilaya ilikuwa na viongozi watatu. Gavana au Walii, mkusanyaji mapato ya Serikali (Amil) na mwanasheria (Kadhi). Gavana alifanya kazi zote za Khalifa mkoani kwake. Aliendesha swala za kila siku ya Ijumaa, Idi zote mbili, na kuongoza msafara wa Hija wa watu wa mkoa wake. Alisimamia amani na utulivu mkoani kwake, pale ambapo kamanda wa kijeshi wa mkoa hakuwepo mkuu wa mkoa ndiye aliyejaza nafasi hiyo na kuwa kamanda wa majeshi ya mkoa na mara nyingine kuongoza mapigano dhidi ya maadui.


Pamoja na Gavana viongozi wengine waliokuwa mkoani ni Sheikh Ul-Kharaj au msimamizi wa mapato ya Serikali. Sahib Ahdath (mkuu wa polisi), Kadhi na Kamanda wa majeshi. Wakati wa ukhalifa wa Umar kiongozi alipoteuliwa aliorodhesha mali zake na itapoonekana anaongezeko lisiloeleweka aliulizwa na mali yake kutaifishwa.





                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 578

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰3 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰4 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Vita vya uhudi

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kusilimu kwa Wachawi wa Firaun

Mawaziri waliokuwa washauri wakuu wa Firauni wakataka wakusanywe magwiji waliobobea katika uchawi nchi nzima, kisha wapambanishwe na Nabii Musa(as).

Soma Zaidi...
Historia ya Watoto Wawili wa Nabii Adam

β€œNa wasomee khabari za watoto wawili wa Adam kwa kweli, walipotoa sadaka, ikakubaliwa ya mmoja wao na ya mwingine haikukubaliwa Akasema (yule asiyekubaliwa sadaka yake): β€œNitakuua”.

Soma Zaidi...
MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AANALELEWA NA BABU YAKE MZEE ABDUL-ALMUTALIB AKIWA NA UMRI WA MIAKA SITA (6)

KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee β€˜Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana.

Soma Zaidi...
Umuhimu wa jihad katika kusimamisha uislamu katika jamii

Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...