Chanzo cha Mapato katika serekali ya Kiislamu wakati wa Makhalifa

Chanzo cha Mapato katika serekali ya Kiislamu wakati wa Makhalifa

Pato la Serikali



Moja ya shughuli muhimu katika uendeshaji wa Serikali ni namna Serikali ilivyopata mapato yake na ilivyotumia. Wakati wa Mtume(s.a.w) vyanzo vya pato la Serikali vilikuwa zaka, jizya, kharaj, khums na fay. Katika kipindi cha makhalifa wanne vyanzo vya pato la Serikali viliongezeka kama ifuatavyo;


Ushr; Ushr ni kodi ya mazao kutoka katika ardhi ya Waislamu iliyotekwa kivita na kugawiwa askari waliopigana au ardhi ya Serikali iliyoandaliwa kwa kilimo au mifugo. Kwa ardhi inayotegemea mvua ya asili, mabwawa na mito ya asili kima chake ni 1/10 (10%) ya mazao na kwa mashamba yanayomwagiliwa kiwango cha ushuru ni 1/20 (5%) ya pato la mwaka.


Kharaj au kodi ya Ardhi: Kodi hii iliwahusu wasio waislamu ambao ardhi yao ilitekwa kivita lakini wenyewe wameruhusiwa kuedelea kutumia ile ardhi iliyotekwa ambayo ni mali ya dola ya Kiislamu. Kodi hii iliwekewa kima maalum baada ya tathmini ya ardhi na ililipwa kwa mwaka.


Jizya; ilikuwa chanzo kingine cha pato la Taifa. Kodi hii iliwahusu wasio waislamu tu, waliojulikana kwa jina la 'Dhimmi'. Serikali ya Kiislamu inachukua dhamana ya kuwalinda wasio Waislamu, wao na mali zao. Wasio Waislamu wanalipa kodi hii ya jizya ikiwa ni malipo ya kazi ya ulinzi wanayofanyiwa na Serikali. Kodi hii pia iliwekewa kiwango maalum na haikuwahusu vikongwe, watoto, walemavu na wanawake.


Zaka na Sadaqa nazo zilibakia kuwa vyanzo vya msingi vya pato la Serikali.


Ngawira ni mali inayopatikana kwa kumshinda adui. Hii nayo ilitumika kama chanzo cha pato la Serikali. Wapiganaji walichukua
asilimia 80 au (4 /5) na pato la serikkali lilikuwa asilimi 20 au ( 1/5) ya ngawira.


Fay kilikuwa ni chanzo kingine cha pato la Serikali katika kipindi cha Makhalifa. Fay ni mali iliyotolewa na adui hata bila ya kupigana.


Zaraib ni kodi za muda zilizotozwa na serikali kwa maslahi ya nchi
Mapato mengine ya Serikali yalitokana na wakfu, kodi za madini,kodi ya mali inayoingia nchini au inayopitishwa, n.k.


Kwa vyanzo hivi Serikali iliweza kukusanya mapato yaliyowezesha kuendesha Serikali bila matatizo. Palikuwa na Baitil-Mali(Hazina). Mali ya Serikali ilitumika kwa mujibu ya maelekezo ya mafungu yake, maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla.


Maendeleo ya nchi yaliyopatikana wakati wa Makhalifa ni pamoja na ujenzi wa mifereji(Canals). Katika Ukhalifa wa 'Umar(r.a)ulijengwa mfareji kutoka mto Euphrates hadi Basra kuliko kuwa na ukame wa maji. Mfreji huu uliitwa kwa jina la Gavana wa Basra, 'Canal Abi Musa'. Mifereji mingine iliyojengwa kutoka Mto Euphrates ni 'Canal Maakal na Canal Saad' iliyopeleka maji sehemu mbali mbali zilizokuwa kame.


Mfereji mwingine maarufu ni ule uliounganisha mto Nile na Red See (Bahari ya Shem) ambao uliitwa kwa jina la 'Canal Amirul-Muuminina'.


Maendeleo mengine yaliyofanywa kutokana na pato la Serikali katika kipndi cha Makhalifa ni ujenzi wa barabara na madaraja, majengo ya ofisi, nyumba za wafanyakazi,ngome na kambi za jeshi, nyumba za wageni, majengo madhubuti ya Baitul- Mali na magereza. Visima na vituo kadhaa baina ya Makkah na Madina vilijengwa. Miji nayo ilianzishwa na maarufu katika hiyo ni Basra, Kufa, Fustat na Mosul.


Kazi ya ujenzi wa misikiti na upanuzi wa misikiti ya Makkah na Madinah ilishamiri katika kipindi cha Makhalifa. Misikiti elfu nne (4,000) inakadiriwa kujengwa katika Ukhalifa wa 'Umar(r.a). Misikiti ya Makkah na Madina ilipanuliwa kwa kununua nyumba za majirani katika kipindi cha 'Umar na 'Uthman(r.a).




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 204

Post zifazofanana:-

MAZINGIRA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Mchango wa Waislamu Katika Kuleta Uhuru Tanganyika
i. Soma Zaidi...

DATSA LA KUJIFUNZA KUHUSU QURAN NA SUNNAH
Soma Zaidi...

siku za kupata mimba
Makala hii inakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba na dalili za siku hizo. Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki katika quran
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Kisamvu
Soma Zaidi...

KITABU CHA MATUNDA
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

Adabu za kusikiliza quran
ADABU ZA KUSIKILIZA QURANI 1. Soma Zaidi...

haki za mwanamke za kisiasa katika uislamu
Haki ya Kushiriki Katika Siasa. Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMAN
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu maji, kazizake mwilini na athari za upungufu wake mwilini
Hpa utafahamu faida za maji mwilini pamoja na athari za upungufu wa maji mwilini na dalili zake Soma Zaidi...

Kulaaniwa Bani Israil
Pamoja na kuteuliwa na Allah(s. Soma Zaidi...