Chanzo cha vita vya Ngamia Vita Kati ya Bibi Aisha na Khalifa Ali

Chanzo cha vita vya Ngamia Vita Kati ya Bibi Aisha na Khalifa Ali

Vita Kati ya Bibi Aisha na Khalifa Ali



Khabari za kutekwa Basra zilimchukua kwa mshangao mkubwa Khalifa Ali ambaye alikuwa aende Syria kumrudi Muawiya lakini alilazimika kwenda Basra kwanza kutuliza hali ya kule.


Alipofika Dhi-Qarโ€™a mahali karibu na Basra-alituma ujumbe kwa Aisha, Talha na Zubeir wafanye mazungumzo ya amani. Nafasi ilipatikana mazungumzo yakafanywa na wakawa karibu kukubaliana baada ya Ali kuahidi kuwa atawaadhibu wauwaji wa Uthman Dola itakapokuwa na amani. Lakini mpango wa amani haukuwa na maslahi kwa lile kundi la Ibn Sabaa ambalo lilifanya sehemu ya jeshi la Ali.


Walinongโ€™onezana kuwa Ali anataka kufikia makubaliano ya amani na ameahidi kuwaadhibu waliomuua Uthman. Kundi hili lilikuwa ndilo lililomuua Khalifa Uthman halikupendezwa na mpango huu, wakaunda hila iliyochochea kutokea vita. Mbinu mbili walizitumia. Kwanza walipeleka umbea Basra kuwa Ali akiingia Basra atawafanya watumwa wakazi wote na atawaua vijana wote. Kwa sababu hii watu wa Basra lazima wapigane.66 Ibn Sabaa na wachochezi wake usiku usiku walivamia jeshi la mama Aisha ambaye aliarifiwa na kwa namna hii vita vikaanza. Vita hivi vinajulikana kwa jina la Vita vya ngamia.


Vita vilikuwa vikali kwa vile ukubwa wa jeshi ulilingana. Baada ya mapigano makali na kuuawa Waislamu wapatao elfu kumi, Talha aliuwawa na , Zubair aliacha kupigana na akawa anaelekea Madina ndipo akauliwa njiani. Wakati wote wa vita mama Aisha alikuwa katika sehemu ya uwanja wa vita akiwa amepanda ngamia. Kuwepo kwake kulifanya mapigano yaendelee kwa kasi kubwa, bila kukoma, ndipo Ali alipoamuru ngamia wake akatwe miguu ya nyuma. Ngamia aliangukia miguu yake ya mbele na kwa heshima zote akatolewa mama Aisha ndani ya kikalio cha ngamia na vita vikaisha. Mama Aisha akasindikizwa Madinah na kaka yake Muhammad bin Abubakar.


Baada ya vita, Ali alizungumza na Waislamu katika msikiti wa Basra na Waislamu wakampa mkono wa utii. Alipoondoka alimuacha Abdallah bin Abbas kuwa Gavana wa Basra.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1446

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰2 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰3 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰4 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Ukasha bin Mihsan ni Sahaba aliyechangamkia Fursa

Katika somo hili utakwnda kujifunz anamna nambavyo Sahaba Ukasha alivyochangamkia fursa katika mambo ya heri

Soma Zaidi...
Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao

Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a.

Soma Zaidi...
Hatua mbili kuu za kushuka kwa Quran

Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Yusufu(a.s)

โ€œKwa yakini katika (kisa cha) Yusufu na ndugu zake yako mazingatio mengi kwa wanaouliza (mambo wapate kujua)โ€.

Soma Zaidi...
Mji wa Makkah na kabila la kiqureish

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mtume Muhammad s.a. w amelewa na Baba yake mdogo

Historia na sura ya Mtume Muhammad, sehemu ya 10.

Soma Zaidi...